Nauli tangulizi na uidhinishaji wa malipo kabla ya kumaliza safari yako ya Uber
9 Februari 2017 / Tanzania
Hapa Uber, sisi daima hujitahidi kadri tuwezavyo ili kukupa huduma bora inayodumu, kuanzia pale unapoagiza usafiri hadi utakapowasili sehemu unayokwenda. Ndiyo maana tuna msisimko mkubwa kutangaza kuzinduliwa kwa mfumo wa nauli tangulizi hapa nchini Tanzania!
Kukiwa na utambuzi wa awali wa nauli, unachohitajika kufanya ni kuchagua sehemu ya kuchukuliwa na eneo la kushukia, na kifaa hiki kipya kitakuonyesha bei ya safari hiyo. Nauli tangulizi huhesabiwa kwa kutumia muda unaotarajiwa na masafa ya safari hiyo, hali ya magari barabarani, pamoja na uwepo kwa madereva-washirika wetu. Kwa njia hii, wakati wowote utaweza kuamua usafiri unaokufaa kuambatana na bajeti yako.
Ni rahisi, Chagua tu sehemu ya kuchukuliwa na eneo la kushukia, na utazame nauli ya uhakika inayoonyeshwa kwenye programu. Pindi utakapo kamilisha safari yako, hatimaye utapokea stakabadhi inayoonyesha nauli yako tangulizi. Iwapo utasimama sehemu mbali mbali au ilikubidi ubadilishe mwelekeo wa safari baada ya kufikia nusu ya safari yako, usiwe na wasiwasi! Tutarejesha Ukadiriaji wa nauli wa awali kwa ajili ya safari hio ikizingatia muda na umbali wa safari hio.
Kutokana na kuzinduliwa kwa mfumo huu wa nauli tangulizi, utashuhudia mabadiliko kidogo. Sawa tu na jinsi ambavyo mahoteli yanavyowalipisha wageni wao, Uber sasa inaidhinisha malipo yako ya njia isiyo ya pesa taslimu kwa safari unayoagiza, kwa kiasi kile cha Nauli tangulizi. Wakati wa kuanza safari, Uber wanaweza kuweka idhini ya muda ya kushikilia makato ya nauli yako tangulizi. Hii itaonyeshwa kama malipo yaliyo katika hali ya “kusubirishwa” katika akaunti yako.
Wakati safari inapokamilika, hii hali ya kusuburishwa inabadilishwa kuwa ada ya kutozwa kufidia nauli ya safari hiyo. Iwapo safari imeghairishwa au jumla ya nauli ni tofauti na bei iliyotolewa awali, ile idhini ya awali iliyozuiwa inastahili kuondolewa kutoka kwa akaunti yako, lakini kulingana na sera za benki yako hii inaweza ikachukua muda wa siku chache.
Ikiwa ungependa kuthibitisha jambo maalum katika taarifa yako ya benki, tafadhali wasiliana na benki yako moja kwa moja.
MASWALI YAULIZWAYO MARA KWA MARA:
Je, kwa nini tunatekeleza mfumo huu?
Unapokwenda kuagiza tiketi ya ndege au chumba cha kulala hotelini, huwa unajulishwa bei kwanza kabla ya kununua. Hakuna hesabu za kutatiza wala kushtukizwa– ndio maana tuliona mwelekeo huu kuwa wa muafaka kwa Uber.
Je, ongezeko la bei litajumlishwa kwenye mfumo huu wa nauli tangulizi?
Ndiyo, ikiwa kuna abiria wengi wanaoagiza magari kuzidi madereva tulio nao, nauli itapanda kupitia. Bei anayoonyeshwa msafiri huwa imethibitishwa awali, na huwezi kuagiza usafiri bila ya kukubali gharama yake mwanzoni.
Je, kuna wakati nitalipishwa zaidi ya kiasi cha nauli tangulizi?
Ni nadra sana, kulipishwa muda wa kusubiri. Malipo ya muda wa kusubiri hutozwa zimalizikapo dakika 2 baada ya dereva kuwasili mahala ulipo ili kukuchukua, kwa hivyo wakati wote hakikisha kuwa uko tayari kuondoka wakati wa kufanya ombi lako la usafiri. Malipo ya muda wa kusubiri yataongezwa kwenye nauli yako tangulizi, na itaonyeshwa kama kipengele kwenye stakabadhi yako. Ikiwa mahali pa kuchukuliwa au pa kushukia pamebadilika, basi nauli yako itarejea katika ukadiriaji wa nauli wa awali ikizingatia muda na umbali wa safari hio.
Je, itakuwaje iwapo nahitaji kubadilisha mwelekeo wa safari yangu?
Unaweza kubadilisha kwa urahisi mwelekeo wa safari yako katika programu ya Uber. Wakati unapobadlisha mahali unapotarajia kwenda baada kufanya ombi, basi nauli yako huenda ikarejea katika ukadiriaji wa malipo yanayoambatana na muda na masafa.
Je, Ada ya Msafiri ni nini?
Ada ya msafiri ni gharama ambayo hutozwa kwenye safari iwapo safari yenyewe inatozwa kiingilio au malipo ya ziada kwa sababu ya matumizi ya barabara fulani. Ili kuwapa wasafiri wetu uzoefu unaofaa Zaidi, gharama hizi tayari zimejumulishwa katika nauli tangulizi..
Je, kuna mabidiliko ya jinsi nauli inavyohesabiwa?
Hapana. Nauli tangulizi huzingatia mambo yote ambayo kwa kawaida yanaweza kuathiri bei ya safari, ikiwemo muda, umbali, na foleni za barabarani, pamoja na kuzingatia wasafiri wangapi wanaomba usafiri na ni madereva wangapi walio katika eneo lililo karibu nawe. Badiliko la pekee ni kuwa sasa tunakuonyesha nauli yako tangulizi– hakuna mahesabu, hakuna kushangaa.
Ni kwa nini nilipokea arifa kutoka kwa benki yangu kabla ya safari kuanza?
Kushikilia idhini kutafanyika wakati unapoagiza usafiri wako. Baadhi ya benki huenda wakakutumia ujumbe wa SMS kuwa idhini ya kushikilia imetozwa kwa akaunti yako. Hata hivyo wakati mwingine hizi huwa sawa tu na gharama halisi – usiwe na wasiwasi, idhini iliyoshikiliwa na malipo yanaweza ikageuka kuwa malipo halisi au kubatilishwa na benki yako katika muda wa siku chache.
Ikiwa nitaagiza na kusafiri mara nyingi katika siku hiyo hiyo, nitapokea idhini za kushikilia mara nyingi pia?
Itategemea – ikiwa idhini ya kushikilia ya safari ya awali bado haijakamlishwa au kufutwa, hiyo hiyo idhini ya kushikilia inaweza kutumika kwa safari hizo nyingine. Hata hivyo, inawezekana kupokea idhini nyingi za kushikilia kwa siku hiyo hiyo iwapo idhini za awali tayari zimetumika.
Je, ni kwa nini kiasi cha idhini iliyoshikiliwa ni juu zaidi ya bei yangu ya nauli tangulizi?
Kwa sasa, idhini za kushikilia malipo ni ya gharama yote kamili ya safari, bila kujumulisha promosheni wala punguzo loloote. Hata hivyo usijali, wakati wowote ule utatozwa tu kiasi sahihi, na kiasi chochote cha malipo yaliyoshikiliwa ambacho kilisalia kitarudishwa kwako kupitia njia yako ya malipo.
Je, nitatofautisha vipi baina ya malipo yaliyoidhinishwa na malipo halisi?
Katika taarifa ya kadi yako ya benki, malipo yanastahili kuonyeshwa kuwa yanasubirishwa au yamebatilishwa, na hayatoanyeshwa kuwa yamelipwa. Ikiwa utahitaji ufafanuzi wa sera za benki yako kuhusu uidhinishwaji wa nauli, tunapendekeza uwasiliane moja kwa moja na benki yako.
Ni kwa nini niliombwa kuongeza njia nyingine ya malipo?
Hii inaweza kutokea iwapo kuidhinishwa kwa ushikilizi wa malipo haukufualu. Ikiwa kiasi cha Nauli tangulizi haipatikani kwetu kuishikilia, hutaweza kuitisha usafiri. Itokeapo hali hii, tunapendekeza kuongezwa kwa njia nyinginei ya malipo, au kufuatilia suala hilo na benki yako.
Je, nini hufanyika iwapo nitaghairi safari?
Ikiwa utaghairi safari kwa kuzingatia sera ya Uber ya Kughairi safari, hii idhini ya kushikilia malipo itabatilishwa mara moja, ijapokuwa itachukua siku kadhaa za kazi kwa tukio hili kuonyeshwa katika mfumo wako wa malipo.
Je, ilikuwaje nililipishwa mara mbili kwa safari hiyo moja?
Hili linaweza kutokea ikiwa utabadilisha mwelekeo wa safari yako wakati ukiwa safarini, kupelekea nauli yako kuwa juu zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa awali. Ikiwa idhinisho la pili la kushikilia malipo yote kamili halikufanikiwa, kiasi unachodaiwa kinaweza kugawanywa kwa stakabadhi mbili. Tafadhali wasiliana nasi kwenye tovuti yetu ya help.uber iwapo una maswali yoyote yanayohusu uidhinishwaji wa malipo.
Posted by Aisha
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
