관할 지역 선택:
미국
언어 선택:
스와힐리어(탄자니아)
Last modified: 12/1/2020
Sera ya Uber ya Kutobagua
Uber inajitahidi kuhakikisha kwamba chagua salama, aminifu, na za ubora wa juu za usafirishaji zinapatikana kwa kila mtu. Kwa hivyo, Uber na washirika wake wanapiga marufuku ubaguzi dhidi ya wasafiri au madereva kwa msingi wa mbari, dini, asili ya kitaifa, ulemavu, mwelekeo wa kijinsia, hadhi ya ndoa, utambulisho wa kijinsia, umri au sifa nyingine yoyote iliyolindwa chini ya sheria husika za kitaifa au jimbo. Ubaguzi huo unajumuisha, lakini sio tu, kukataa kutoa au kukubali huduma kwa msingi wa sifa zozote kati ya sifa hizi. Msafiri au dereva yeyote anayepatikana kukiuka marufuku haya hataweza kufikia jukwaa la Uber.
선호하는 언어 선택