Sera ya Kutobagua ya Uber
Uber imejizatiti kutoa ufikiaji wa machaguo ya huduma ambayo ni jumuishi, ya kuaminika na yenye ubora wa juu kwa kila mtu. Kwa hivyo Uber na washirika wake wanakataza ubaguzi dhidi ya watumiaji kwa msingi wa mbari, kabila, rangi ya ngozi, umri, ulemavu, utambulisho wa kijinsia, hali ya ndoa, ujauzito, asili ya kitaifa, dini, jinsia, mwelekeo wa kingono, lugha, eneo la kijiografia au sifa nyingine yoyote inayolindwa kwa mujibu wa sheria husika. Ubaguzi huo unajumuisha, lakini si tu, mtumiaji yeyote anayekataa kutoa au kukubali huduma kulingana na sifa yoyote kati ya hizi au kumkadiria mtumiaji mwingine kulingana na sifa yoyote inayolindwa.
Ubaguzi kwa msingi wa ulemavu unaweza kujumuisha kukataa kumbeba msafiri aliye na mnyama wa huduma au vifaa vya usaidizi, ikiwa vimewekwa katika Sera ya Mnyama wa Huduma na Kifaa cha Usaidizi ya Uber.
Ubaguzi kwa msingi wa eneo la kijiografia haujumuishi dereva au msafirishaji wa bidhaa anayekataa safari ambayo haimfai, lakini kukataa au kughairi maombi kwa makusudi au kutumia vipengele kwenye Tovuti ya Uber Marketplace ili kuepuka kupokea maombi ya safari au usafirishaji wa bidhaa, kwa ajili tu ya kuepuka kitongoji fulani kwa sababu ya sifa za watu au biashara iliyo katika eneo hilo, hakuruhusiwi.
Mtumiaji yeyote anayepatikana kuwa amekiuka marufuku hii atapoteza uwezo wa kuingia kwenye tovuti ya Uber. Sheria zinazotumika katika mamlaka fulani za kisheria zinaweza kuhitaji na/au kuruhusu utoaji wa huduma na kwa manufaa ya aina mahususi ya watu. Katika mamlaka hizo za kisheria, huduma zinazotolewa kwa kufuata sheria hizi na masharti husika zinaruhusiwa kwa mujibu wa sera hii.