Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi na Madereva Kuhusu Huduma Zetu Nchini Tanzania
15 Aprili 2020 / Tanzania
“Bila shaka wiki zijazo zitakuwa na changamoto kubwa kwa kila mtu na tunafahamu kwamba haitakuwa rahisi kwa madereva wengi kama wewe. Lakini tunapenda kukuhakikishia kwamba hali hii sio ya kudumu kwa muda mrefu na tunashirikiana na mamlaka za serikali na wadau wengine kwa niaba yako ili kuhakikisha kwamba unapata msaada unaohitaji katika kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja katika hili. ” – Alon Lits, Meneja Mkurugenzi wa Uber Kusini mwa Jangwa la Sahara
Swali: Je, ni hatua gani mtachukua nikithibitika kuwa na virusi vya COVID-19?
Madereva wanaothibitika kuwa na virusi vya COVID-19 au kutengwa kwa maagizo ya wizara ya afya watapata msaada wa kifedha kwa kipindi cha hadi siku 14.
Swali. Ni mara ngapi ninatakiwa kutumia sabuni maalum kusafisha gari langu?
Hakikisha unatumia sabuni maalum kama Dettol kusafisha gari lako baada ya kila safari.
Swali: Nitapata wapi vitakasa mikono kwa matumizi ndani ya gari langu?
Uber itawapatia madereva vitakasa mikono vyenye kiwango cha kileo (alcohol)
kisichopungua asilimia 60%. Hivi vitakasa mikono vitasambazwa katika vituo viwili, River Tower na Mikocheni. Utapokea ujumbe wa SMS na msimbo, utakaokuambia siku uliyopangiwa kuchukua vitakasa mikono vyako.
Swali. Je, kuna ushauri wowote wa afya ninaotakiwa kuzingatia?
Usiendeshe gari lako kama unajihisi mgonjwa.
Ikiwa unaendesha gari lako:
Tumia barakoa (mask) kufunika kinywa na pua yako. Hakikisha unatumia kiwiko chako au kitambaa safi kufunika kinywa chako unapopiga chafya au kukokohoa.
Hakikisha wasafiri wanatumia kiti cha nyma ili kuepuka kugusana.
Teremsha vioo vya gari.
Tumia vitakasa mikono kuosha mikono yako mara kwa mara na uhakikishe unatakasa sehemu za gari lako baada ya kila safari.
Swali: Ni hatua gani nayopaswa kuchukua nikiona kwamba msafiri ni mgonjwa?
Iwapo dereva hatokuwa na amani kumchukua abiria kwa kuhofia usalama wake, anaweza kutokubali ombi la safari au kughairi safari. Hata hivyo, ni kinyume cha Mwongozo wa Jumuiya ya Uber kumbagua mtu yeyote kwa misingi ya rangi au utaifa wake.
Swali: Je, kuchukua pesa au kutokuvaa glovu kunaniweka katika hatari ya maambukizi?
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hakuna ushahidi wowote kwamba pesa zinasambaza ugonjwa wa COVID-19. Unaruhusiwa kuvaa glovu, lakini watalaam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanashauri kwamba ni bora zaidi kunawa mikono ili kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya COVID-19 kuliko kuvaa glovu.
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
