
Tunaamini kila mtu hanabudi kujihisi salama awapo safarini. Hivyo tumeandaa miongozo hii unayotakiwa kuizingatia katika safari zako:
- Kuheshimu tofauti na mipaka ya watu mbali mbali wakati wote.
- Hakikisha maswali yako ni ya kiujumla na wala sio yanayohitaji mtu akupe taarifa zake binafsi
- Kumbuka kuwa baadhi ya vitendo vinaweza kutafsiriwa kimakosa kuwa ni ushawishi wa kingono hivyo yakupasa kuviepuka (kukonyeza, ushaufu, kugusa, kusifia mwonekano wa mtu, n.k.)
- Ni marufuku kushiriki ngono wakati wa safari.
- Kabla ya kumsaidia mtu, kila mara omba idhini kabla ya kufanya hivyo.
Je, unahisi uko hatarini ukiwa safarini? Gusa kwenye Kitufe cha Dharura kwenye Zana za Usalama (Ngao ya bluu) ili kuwasiliana na polisi.