Tunataka kuhakikisha kwamba wasafiri na madereva wana zana za kuwasaidia wawe salama wanapotumia huduma zetu. Ili kukusaidia upate usaidizi unaouhitaji wakati wa dharura, unaweza ukapiga simu kwa 911 kupitia programu ya Uber. Panapowezekana, tutatuma maelezo ya mahali ulipo na taarifa nyingine za safari kwa mhudumu wa 911. Maelezo ya safari tutakayotuma ni pamoja na kisio la mahali ulipokuwa ulipopiga simu kwa 911, muundo, rangi na namba pleti ya gari, jina lako na namba yako ya simu, eneo la kuchukuliwa na la kushukishwa pamoja na jina la dereva wako.
Ni wewe utakayeamua ikiwa ungependa kutuma maelezo ya mahali ulipo na taarifa nyingine za safari kwa mhudumu wa 911. Unaweza ukazima chaguo la kuonesha mahali ulipo na maelezo mengine kwa kufungua ukurasa wa Kutuma Data ya Dharura katika Mipangilio ya Faragha ya programu yako.
Maelezo ya mahali ulipo tunayotuma kwa mhudumu wa 911 yanatokana na longitudo na latitudo ya mahali ulipo, jinsi zinavyobanishwa na mfumo wa uendeshaji wa simu yako unapopiga simu. Maelezo ya mahali ulipo yanayotolewa na simu yako huenda yasiwe sahihi, hasa katika maeneo ya miji yenye watu wengi.
Unapochagua kutuma maelezo ya mahali ulipo na maelezo mengine ya safari kwa mhudumu wa 911, tutatuma maelezo ya mahali ulipo na taarifa za safari kwa RapidSOS, ambayo hutoa mfumo wa teknolojia unaotuwezesha kutuma data kutoka simu zilizo kwenye mtandao kwa wahudumu wa 911. Mfumo wa dharura wa RapidSOS unaweza tu ukatumiwa na wahudumu wa 911 katika baadhi ya maeneo ya Marekani tunapohudumu. Ikiwa hatuwezi kutuma maelezo ya safari yako kwa mhudumu wa 911, utaona arifa kuhusu hilo kwenye programu ya Uber kabla hujapiga simu kwa 911. Wakati mwingine, vituo vya kupokea simu za 911 na RapidSOS vinaweza kuchakata baadhi tu ya maelezo, wala si maelezo yote ya mahali ulipo na taarifa za safari. Kwa mfano, mhudumu wa 911 anaweza akaona kisio la mahali ulipo lakini huenda asione eneo ulipochukuliwa wala utakaposhukishwa.
Ili tukulinde, Uber itahifadhi maelezo ya mahali ulipo na taarifa za safari pamoja na maelezo ya wakati ulipotumia programu kupiga simu kwa 911. Uber inaweza ikaweka maelezo haya kwa muda unaoruhusiwa na sheria, baada ya hapo maelezo hayo yatafutwa. RapidSOS itafuta maelezo ya mahali ulipo na data ya safari baada ya siku 180, lakini inaweza ikaweka muhtasari wa maelezo yanayoonesha kiasi na idadi ya simu inazochakata. Muhtasari wowote wa maelezo yanayowekwa na RapidSOS hautajumuisha vipengele vya utambulisho ili usiweze kumtambulisha mtu yeyote. Uber na RapidSOS hazitawahi kurekodi au kusikiliza simu unazopiga kwa 911 wala kutoa nukuu za simu unazopiga.
Chagua lugha ambayo unapendelea
Kuhusu