
Huna hakika? Vizuri, Eric ni msafiri mwenye tathmini ya nyota 5 – kuwa kama Eric!
Tunapenda kumsafirisha Eric ndani ya jiji. Madereva-washirika wetu wana hadithi nzuri za kukushirikisha juu yake.
Tazama baadhi ya vidokezo muhimu toka kwa Eric mwenyewe ili kujifunza jinsi ya kufanya safari ndani ya jiji kama msafiri bora na kuhakikisha una kuwa msafiri mwenye uzoefu wa tathmini ya nyota 5 kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kama yeye. Kuwa kama Eric!
Eric hutuma ombi la safari wakati akiwa tayari kufanya safari. Hamsubirishi dereva.
- Kumbuka, muda wa dereva-mshirika ni una thamani pia na wana furaha kubwa kukuhudumia kwa haraka sana mara baada ya kupokea ombi lako.
- Kwa muda gani unaweza kumsubirisha dereva wako? Dakika 5-10. Unahitaji aendelee kukusubiri zaidi? Tunakuushauri ukamilishe safari hii na kutuma ombi jingine wakati unapokuwa tayari kuondoka.
Eric anajua anpoelekea. Mara zote huandika jina la eneo analoelekea, ndani ya eneo ambalo Uber inafanya kazi.
- Hakikisha jina la eneo la kupakiwa/kuanzia safari ndani ya ramani kabla ya kugusa kitufe cha ‘Kutuma ombi’ Kupeleka pini kwa usahihi kwenye eneo la kuanzia safari kutawasaidia wote wewe na dereva kwa kuokoa muda ili muanze safari kwa mapema.
Eric ana kumbukumbu. Anahakikisha picha ya dereva na namba ya gari kabla ya kuingia ndani ya gari.
- Thibitisha kuwa napanda gari sahihi. Kama jina/namba ya gari iliyokuja kukuchukua haifanani na taarifa unazoziona kwenye kioo cha simu yako, katisha safari na toa ripoti kwetu _ Pitia taarifa za safari zako kwa kuchagua ‘Usaidizi na msaada` ndani ya programu ya Uber.
Eric husafiri na rafiki zake wasiozidi watatu (3). Kama kuna sherehe kubwa, huwa anawashauri rafiki zake watume maombi kwa magari mengine ya Uber.
- Gari uliloagiza lina uwezo wa kupakia msafiri wasiozidi wanne (4) – safiri kwa raha.
Eric ni mstaarabu, humsalimu dereva kwa tabasamu.
- Waheshimu madereva wako. Kupaza sauti au kutumia lugha chafu siyo tabia alizo nazo Eric.
Eric ana heshima. Hali wala kuvuta au kunywa ndani ya gari. Kamwe!
- Heshimu matatarajio ya madereva wako kwa kuwa umekaa ndani ya ofisi yao. Msaidie dereva wako kwa kuhakikisha kuwa gari lake lipo safi.
Eric hubeba hela ndogondogo na yakutosha ili kulipia safari za pesa taslimu.
- Hakuna tena sababu ya kugombana wala kuzozana na dereva-washirika.
Eric huwatathmini madereva kila baada ya safari. Huwapa tathmini ya nyota 5 kwaajili ya huduma nzuri.
- Watathmini madereva wako kulingana na utendaji wake na ubora wa huduma. Madereva hawapangi bei. Kama una swali, chagua safari yako na tuelezwe zaidi juu ya tatizo lako, ndani ya eneo la Usaidizi kwenye programu yako na tutakuwa na furaha kubwa kupitia nauli yako.
TAMBUA TATHMINI YAKO!
Ungependa kujua wapi unaweza kupata tathmini yako? 5 ni bora zaidi!
Unaweza kupata kwa urahisi ndani ya programu yako!
Ni rahisi sana, chagua:
- Usaidiza
- Akaunti na malipo
- Mipangilio ya Akaunti na Tathmini.
- Ningependa kujua tathmini yangu.
Safiri kwa furaha!
Posted by Grace
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
