
Uber imewasili katika mji mashuhuri wa Tanzania! Dar es Salaam ni mji uliojaa neema. Wenye hazina ya tamaduni mbalimbali na eneo linalokua kibashara ambapo umebadilikwa na kunonekana kuwa ni mji unaokuwa kwa kasi barani Afrika.
Hizi ni baadhi ya sababu kwanini Uber inaipenda Dar es Salaam na tunayo furaha kutamka kuwa ni mji wa 12 wa Uber barani Afrika. Tunaahidi kuwapa watu wa Dar es Salaam usafiri salama na nafuu kwenda maeneo mbalimbali ya jiji.
Bonyeza tu kitufe na Uber itakuunganisha na dreva aliye karibu jijini, tayari kukuchukua kwa dakika chache. Utaona picha ya dereva, gari linalokuja na pia unaweza kumwona kwenye App ya Uber jinsi anavyokukaribia.
Uzoefu wako ndio kipaumbele chetu cha kwanza, na tunayo furaha kukuletea usafiri nafuu na wa uhakika, hivyo ungana nasi kusherehekea Dar es Salaam!
Uber ni nini?
Wale wasiojua kuhusu Uber, tunasaidia watu kupata usafiri kwa kiasi cha kubonyeza kitufe-hakuna haja ya kusimama barabarani kusimamisha taksi au kutumia gari usilolijua. Ni njia rahisi ya kupata usafiri salama, nafuu na wa kuaminika-App itatambua mahali ulipo, itakujulisha kuhusu dereva wako mapema, na unaweza kuchagua kulipa kwa kadi au kwa pesa taslimu hivyo ni rahisi na salama kwa dereva na msafiri.
Kwanini usubiri?
1. Pakua App ya Uber katika Play store au App store.
2. Sajili kwa kuweka taarifa zako binafsi.
3. Chagua sehemu unapotaka kuchukuliwa, chagua gari na pata gari kwa muda halisi.
Mara zote husherehekea mji wake, tunachagua msafiri wa kwanza! Diamond Platnumz kuchagua msafiri wa kwanza wa Uber Dar es Salaam
Kwa Uber wasafiri wanaweza kutumiana gharama za usafiri kwa kubonyeza tu kitufe-ikimaanisha kama unaenda uwanja wa ndege kufanya manunuzi katika duka la Acacia, kuangalia sinema katika Uwanja wa Nelson Mandela au kwenda kwenye hafla ya usiku Aphrodisiac, utafikishwa kwa gharama pungufu.
Pricing in Dar es Salaam:
TZS 1,000 Base Fare + TZS 470 per kilometer + TZS 95 per minute
Minimum Fare: TZS 3,000
Cancellation Fee: TZS 3,000
Mfano wa baadhi ya safari na Uber:
- Julius Nyerere Airport hadi Dar es Salaam Serena Hotel: TZS 13,000
- Mlimani City Mall hadi Slipway Shopping Center: TZS 10,000
- Kigamboni Ferry Terminal hadi Kariakoo: TZS 6,000
MAKUBALIANO (vigezo kwa usafiri wa bure)
- Ni lazima upakue App ya Uber na weka kificho cha promosheni MoveTanzania ili upokee usafiri wa bure
- Usafiri wa bure utapatikana kutoka Alhamisi Juni 16 saa 6 mchana mpaka Jumapili Juni 19 katikati ya usiku
- Watumiaji watapata usafiri wa bure kwa safari sita tu na kila safari isizidi kiasi cha shs 12,000
- Usafiri wa bure utapatikana tu kwa safari zinazoanzia na kuishia maeneo ya Dar es Salaam yaliyopangwa
Uber, bado ipo kwenye majaribio hivyo kunaweza usafiri unaweza usipatikane baadhi ya maeneo kutoka wakati hadi wakati kwa kadri tunavyoendelea jijini Dar es Salaam. Tafadhali kuweni wavumilivu kwa wiki chache za mwanzo tutawaunganisha na madereva wengi zaidi haraka iwezekanavyo.
Tuna furaha mno kuwa hapa, na tunatumaini hata nawe pia, anza kutumia usafiri wa Uber na tuma ushauri wako kwa support@uber.com au twitter kwenye @Uber_Tanzania.
Tunakutakia safari njema!
Uber Team Dar es Salaam
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
