Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Montréal–Pierre Elliott Trudeau (YUL)

Tumia Uber kusafiri popote, iwe unasafiri kutoka YUL hadi katikati mwa mji wa Montréal au kutoka kwenye hoteli yako hadi Uwanja wa Ndege wa Montréal.

975 Romeo Vachon Boulevard North, Dorval, QC, H4Y 1H1, Canada
+1 514-394-7377

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri katika zaidi ya viwanja vikuu 600 vya ndege.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

 • Taxi

  1-4

  Local taxi-cabs at the tap of a button

1/5

Kuchukuliwa ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Itisha usafiri ukiwa tayari kuondoka nje

Chagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kwenye daraja la Wanaoondoka au Wanaowasili

Elekea kwenye Mlango wa 7 katika sehemu ya Wanaoondoka au wa 20 katika sehemu ya Wanaowasili.

Mtafute dereva wako

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Montréal na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Ada

$42 kila siku
$39 kila siku
$31 kwa siku
$26 kila siku
$22 kila siku
$20 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 17 Desemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Montréal

Uwanja wa Ndege wa Montréal una kituo chenye ghorofa 2 kinachoweza kuwahudumia wasafiri wanaowasili kimataifa na nchini.

Vidokezo katika Uwanja wa Ndege wa YUL

Jinsi ya kuunganisha kwenye wi-fi

 • Chagua YUL Wi-Fi kwenye orodha ya mitandao
 • Ukishaunganishwa, fungua kivinjari chako cha intaneti
 • Kubali vigezo na masharti unapoulizwa kufanya hivyo

Mizigo mikubwa na wasafiri wengi

Ikiwa mko wengi na mna mizigo mingi au ungependa nafasi kubwa, tunakushauri utumie UberXL.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa YUL inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Montréal

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Montréal–Pierre Elliott Trudeau (YUL) ndio wa 3 kwa shughuli nyingi nchini Kanada kwa kuzingatia idadi ya wasafiri, unawahudumia takribani wasafiri milioni 18 kila mwaka. Uwanja upo katika Kisiwa cha Montréal, kilomita 19 (maili 12), au mwendo wa dakika 20 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani kutoka katikati mwa Montréal.

Vituo katika uwanja wa ndege wa Montréal

Uwanja wa Ndege wa Montréal una vituo 4 vilivyogawanywa katika vitengo 4: kitengo cha umma (daraja la wanaoondoka na wanaowasili), Bunta ya Safari za Ndani, Bunta ya safari za Kimataifa na Bunta ya safari za Nje ya Mipaka. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa YUL zinapatikana katika maeneo yote ya vituo. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Bunta ya Safari za Ndani

 • Air Canada
 • Air Creebec
 • Air Georgian
 • Air Inuit
 • Air Transat
 • Bearskin
 • First Air
 • Jazz
 • Miami Air International
 • Porter
 • PAL
 • Sky Regional
 • WestJet
 • Ukumbi wa Air Canada Maple Leaf

Bunta ya safari za Kimataifa katika YUL

 • Aeroméxico
 • Air Algérie
 • Air Canada
 • Air France
 • Air Saint-Pierre
 • Air Transat
 • All Nippon
 • British Airways
 • Corsair International
 • Cubana de Aviación
 • Japan
 • KLM
 • Lufthansa
 • Monarch
 • Qatar
 • Royal Air Maroc
 • Royal Jordanian
 • SATA International
 • Sunwing
 • SWISS
 • WestJet
 • Ukumbi wa National Bank

Bunta ya safari za Nje ya Mipaka YUL

 • Air Canada
 • Air Canada Express (Air Georgian)
 • Air Canada Express (Jazz)
 • Air Transat
 • Air Wisconsin
 • American
 • American Eagle
 • Compass
 • ExpressJet
 • GoJet
 • Republic
 • Sunwing
 • TACA
 • WestJet
 • Ukumbi wa Air Canada Maple Leaf

Kituo cha kimataifa cha YUL

Bunta ya Kimataifa kwa ajili ya safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Montréal Airport (Malango 50-53 na 55-68). Uwanja wa Ndege wa YUL hutoa usafiri wa moja kwa moja kuelekea maeneo 89 ya kimataifa.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Kuna zaidi ya maeneo 40 ya kupata chakula na vinywaji katika vituo na bunta zilizo katika Uwanja wa Ndege wa Montréal, zikiwemo migahawa inayouza vyakula vya kufangashiwa, baa na migahawa ya huduma ya kulia mezani. Wasafiri wanaweza kupata mapishi ya aina nyingi yakiwemo ya Kigiriki, ikari na sushi. Baadhi ya migahawa na maduka ya kahawa katika Uwanja wa Ndege wa YUL yanapatikana kabla ya ukaguzi wa usalama katika sehemu ya umma.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Uwanja wa Ndege wa Montréal hauna mifumo ya usafiri wa ndani. Usaidizi wa ziada katika uwanja wa ndege unapatikana kupitia kwa shirika la ndege unalotumia.

Mambo ya kufanya ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Uwanja wa Ndege wa YUL ni makao ya vivutio kadhaa, ikijumuisha Sanaa katika Uwanja wa Ndege, ambayo huonesha sanaa katika eneo lote la kituo. Watoto wanaweza kucheza katika maeneo yaliyo karibu na sehemu nyingi za kuabiria. Kwa watu wazima, kuna spaa katika Bunta ya Kimataifa karibu na Lango la 50. Vilevile, kuna maduka na maduka ya nguo katika Uwanja wa Ndege wa Montréal katika eneo la umma na mabunta.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Montréal

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa YUL zipo katika eneo la umma, katika Bunta ya Usafiri wa Ndani karibu na Lango la 1 na katika Bunta ya Safari za Kimataifa karibu na Malango ya 50, 53 na sehemu ya mizigo.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Montréal

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na YUL, kuna zaidi ya hoteli 20 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuzuru karibu na YUL

 • Mount Royal
 • Old Port of Montréal
 • Saint Helen’s Island
 • Saint Joseph’s Oratory

Pata maelezo zaidi kuhusu YUL hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.