Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Fort Lauderdale–Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hollywood (FLL)

Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa FLL kwenda Lauderdale Beach au Las Olas Boulevard, Uber itakuwezesha kufika huko.

100 Terminal Drive, Fort Lauderdale, FL 33315
+1 954-359-1200

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • Pool1-2

  Usafiri wa pamoja, bei nafuu

 • UberX1-4

  Usafiri wa bei nafuu unaopatikana kila siku

Kupata usafiri katika Uwanja wa ndege wa Fort Lauderdale

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Hakikisha umechagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Halafu uweke eneo ambapo ungependa kuchukuliwa kuwa sehemu ya Magari ya Wasafiri wa Kibiashara, ambalo lipo kati ya vituo viwili.

Ondoka kupitia ghorofa ya chini ya wanaowasili.

Fuata mabango kwenye maeneo ya usafiri wa pamoja, yanayopatikana kati ya Vituo vya 1 na 2 na 3 na 4 katika upande wa ndani kabisa kando ya barabara. Hapa ndipo madereva wote washirika wa Uber katika uwanja wa ndege wa FLL huwapata na kuwachukua wasafiri.

Subiri kando ya barabara

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana na yeye kupitia programu ili umthibitishie mahali ulipo.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Wahudumu wa Kuegesha Gari Kando ya Barabara

Jumba la Maegesho ya Kiotomatiki

Ada

$25 kila siku
$3 kila saa; $15 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Uwanja wa Ndege wa FLL una vituo 4 vinavyoshughulikia safari za kimataifa: Kituo cha 1 kina kumbi 3 (A, B na C), Kituo cha 2 kina Ukumbi wa D, Kituo cha 3 kina Kumbi wa E na F, nacho Kituo cha 4 kiko kwenye Ukumbi wa G.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa FLL inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi maombi ya usafiri.

Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye programu kwa kutegemea hali za wakati huo.

Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye programu kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Fort Lauderdale–Hollywood (FLL) ni wa 19 kwa ukubwa zaidi nchini Marekani, kwa kuzingatia idadi ya abiria. FLL upo umbali wa dakika 10 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani kutoka katikati ya jiji la Fort Lauderdale, ambalo lipo maili 4 (kilomita 6) kaskazini mwa uwanja wa ndege. FLL upo maili 5 (kilomita 8) kaskazini mwa jiji la Hollywood, Florida.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

FLL una vituo 4: 1, 2, 3, na 4 ambacho ni kituo cha kimataifa. Kituo cha 1 kina kumbi 3 (A, B na C), Kituo cha 2 kina Ukumbi wa (D), Kituo cha 3 kina Kumbi 2 za (E na F) nacho Kituo cha 4 kikiwa na ukumbi mmoja wa (G), kina ya malango 64 katika vituo vyote. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa FLL zinaweza kupatikana katika Kituo cha 1 na 2. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika FLL

 • Alaska
 • Allegiant
 • Bahamasair
 • Copa
 • Silver
 • Kusini magharibi
 • Swoop
 • United
 • WestJet
 • United Club

Kituo cha 2 katika FLL

 • Air Canada
 • Delta
 • Delta Sky Club

Kituo cha 3 katika FLL

 • American
 • Azul
 • Emirates
 • JetBlue
 • Norwegian

Kituo cha 4 katika FLL

 • Air Transat
 • Avianca
 • British Airways
 • Caribbean
 • Frontier
 • IBC
 • SkyBahamas
 • Spirit
 • Sunwing
 • TAME

kituo cha kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Kituo cha kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Fort Lauderdale kipo katika Kituo cha 4, huku kikiwa na malango 10 yanayohudumu. FLL una safari za moja kwa moja za kimataifa kuelekea maeneo 60 katika nchi 33.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale una zaidi ya maeneo 50 ya kupata mlo yakiwemo baa, migahawa na migahawa iliyo na huduma ya kulia mezani. Wasafiri wanaweza kuchagua maeneo ya kulia, yakiwemo migahawa inayouza sandwichi na vitafunio vingine. Maeneo ya kulia kabla ya ukaguzi wa usalama yanayopatikana katika vituo vyote, na ukumbi wa maakuli unapatikana katika Ukumbi wa F katika kituo cha 3.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Fort Lauderdale–Hollywood hauna mfumo wa kusafirisha watu katika uwanja wa ndege. Ili usafiri kutoka kituo kimoja kwenda kingine, unaweza kutumia mabasi yasiyotozwa katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale yaliyo karibu na daraja la chini ya kila lango.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

FLL una vivutio mbalimbali, zikiwemo zaidi ya sanaa 40 zilizo katika maeneo mbalimbali kwenye kituo na sehemu ya kukodi gari. Vilevile, abiria wanaweza kusikiliza muziki ikiwemo blues, jazz na rock katika moja ya maeneo ya utumbuizaji katika uwanja wa ndege kila siku. Rafu za majarida na maduka katika uwanja wa ndege wa FLL yapo katika vituo na kumbi mbalimbali.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale zipo katika Kituo cha 2 kwenye Kituo cha Huduma za Kibiashara, kabla ya ukaguzi wa usalama katika daraja la tiketi, na katika Kituo cha 4 kwenye sehemu ya kuchukua mizigo katika daraja la chini.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na FLL, kuna zaidi ya hoteli 20 na maeneo ya kulala karibu. Pia kuna hoteli katika maeneo ya katikati ya Fort Lauderdale na katikati ya Hollywood.

Vivutio karibu na Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale

 • Everglades National Park, Homestead
 • Ufukwe wa Fort Lauderdale
 • Ufukwe wa Hollywood
 • Bustani ya Sawgrass Recreation, Weston

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale hapa.

Facebook
Twitter