Kufanya malipo ndani ya App ya Uber Driver
Ukiona salio hasi (-) kwenye akaunti yako ya Uber, ina maana kwamba unadaiwa ada ya huduma kutokana na hela ulizokusanya kutoka kwa wasafiri waliolipa pesa taslimu (cash).
Utakuwa na siku mbili za kufanya malipo baada ya kupokea ujumbe wa kukutaka ufanye malipo. Tafadhali fuata utaratibu ufuatao unapofanya malipo ya ada yako ya huduma:
Jinsi ya kufanya malipo
M-Pesa

Fungua app ya dereva halafu ubonyeze mistari mitatu juu kushoto

Fungua inbox, halafu chagua ujumbe unaohusiana na malipo.

Bonyeza ‘view payment details’ halafu bonyeza ‘start now’

Weka kiasi unachotaka kulipa (hakikisha kiasi unachoweka si chini ya kiwango cha chini kilichowekwa)

Chagua M-pesa kama njia ya malipo unayotaka kutumia.

Weka namba unayotaka kutumia kufanya malipo

Thibitisha malipo

Weka namba ya siri ya mobile money yako

Muamala umekamilika
Tigo pesa

Andika kiasi unachotaka kulipa

Chagua Tigo pesa kama njia ya malipo unayotaka kutumia

Weka namba unayotaka kutumia kufanya malipo

Thibitisha malipo

Weka namba ya siri

Muamala umekamilika
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
- Ni wakati gani ninaotakiwa nifanye malipo?
Uber itakutumia ujumbe muda wa kufanya malipo ukifika, kiasi unachodaiwa, na jinsi ya kufanya malipo. Utatakiwa ufanye malipo ndani ya siku mbili baada ya kupokea ujumbe unaokutaka ulipe ada ya huduma.
- Nililipa ada ya huduma lakini muamala huonekani kwenye akaunti yangu
Down Small Malipo huoneshwa papo hapo, baada ya kufanya malipo, lakini, inaweza kuchukua hadi saa 48 kabla ya ada unayodaiwa kufutwa.
- Je, ni nini maana ya kiasi cha chini (minimum amount)
Down Small Ili kuwapa madereva uhuru wa namna wanavyolipa, Uber inaruhusu walipe kiasi kisichopungua ukomo fulani ambacho ni kidogo ikilinganishwa na jumla ya ada anayodaiwa. Kiasi cha chini, ni kiasi cha chini kabisa ambacho utatakiwa ulipe ili upunguze ada unayodaiwa. Ukikosa kulipa ada unayodaiwa au kiasi cha chini kinachoruhusiwa unaweza kufungiwa akaunti yako hadi utakapofanya malipo.
- Je, ninaweza kulipa zaidi ya kiasi nilichoambiwa nilipe?
Down Small Hapana, huwezi kulipa zaidi ya ada ya huduma unayodaiwa.
- Ni shilingi ngapi naweza kulipa kwa mkupuo?
Down Small Unaweza kulipa kiasi chochote kuanzia kiasi cha chini na hata ada yote ya huduma unayodaiwa.
- Ni lini nitatakiwa nilipe?
Down Small Uber itakutumia ujumbe wenye maelezo ya muda wa kulipa, kiasi unachodaiwa, kiasi cha chini unachoweza kulipa na utaratibu wa kufanya malipo. Utakuwa na siku 2 za kufanya malipo baada ya kupokea ujumbe unaokutaka ulipe ada ya huduma.
- Ni mara ngapi ntalipa ada ya huduma?
Down Small Kiasi na unacholipa na jumla ya miamala inategemea uendeshaji wako mwenyewe na kiasi cha pesa unachokusanya kwa safari za pesa taslimu.
- Ni nini kitafanyika nikilipa kiasi cha chini?
Down Small Akaunti yako itafunguliwa tena ukilipa kiasi cha chini, hata hivyo, ina maana kwamba utapata ujumbe mwingine wa kulipa nyingine ndani ya siku chache.
- Kwa nini kiasi cha chini ninachotakiwa kulipa ni tofauti ikilinganishwa na wengine?
Down Small Ada unayotakiwa kulipa (yaani ada ya huduma) inategemea idadi ya safari unazofanya, na iwapo wasafari uliobebab walilipa kwa pesa taslimu. Ukifanya safari nyingi za pesa taslimu ikilinganishwa na safari za kadi basi utakuwa na salio hasi kwa hiyo ada utakayolipa itakuwa kubwa.
- Inachukua muda gani akaunti kufunguliwa baada ya kulipa ada ya huduma?
Down Small Akaunti yako itafunguliwa mara tu utakapolipa kiasi cha chini uliambiwa katika kulipa ada ya huduma unayodaiwa, hata hivyo, kuna mazingira ambayo inaweza kuchukua hadi saa 48. Hakikisha unalipa ada ya huduma kwa muda ili usipate usumbufu wowote.
- Inachukua muda gani kabla ya malipo muamala kuonekana kwenye akaunti ya dereva?
Down Small Muamala huoneshwa kwenye akaunti yako ya Uber papo hapo lakini inaweza kuchukua hadi saa 48 ada ya huduma unayodaiwa kutoweka (hii inaoneshwa kwenye akaunti yako ya benki au makato kufanywa kwenye njia yako ya malipo) baada ya kufanya muamala wako.
Posted by Monica Mziray