Sera ya Maudhui Yanayoletwa na Mtumiaji
Huenda Uber, kwa hiari yake pekee, ikakuruhusu mara kwa mara kuwasilisha, kupakia, kuchapisha au vinginevyo ukapeana kwa Uber maudhui na taarifa za kimaandishi, sauti, na/au picha za Huduma, ikijumisha maoni husiani na Huduma hizi, kuanzishwa kwa maombi ya usaidizi, na wasilisho la ushiriki katika mashindano na tamasha za ukuzaji (“Maudhui ya Mtumiaji”). Huenda Uber, kwa hiari yake pekee, ikaondoa, ikarekebisha au ikazima Maudhui ya Mtumiaji kwa sababu yoyote, ikiwa ni pamoja na iwapo Uber itabaini kwamba Maudhui ya Mtumiaji yanakiuka Makubaliano haya. Uber haitawajibikia lolote au kugharamia Maudhui ya Mtumiaji, kwa kuyaondoa, au kutoyaondoa au Maudhui mengineyo. Uber haikagui kimbele Maudhui yote ya Mtumiaji na haikubalii au kuidhinisha Maudhui yoyote ya Mtumiaji yaliyoko kwenye Huduma hizi.
Maudhui yoyote ya Mtumiaji uliyotoa yanasalia kuwa mali yako. Hata hivyo, kwa kupeana Maudhui ya Mtumiaji kwa Uber, unaipa Uber leseni ya kote ulimwenguni, ya milele, isiyoweza kubatilishwa, inayoweza kuhamishika, leseni isiyolipiwa mrahaba, ikiwa na haki ya kupeana leseni ndogo, ya kutumia, kunakili, kurekebisha, kuunda kazi zinazofanana, kusambaza, kuonyesha hadharani, kufanyia maonyesho hadharani, na vinginevyo kutumia kwa njia yoyote Maudhui hayo ya Mtumiaji katika mifumo na mbinu zote za usambazaji zinazojulikana sasa au zitakazovumbuliwa baadaye (ikijumuisha zinazohusiana na Huduma na biashara ya Uber na kuhusu tovuti na huduma za vyombo vingine), bila ya ilani za ziada kwako au ridhaa kutoka kwako, na bila ya hitajiko la kukulipa wewe au mtu au chombo kingine.
Unawakilisha na kuhakikishia kwamba: (i) aidha wewe ni mmiliki wa kipekee wa Maudhui yote ya Mtumiaji au una haki, leseni, ridhaa na vibali vyote vinavyohitajika ili kuipa Uber leseni ya Maudhui ya Mtumiaji kama ilivyoelezwa hapo juu; na (ii) Maudhui ya Mtumiaji wala wasilisho, upakiaji, uchapishaji wako au vinginevyo kufanya Maudhui hayo ya Mtumiaji kupatikana wala utumizi wa Uber wa Maudhui ya Mtumiaji kama ilivyoruhusiwa hapa kutakiuka, kutumia vibaya au kukiuka haki miliki au haki za mali, au haki za utangazaji au faragha za chombo kingine, au kusababisha ukiukaji wa sheria au kanuni yoyote husika.
Unapofikia au kutumia Huduma hizi, unakubali kwamba:
- Hutakiuka sheria, amri au kanuni yoyote.
- Hutahitilafiana na au kukatiza Huduma hizi au seva yoyote kuu au mtandao unaotumika kusaidia au kutoa Huduma, ikijumuisha udukuzi wa Huduma hizi.
- Hutatumia programu yoyote ambayo huharibu, huhitilafiana na au kukatiza Huduma hizi au kompyuta au mali ya mtu mwingine, kama vile mashambulizi ya kukatiza huduma, barua taka, udukuzi, au upakiaji wa virusi vya kompyuta, programu hasidi kwa ujumla na faili vurugu.
- Kutumia Huduma hizi kuudhi, kukasirisha, kusumbua, au kuharibu mali, kwa mfano kutumia lugha chafu au lugha ya kudhulumu, kutumia matusi, au baruapepe taka, kwa yeyeto yule anayetumia Huduma hizi. Lugha ya chuki haikubaliki.
- Kuchangia Maudhui ya Mtumiaji au kupanga au kushiriki katika harakati zozote, kikundi au muungano usiofaa, wenye matusi, unaodhulumu, usioheshimu, unaotishia, wenye chuki, unaoudhi, wenye lugha chafu, unaoashiria ngono hadharani, unaochafuliana jina, unaokiuka, unaoingilia usiri wa mtu mwingine, au vinginevyo unaoweza kuchukiza.
- Kuchapisha, kutuma, kupakia au kusambaza Maudhui ya Mtumiaji ambayo si halali au usio na idhini ya kusambaza, ikijumujisha taarifa za kibinafsi za mtu mwingine.
- Kuchapisha, kutuma, kupakia au kusambaza maudhui yoyote ambayo Uber (ikitenda kwa ubusara na kuzingatia malengo) itabainisha kuwa hayafai, ni yenye matusi, ni yenye chuki, yanayodhulumu, yasiyo na heshima, yanachafulia mtu sifa, yenye kutishia, ni yenye chuki, ya lugha chafu, yanayoashiria ngono hadharani, yanayokiuka, yanayoingilia usiri, yenye lugha chafu, yenye kuudhi, machafu au yasiyo ya kisheria.
- Kuchapisha ujumbe wowote kwa kusudu lolote kando na la mawasiliano ya kibinafsi. Jumbe zilizopigwa marufuku zinajumuisha matangazo ya kibiashara, baruapepe taka, barua mfululizo, miradi ya piramidi na utafutaji mwingine au shughuli zingine za kibiashara.
- Kujifanya kuwa mtu mwingine au kudanganya kuwa wewe ni mfanyakazi wa Uber, Mbia au mwakilishi wa Uber.
- Kutumia vibaya usiaidizi wa ndani mwa programu au vitufe vya kuzua malalamiko au kupeana ripoti zisizo za kweli kwa wafanyakazi wa Uber.
- Kujaribu kupata, au kudukua, nenosiri, taarifa za akaunti, au taarifa nyingine za kibinafsi kutoka kwa yeyote yule anayetumia Huduma hizi.
- Kutumia roboti yoyote, programu ya kudukua au vyombo vingine au taratibu zongine otomatiki kufikia Huduma hizi kwa madhumuni yoyote au kunakili nyenzo zozote kutoka kwa Huduma hizi.
- Kujaribu kutumia Huduma hizi kwenye au kupitia kwa huduma yoyote ambayo haijathibitiwa au kuidhinishwa na Uber.
- Kukuza, kuhamasisha au kushiriki kwenye shughuli zozote zilizopigwa marufuku zilizoelezewa hapa juu.
Iwapo wewe au mtu anayetumia Akaunti yako atakiuka Makubaliano haya, atakosa kusuluhisha ukiukaji huu baada ya kuonywa, huenda Uber ikachukua hatua dhidi yako, ikijumuisha kubatilisha ufikiaji kwenye baadhi au Huduma zote, au kufunga Akaunti yako. Katika hali ya ukiukaji mbaya zaidi, huenda Uber ikachukua hatua hizi bila kukupa onyo la awali. Ikiwezekana, Uber itakufahamisha kuhusu hatua itakayochukua kama adhabu ya ukiukaji wa sheria hizi au ukiukaji wa Sera hii.
Huenda Huduma Fulani za Uber zikaweka sheria za ziada ambazo zinatumika katika mwenendo wako kwenye hizo huduma.
Iwapo utakumbana na Mtumiaji mwingine ambaye anakiuka sheria yoyote kati ya hizi, tafadhali ripoti kisa hicho kwa Uber kwa kutuma baruapepe kwa profilenotice@uber.com.
Huenda Uber, kwa hiari yake pekee, ikafuatilia au kurekodi shughuli za mtandaoni au Maudhui kuhusu Huduma hizi na huenda ikaondoa Maudhui yoyote kutoka kwenye Huduma yoyote kwa hiari yake pekee. Kumbuka kwamba mawasiliano na Maudhui yako ya Mtumiaji kwenye Huduma zozote ni ya umma na yataonekana na watu wengine.
Rólunk