
Kuanzia tarehe 27 Agosti 2021, tuliacha kupokea maombi ya sera ya msaada wa kifedha wa COVID. Ili upate nyenzo za ziada na maelezo mengine ya usalama, tafadhali tembelea ukurasa wa nyenzo za COVID.
Katika kipindi cha wiki chache zilizopita kumekuwa na changamoto kubwa kwa kila mtu. Lakini tunajua kwamba madereva kama wewe ndio walioathirika zaidi.
Ikiwa bado unaendelea na biashara yako ya kuendesha gari, au unaendelea kutoa huduma muhimu katika kipindi hiki kigumu—kwa mfano kuwasafirisha watendji muhimu kwenda kazini. Tumeanza kuwapa madereva vipukusi bure ili vikusadie kujilinda dhidi ya maambukizi ya Corona, na tumenunua mamilioni ya barakoa. Ingawa bidhaa hizi ni chache, tunafanya kila juhudi kuwafikishia madereva bidhaa hizi, tukianza na miji yenye uhitaji mkubwa. Tumezindua pia kituo cha COVID-19 Hub, huu ni ukurasa wenye taarifa na msaada muhimu zinazopatikana ndani ya app mahususi kwa ajili ya kupata taarifa za usalama kutoka kwa Uber.
Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, tumekuwa tukitoa msaada wa kifedha kwa madereva waliopimwa na kuthibitika kuwa na ugonjwa wa COVID-19 au walioagizwa na daktari au afisa wa afya kukaa kwenye karantini au kujitenga kwa kuhofiwa kuwa na maambukizi. Tumeharakisha utaratibu wa kubuni sera hii ingawa zoezi zima la kuharakisha sera hii ina maana kwamba hatukupata taarifa za kutosha, tulifanya hivi kwa sababu tulitambua umuhimu wa kuwa na mkakati wa kuwapa msaada madereva wanaotumia mfumo wetu haraka iwezekanavyo.
Tangu kuzinduliwa kwa mpango huu, tumepokea maoni kutoka kwa madereva ambao wamehoji kwamba mpango ulinuiwa kusaidia madereva wachache na mchakato wa kupata fedha hauko wazi na unawatatiza. Leo tumechukua hatua ya kufanya mabadiliko 2 muhimu:
1. Tunaweka msukumo mkubwa kwa madereva ambao wanaendelea kutoa huduma za usafiri wakati wa kipindi hiki kigumu.
2.Tunapanua wigo wa mpango huu ili uwafaidi madereva walioagizwa kukaa kwenye karantini kwa sababu wanaugua maradhi mengine yanayohatarisha afya yao iwapo watapata maambukizi ya COVID-19. Hii ina maana kwamba madereva wengi watafaidi ikilinganishwa na mpango wa awali, tumechukua hatua ya kuweka kiwango cha juu ambacho mtu anaweza kulipwa ili kusaidia mpango huu uwe endelevu.
Mpango huu utawafaidi madereva wote wanaotumia mfumo wa Uber nchini Tanzania kuanzia leo. Ikiwa wewe ni dereva anayeendesha gari la bosi, pesa hizi za msaada wa kifedha zinazotolewa chini ya mpango huu zitatumwa kwenye akaunti ya mmiliki wa gar. Kwa hiyo, unatakiwa kumwambia mmiliki wa gari akutumie pesa hizi punde tu akishazipokea.
Kutuma maombi ya msaada wa kifedha chini ya mpango huuu
Sifa za mwombaji; Lazima uwe na barua kutoka kwa daktari mwenye kibali au afisa kutoka wizara ya afya inayoonesha kwamba:
Umethibitika kuwa umeambukizwa ugonjwa wa COVID-19; au
Umeagizwa kukaa karantini kwa sababu ya kukisiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19; au
Umeagizwa kukaa karantini kwa sababu unaugua maradhi ambayo yanakuweka katika hatari kubwa iwapo utaambukizwa ugonjwa wa COVID-19
Unaweza kusoma maelekezo kuhusu utaratibu wa kutuma maombi ya msaada wa kifedha hapa. Ombi lako litachakatwa ndani ya siku 7 za kazi. Hakikisha unasoma kwa makini masharti yote yaliyoorodheshwa kwenye tovuti iliyotajwa hapo juu kabla ya kutuma maombi yako. Wakati unatuma maombi, akaunti yako ya Uber itafungwa kwa muda kama hatua ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19. Ingawa akaunti yako imefungwa kwa muda, bado tutathmini maombi yako ili kujiridhisha kama una sifa za kupata msaada wa kifedha.
Mabadiliko tunayotekeleza kwenye mpango wa msaada wa kifedha
Mpango wa Awali | Mpango Mpya | |
Sifa za mwombaji | Madereva wanaotuma maombi sharti wawe wamefanya angalau safari moja ndani ya kipindi cha siku 30 kabla ya tarehe 6 Machi, wakati mpango huu ulipotangazwa. | Uwe umefanya angalau safari moja ndani ya muda wa siku 30 kabla ya tarehe uliyowasilisha hati au siku uliyoiandikia Uber ukiomba msaada wa kifedha, haijalishi ni gani itakayotangulia. Tunatekeleza mabadiliko haya ili tuweke msukumo mkubwa kwenye madereva wanaoendelea kutoa huduma ya usafiri licha ya kuhatarisha maisha yao wakati wa janga hili. |
Kipindi kinachotumika kukokoyoa malipo | Tulikuwa tunatumia kigezo cha wastani wa mapato ya kila wiki kwa kipindi ha miezi 6 kabla ya tarehe 6 Machi kukotoa fedha za kumlipa dereva. | Tutazingatia wastani wa mapato yako ya kila wiki ndani ya kipindi cha miezi 3 kabla hujatuma maombi ya kutaka msaada wa kifedha. |
Kiwango cha juu cha fedha anazopata dereva | Msaada wa kifedha ulifidia hadi siku 14 kulingana na historia ya mapato ya dereva mahususi. | Ingawa tutaendelea kutoa msaada wa kifedha hadi siku 14, tumeweka kiwango cha juu ambacho dereva yeyote anaweza kupata. Kiwango hiki kinatofautiana kutoka jiji moja hadi lingine. |
Tunatambua kwamba utaratibu wa kuweka kiwango cha juu anachoweza kupata dereva yeyote kitawaathiri madereva wanaofanya safari nyingi, kwa sababu watapata pesa kidogo ikilinganishwa na kiasi ambacho huwa wanajiingizia katika siku za kawaida kabla ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19. Lakini kupitia kupanua wigo wa madereva wanaoweza kufaidi kutokana na mpango huu, ni matumaini yetu kwamba msaada huu wa kifedha utakuwa faraja kubwa kwa madereva wengi, wasafirshaji vyakula, na familia zao.
Tunapenda kukumbusha kwamba mpango wetu wa kuwalipa madereva kiasi cha chini cha TZS 25,000 ikiwa umekuwa ukitumia mfumo wetu kuendesha gari lako nchini Tanzania hata kama umefanya safari moja tu ndani ya siku 30 kabla ya kutuma maombi yako ya msaada wa kifedha.
Jamii zetu zinapozongwa na janga hili ambalo halijawahi kutokea kwa miaka mingi, tunatambua kazi yako na juhudi unayofanya kutoa huduma muhimu na tuko tayari kukupa usaidizi unaohitaji. Bila shaka tunajifunza mengi kadri muda unavyoenda. Kwa sababu hatuwezi kutabiri hali itakuwa vipi mwezi ujao, tutaendelea kusikia maoni yako, kutumia maoni haya, na kufanyia mapitio mpango wetu wa msaada wa kifedha ili kutekeleza mabadiliko muhimu.
Taarifa iliyo hapo juu inainisha mkakati wetu kote duniani wa kutoa msaada wa kifedha kwa madereva ambao watathibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 au watakaoagizwa na afisa wa wizara ya afya kukaa karantini. Kila nchi ina masharti yake yanayotakiwa ili kufuata sheria, kanuni, na miongozo ya biashara ya nchi husika kuhusu masuala kama vile hati za maafisa wa afya, maagizo ya afya ya umma, au kodi inayotozwa misaada ya kifedha. Makala haya hayajazungumzia masharti ya nchi mahususi, na Uber ina haki ya kubadilisha sifa na maelezo yaliyoainishwa hapo juu kwa mujibu wa masharti ya nchi mahususi. Kwa sababu hali ya ugonjwa huu inabadilika kwa kasi, tuna haki ya kubadilisha mkakati wetu, ikiwa ni pamoja na kiasi cha pesa kinacholipwa na utaratibu wa kuwachagua watakaofaidi kutokana na mpango huu kadri hali inavyoendelea kubadilika.
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
