Jinsi ya kutumia Uber vizuri – maelekezo ya safari yako nyingine ya Uber
4 Julai 2017 / Tanzania
Uber imejitolea kutoa huduma ambayo ni rahisi na nzuri kwa abiria na madereva. Sehemu ya kuunda uzoefu huu rahisi ni kutoa maelekezo kuhusu jinsi madereva na abiria wanapaswa kufanya na kutendeana safarini. Hiyo ndiyo maana Uber imetoa Maelekezo yao yaliyosasishwa ya Jamii, mwongozo huu sio tu wa ‘jinsi ya’ kwa madereva washiriki wa Uber, bali pia kwa abiria wa Uber.
Hii ndio mara ya kwanza Uber imechapisha sera inayoelezea ni kwa nini abiria wanaweza kupoteza uwezo wao wa kupata Uber. Hii ni muhimu kwa sababu wakati madereva wanatumia Uber wanafanya zaidi ya kuendesha gari tu: wanashiriki gari, nafasi na muda wao na abiria. Na ijapokuwa abiria wengi wanawaonyesha madereva heshima, kwa bahati mbaya sio kila wakati.
Maelekezo yaliyosasishwa ya Jamii ya Uber husaidia kuelezea ni nini Kisichokubalika kwenye safari ya Uber. Nyingi kati ya hizi ni mambo ya kawaida kwa wengi wetu lakini yanapaswa kuzingatiwa – iwe ni kutapika kwenye kiti cha nyuma au kuacha takataka ndani ya gari, orodha iliyo hapa chini ya maelekezo ni moja ambayo kila mtu anayetumia Uber anapaswa kuelewa – madereva na abiria na hata pia wale wanaosafiri pamoja na abiria / marafiki wengine.
Heshima:
Heshima ni muhimu, hakuna wakati wowote abiria au madereva wanapaswa kutoheshimiana. Magari yanayotumika kwenye app ya Uber ni ya madereva washiriki na wanajivunia kuweka magari yao katika hali nzuri kwa ajili ya starehe ya abiria. Abiria wanapaswa kuheshimu magari wanayoyatumia na wanapaswa kuacha magari hayo katika hali ambayo waliyapata.
Tabia ya ukaidi kama vile kuharibu gari haitakubaliwa. Kutumia lugha mbaya imepigwa marufuku pia. Kuwa na fujo au ubaguzi kunaweza kusababisha abiria kupigwa marufuku kutumia app hii. Uber haibagui kwa misingi ya jinsia au umbari na abiria yeyote ambaye hashiriki mtazamo huu hakaribishwi kutumia app hii.
Wape abiria na madereva nafasi yao ya binafsi:
Ijapokuwa mazungumzo ya kirafiki hayana madhara yoyote wakati wa safari, heshima inapaswa kudumishwa kila wakati. Abiria na madereva wanapaswa kupeana nafasi ya binafsi na hawapaswi kufanya yule mwingine ajihisi vibaya. Uber ina sheria ya ‘hakuna vitendo vya kimapenzi’, inayomaanisha hakupaswi kuwa na vitendo vya ngono kati ya madereva na abiria. Hiyo ni pamoja na kuchezeana na kugusana. Migusano yoyote ya kimwili kama vile kumgonga au kujaribu kumuumiza dereva yamepigwa marufuku.
Ili kuhakikisha usiri na kuimarisha usalama, Uber haiwaruhusu abiria na madereva kuangalia maelezo ya kibinafsi ya yule mwingine, kama vile nambari za simu ya mkononi, kupitia app hii. Kutuma sms, kupiga simu, au kumtembelea mtu baada ya safari kukamilika kumepigwa marufuku kabisa. Nafasi ya binafsi inapaswa kuheshimiwa.
Usalama kwanza:
Kufika mwisho wa safari yako ndio kipaumbele cha juu. Hii ndio maana madereva wanapaswa kutii sheria za barabarani kwa mfano, kufuata kasi inayoruhusiwa, kutoendesha kama wamelewa au kutumia dawa na kutotumia simu wanapokuwa wakiendesha gari. Madereva wanapaswa kupumzika kila wakati ikiwa wamechoka.
Abiria wanapaswa kutekeleza jukumu lao la kuvaa mikanda ya viti na kutojaribu kuwabeba watu zaidi wakati hakuna mikanda ya kutosha ya viti. Abiria wanapaswa pia kujiepusha kubeba vileo au mihadarati ndani ya gari na hawapaswi kumwomba dereva kwenda kwa kasi ya juu kuliko kasi inayoruhusiwa.
Lazima watoto waangaliwe:
Wale walio chini ya umri wa miaka 18 wanaweza kutumia Uber wakisimamiwa na mtu mzima, lakini hawawezi kuwa wenyewe na akaunti ya Uber. Wazazi au walezi wanapaswa kuwa na watoto wao kila wakati.
Kwenda mbele, ikiwa Uber itagundua kwamba mtoto asiyekuwa na mzazi ni mmiliki wa akaunti, akaunti hiyo italemazwa mara moja. Kama Uber itagundua kwamba abiria ana umri wa chini ya miaka 18 lakini mmiliki wa akaunti ni mtu mwingine ambaye amezidisha umri wa miaka 18, Uber itamkumbusha mmiliki wa akaunti hiyo kuhusu sera ya Uber na kulemaza wasifu wake baada ya onyo la pili.
Maoni yanatusaidia sisi wote kuimarika:
Kutoa maoni huwezesha Uber kujua abiria ameridhishwa au kutoridhishwa na nini, hiyo ndio maana madereva na abiria wanapaswa kutoa maoni ya safari yao kila wakati. Wakati watu wanajua kuwa wanatathminiwa wanakuwa makini zaidi kuhusu tabia zao na wanawajibika kwa hatua zao. Ajali, ada isio sahihi ya nauli au mabishano yanapaswa kuripotiwa kwa kubofya kitufe cha msaada kwenye app. Kuna timu ya usaidizi kwa wateja ambayo iko tayari kusaidia kila wakati.
Baada ya kujua kuhusu ukiukaji Uber itawasiliana na dereva ili kuchunguza. Kulingana na hali ya tatizo, akaunti ya abiria inaweza kusitishwa kwa muda wakati wa uchunguzi. Iwapo hoja hiyo itahusisha makosa makubwa yanayohusisha ukatili, makosa kadhaa ya ngono, unyanyasaji, ubaguzi au shughuli ambazo ni kinyume cha sheria, akaunti hiyo inaweza kulemazwa na mamlaka kufahamishwa. Uber itatoa maelezo yoyote ambayo mamlaka itayahitaji ili kuwasaidia katika uchunguzi wao.
Uber inajitahidi kuunda mazingira salama na mazuri kwa abiria na madereva washiriki. Maelekezo haya ni muhimu na hutekelezwa kwa faida za wale wote ambao wanatumia Uber. Madereva na abiria wanahimizwa kujifahamisha Maelekezo haya ya Jamii.
Posted by Uber Spokesperson
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
