
Dar es Salaam tumekuwa tukisafiri wote kwa miaka mitano (5) sasa, na imekuwa ni safari yenye mafanikio!
Ilianza kwa kubonyeza tu kitufe na kufika unakoenda, lakini tumetoka mbali tokea kipindi hicho. Umeturuhusu kushirikiana nawe katika wakati wako maalum, umetufikisha sehemu mbalimbali na zaidi ya yote tumeweza kujifunza kutoka kwako.
Imekua ni safari yenye matukio mengi mazuri, kuanzia kuwa na UberX peke yake mpaka sasa tuna bidhaa 6 na hii yote ni ndani ya miaka mitano (5) ;
- UberBODA (Boda) – Usafiri wa gharama nafuu, na hutumika mara nyingi mtu akiwa na haraka. Ina uwezo wa kubeba mpaka msafiri mmoja.
- UberConnect (Boda) – Hii imeanzishwa hivi karibuni, hutumika katika kufanya delivery ndani ya jiji la Dar. Na hii ni kwa mtu yeyote anaetaka kufanya delivery iwe biashara au mtu binafsi.
- UberPOA (Bajajj) – Usafiri wa gharama nafuu wenye uwezo wa kubeba wasafiri hadi watatu (3).
- UberX – Usafiri wa gari unaoweza kubeba hadi wasafiri wanne (4).
- Hourly – Msafiri anauwezo wa kukodisha usafiri kwa lisaa, hutumika mara nyingi pale mtu anapotaka kwenda umbali mfupi lakini vituo vingi, na
- UberXL – Gari yenye uwezo wa kubeba wasafiri 6- 7.
Sehemu mlizotupeleka katika kipindi hichi cha miaka mitano (5);
Ni mengi yametokea tangu Uber ilivyoingia Tanzania mwaka 2016, kuanzia maboresho ya programu (App), kuongezeka kwa vipengele vya usalama kwa dereva-mshirika na msafiri, ukuaji wa watumiaji wa programu na watu wengi zaidi kutegemea Uber katika shughuli zao za kila siku.
Uber sasa inapatikana katika kila kona ya mji na watu wanaomba usafiri katika sehemu hizo zote, na hii imetufanya tufikirie, watu hutumia Uber kwenye shughuli gani haswa? Kutoka kwenye survey tuliyofanya, tumepata “Top 5” ya shughuli zinazofanywa na watumiaji wa programu ya Uber;
- Safari za kwenda na kutoka ofisini
- Shopping
- Mitoko na kusalimia ndugu na jamaa
- Safari fupi na za haraka (hususani Boda)
- Kwenda kwenye vikao
Kwa miaka mitano (5) umetufundisha mengi, umetupeleka sehemu nyingi na zaidi ya yote umetutengenezea kumbukumbu! Tumefika hapa tulipo, na yote ni shukrani kwako.
Safari bado ndefu – hii ni kwa safari zijazo #UberTanzaniaTurns5
Posted by Monica Mziray
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
