Dar es Salaam… Programu ya Uber kwenye lugha ya Kiswahili inawasili sasa!
19 Februari 2017 / Tanzania
Hapa Uber, tunaahidi kujitolea kukupa huduma bora ya kudumu, kuanzia pale unapofanya ombi la usafiri hadi dakika ya mwisho unapofikia kikomo cha safari yako.
Kama njia moja ya kutekeleza haya, tunapendelea upate fursa ya kutumia Programu tumizi ya Uber katika lugha yako unayoifahamu zaidi. Tunashikwa na furaha tele tunapowatangazia kuwa kuanzia leo, tarehe 16 Februari 2017, Programu tumizi ya Uber sasa utaipata kwa lugha ya Kiswahili!
TEKNOLOJIA UIPENDAYO, KWA LUGHA YAKO UNAYOIPENDA!
Programu hii hufanya uagizaji wa usafiri kuwa rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa – chagua tu mahala unapokusudia kushukia na moja kwa moja hii teknolojia ya kipekee ya smartphone itagundua mahala ulipo hivi sasa.
Jinsi ya kuomba usafiri:
- Fungua Programu tumizi ya Uber
- Bonyeza “unaenda wapi” na uamilishe mwelekeo wa safari yako
- Omba usafiri kama kawaida
- Fuatilia jinsi gari lako linavyokujia katika muda halisi
Kuboreshwa huku kwa kusisimua vile vile kunatolewa kwa madereva-washirika wetu kwa lugha ya Kiswahili, hii ikiwarahisishia upokeaji wa maombi ya usafiri, pamoja na kupata muingozo wa safari kwa kutumia programu hii. Tumeunda programu hii mpya tukitilia maanani abiria na madereva-washirika, ili aliyeabiri na dereva katika Uber wote wawili wapate huduma kwa urahisi na ya kutegemewa.
Je, umeshajaribu programu hii mpya kwa lugha ya Kiswahili? Tujulishe maoni yako kupitia Twitter au Facebook.
*Programu hii ya Uber itagundua moja kwa moja lugha iliyo kwenye simu yako ya mkononi. Nenda palipo na vipimo vya kawaida vya simu yako ya mnkononi na ufanyize upya.
Posted by oliviawaterkeyn
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
