
Tupo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba unapata usafiri salama, wa uhakika na gharama nafuu popote pale na wakati wowote ukiwa ndani ya Dar Es Salaam. Ndio maana tunakupa wewe punguzo la 40% kwenye safari za uberPOA na uberX, ili tuzidi kuipeleka Dar Es Salaam mbele na kukupatia wewe usafiri wa gharama nafuu zaidi!
Wakati ni wako, unaweza kuchagua uberX kwa safari za kuanzia TZS 3000 na uberPOA kwa safari za kuanzia TZS 2000.
Kama kawaida yetu, tuta hakikisha unaendelea kupata huduma ya uhakika, kuanzia pale unapo agiza usafiri mpaka utakapo fika mwisho wa safri yako.
Tuangalie jinis nauli zetu zitakavyokua:
uberX:
Nauli za zamani (TZS) | Nauli mpya (TZS) | |
Posta mpaka Mwenge | 13,000 | 7000 |
Posta mpaka Ubungo | 16,000 | 9,000 |
Mwenge mpaka Tegeta | 16,000 | 9,000 |
uberPOA:
Nauli za zamani (TZS) | Nauli mpya (TZS) | |
Mlimani city mpaka Mbezi beach | 8,000 | 5,000 |
Tabata mpaka Ubungo | 10,000 | 6,000 |
Mwenge mpaka Tegeta | 12,000 | 7,000 |
*Nauli hubadilika kulingana na uhitaji pamoja na njia iliyotumika wakati huo.
Kama Uber, tunaendelea kutengeneza nauli zinazo mfaidisha msafiri pamoja na dereva-mshirika. Punguzo hili la 40% litaongeza wasafiri barabarani, kupelekea kuongezeka kwa safari zitakazo fanywa na madereva-washirika na kuongeza kipato.
Pia dereva mshirika atarudishiwa kiasi kilichotolewa kama punguzo kwenye safari hizi, hii yote ni kuhakikisha ya kwamba Uber itabakia kuwa njia ya wao kujiongezea kipato.
Kwa punguzo hili la bei kwenye app ya Uber, na uwezo wa kuagiza usafiri bila bando ukiwa na Tigo, huna sababu ya kuhairisha safari yako – ni rahisi sana, fungua app, agiza usafiri, nasi tutakufikisha kwa gharama nafuu!
Vigezo na Masharti
- Safari zenye punguzo ni za Uber kupitia uberX na uberPOA
- Nauli zilizo onyeshwa hapa, zinaweza kubadilika kulingana na uhitaji wa usafiri kwa wakati huo, na njia iliyotumika kwenye safari.
Posted by Uber Tanzania
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
