
Siku ya wanawake duniani ni zaidi ya siku ya kusheherekea wanawake mashuhuri duniani waliofanya mambo makubwa. Kwetu sisi ni harakati ya kusherehekea uwezo wa wanawake kwenda popote kwa uhuru. Kuendesha gari sio tu njia ya kufika kazini, inaweza kuwa kazi. Kwa wanawake duniani kote, Uber inakupa kitu tofauti: fanya kazi utakavyoweza, mdaa wowote unaotaka. Madereva wanaweza kutengeneza ela kwa jinsi wanavyotaka na kwa ratiba yao wenyewe.
Tunajivunia kuwatambulisha baadhi ya wanawake wa Uber ndani ya Tanzania:

“Hamasa yangu ni kukutana na watu wapya na kuwajua zaidi.Napenda kutumia mda wangu wa ziada kupika na kuwa pamoja na niwapendao”. - Prisca

“Siku zote ninapenda kuwa huru na kutembea sehemu mbalimbali duniani na hicho ndicho kinachonipa hamasa. Mda wangu wa ziada napenda kusoma vitabu na kujifunza vitu vipya. Ni uhuru nilionao katika biashara yangu unaonifanya nipende kufanya kazi hii”. - Irene

“Napata hamasa kutoka kwenye maisha ya kila siku nikitambua kua wote tuna kusudi la kutimiza na kuna vingi vya kujifunza. Natumaini kuwa bora zaidi na kuleta hamasa kwa wengine na Uber ni mwanzao wa kufikia malengo hayo”- Janeth
Heri ya Siku ya Wanawake Duniani,
Uber Tanzania
Posted by Uber Editor
Get a ride when you need one
Start earning in your city
Get a ride when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular

Uber’s Journey to Ray on Kubernetes: Ray Setup

Case study: how Wellington County enhances mobility options for rural townships

Uber’s Journey to Ray on Kubernetes: Resource Management
