Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Washington Dulles (IAD)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Dulles kwenda kwenye National Mall au shughuli za ununuzi mjini Georgetown.

1 Saarinen Circle, Dulles, VA 20166
+1 703-572-2700

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Green

  1-3

  Low-emission rides

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

 • Pool - Unavailable

  1-2

  Temporarily unavailable

1/6

Kupata usafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Dulles

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

On the baggage claim level, exit the down ramp from doors 2, 4, or 6 and follow signs for Ride App Pickup

Hapa ndipo madereva wote washirika wa Uber katika uwanja wa ndege wa IAD huwakuta na kuwachukua wasafiri.

Thibitisha mahali ulipo

Weka namba ya mlango ili dereva wako ajue mahali atakapokukuta.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Dulles na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Ada

Zisizidi $35 kila siku
$30 kila siku
$25 kila siku
$17 kila siku
$10 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Dulles

Uwanja wa Ndege wa Dulles una kituo kikuu na majengo 2 ya katikati ya uwanja yaliyo na Kumbi A/B na C/D. Kituo hicho kina malango 123.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa IAD inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo ya wageni ya Uwanja wa Ndege wa Dulles

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Washington Dulles (IAD) unapatikana eneo pana la jiji la Washington DC, na huwahudumia zaidi ya abiria milioni 21 kwa mwaka. Uwanja upo maili 26 (kilomita 42) magharibi mwa katikati ya jiji la Washington, unafikika kwa wasafiri wanaoingia na kutoka jijini. Uwanja huu wa ndege upo mwendo wa dakika 50 kwa gari kutoka katikati ya jiji.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Uwanja wa Ndege wa IAD una kituo kimoja kikuu—kituo hicho kina sehemu ya tiketi, sehemu ya kuchukua mizigo na forodhani—na vituo 2 vya nje, kila kimoja kikiwa na kumbi 2 (Malango katika Ukumbi wa A na Ukumbi wa B yapo upande mmoja, upande mwingine yapo malango katika Ukumbi wa C na D). Safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Dulles huanzia katika Ukumbi wa A. Unaweza kupanga safari yako kwa kutumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo Kikuu katika IAD

 • Air Canada Express
 • Frontier

Ukumbi wa A na B katika IAD

 • Aer Lingus
 • Aeroflot
 • Aeroméxico
 • Air China
 • Air France
 • Air India
 • Alaska
 • All Nippon
 • American
 • Austrian Airlines
 • Avianca
 • British Airways
 • Brussels Airlines
 • Cathay Pacific
 • Copa
 • Delta
 • Emirates
 • Ethiopian Airlines
 • Etihad
 • Icelandair
 • JetBlue
 • KLM
 • Korean Air
 • Lufthansa
 • Porter
 • Qatar Airways
 • Royal Air Maroc
 • Saudia
 • Scandinavian Airlines
 • South African Airways
 • Kusini magharibi
 • Turkish Airlines
 • United Express
 • Virgin Atlantic
 • Volaris
 • Ukumbi wa British Airways Galleries
 • Ukumbi wa Lufthansa
 • Ukumbi wa Turkish Airlines

Ukumbi wa C na D katika IAD

 • United
 • United Express
 • United Club

Kituo cha kimataifa katika IAD

Kuabiri kwa ajili ya safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Dulles kwa kawaida huanzia katika Ukumbi wa A. IAD una safari za moja kwa moja za kimataifa kuelekea maeneo 40.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Wasafiri wanaweza kuchagua miongoni mwa maeneo 40 ya kupata mlo katika uwanja wa ndege wa Dulles, yakiwemo migahawa maarufu ya kuuza vyakula vya kufungashiwa na migahawa ya kifahari iliyo na huduma ya kulia mezani. Sehemu za kula katika Uwanja wa Ndege wa IAD zinapatikana katika kituo kikuu na katika kumbi zote 4.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Kwa usafiri katika Uwanja wa Ndege wa Dulles, wasafiri wanaweza kutumia AeroTrain, mfumo wa usafirishaji wa watu kati ya jengo kuu la kituo kuelekea Kumbi zilizo A, B na C. Kutoka stesheni ya kituo kikuu, treni husafiri kutoka Ukumbi wa A na Ukumbi wa C kwenda upande mmoja na kuelekea Ukumbi wa B katika upande mwingine. Treni husafiri kila baada ya dakika 2, na wasafiri wanaweza kuelekea ukumbi husika kwa dakika 2. Ukumbi wa D unafikika kwa kutumia mfumo wa njia ya chini kwa chini.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Uwanja wa Ndege wa Washington Dulles una vivutio kadhaa, vikiwemo maeneo yanayouza bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya kielektroniki na zawadi. Kwa watoto, kuna eneo la kuchezea katika Ukumbi wa B karibu na Lango la B70 ambapo wanaweza kucheza, kuteleza na kukwea vitu. Wasafiri wanaweza kutembelea spaa iliyo katika Ukumbi wa A na B.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Dulles

Sehemu za kubadilisha fedha zinapatikana katika maeneo yote ya uwanja wa ndege. Nayo ni pamoja na:

 • Kituo: Sehemu ya Wasafiri Wanaoondoka, Daraja la Kukata Tiketi, Mashariki na Magharibi na kambarau za juu
 • Ukumbi wa A/B: Lango la A32
 • Ukumbi wa C: Malango C8 na C12
 • Ukumbi wa D: Lango la D16
 • Jumba la Wanaowasili kutoka Safari za Kimataifa karibu na eneo la kutoka, mkabala wa madawati ya kukagua tena mikoba

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Dulles

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na IAD, kuna zaidi ya hoteli 30 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Dulles

 • Georgetown
 • Sanamu ya Ukumbusho wa Lincoln na nyinginezo DC
 • National Mall na makumbusho yanayoizunguka
 • Bustani ya Wanyama ya Kitaifa

Pata maelezo zaidi kuhusu Dulles hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.