Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kaunti ya Detroit Metropolitan Wayne (DTW)

Tumia Uber kusafiri popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Detroit hadi hifadhi ya wanyama au kutoka makavazi hadi DTW.

11050 Rogell Drive #602, Detroit, MI 48242
+1 734-247-7678

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

1/4

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Detroit

Fuata ishara ya kuelekea Ground Transportation Center

Baada ya kuchukua mikoba yako na kuondoka eneo la kukaguliwa, fuata ushoroba wa juu kuelekea GTC.

Tafuta mabango ya “Kusafiri Pamoja”

Pindi unapoweka GTC, tafuta ishara ya “Kusafiri pamoja” upate maelekezo zaidi.

Kutana na dereva wako katika sehemu ya kuchukuliwa iliyobainishwa

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kwenye programu ya Uber.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Detroit na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Ada

$24 kila siku
$14 kila siku
$12 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa Detroit una vituo 2 vikuu. Kituo cha McNamara kina Ukumbi wa A-C, huku Kituo cha Kaskazini kikiwa na Ukumbi wa D.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa DTW inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa Kaunti ya Detroit Metropolitan Wayne (DTW) ndio uwanja wenye shughuli nyingi mno katika eneo la Michigan na moja ya maeneo yenye shughuli nyingi za usafiri wa ndege nchini Marekani. DTW upo takribani maili 20 (kilomita 32) katikati ya jiji la Detroit (mwendo wa takribani dakika 30 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani). Uwanja unaweza kufikika kwa wasafiri wanaoenda au kutoka katika miji ya Detroit, Lake Michigan na Toledo katika jimbo jirani la Ohio.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa DTW una vituo 2 vikuu: Kituo cha McNamara na Kituo cha North. Kituo cha McNamara kimegawanywa katika kumbi 3: A, B na C. Kituo cha North kina ukumbi mmoja: D. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha McNamara katika DTW

 • Aeroméxico
 • Air France
 • Delta

Kituo cha North katika DTW

 • Air Canada
 • Alaska
 • American
 • Frontier
 • JetBlue
 • Lufthansa
 • Royal Jordanian
 • Kusini magharibi
 • Spirit
 • United
 • Wow
 • Lufthansa Club

Kituo cha Kimataifa katika DTW

Safari za kimataifa za Uwanja wa Ndege wa Detroit hufika na kuondoka katika vituo vyote viwili vya McNamara na North. Kituo cha McNamara kina malango 12 yanayotumiwa kwa ajili ya safari za kuondoka na kuwasili, na Kituo cha North kina malango 26. DTW huwa na safari za moja kwa moja kuelekea zaidi ya maeneo 30 ya kimataifa.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa Detroit unakupa chaguo nyingi za kupata chakula, kuna zaidi ya maeneo 100 kati ya vituo hivyo 2, yakiwemo maduka ya kahawa, migahawa inayouza vyakula vya kufangashiwa na migahawa iliyo na huduma za kulia mezani. Vilevile, Uwanja wa Ndege wa Detroit una baa zilizo katika sehemu mbalimbali za vituo.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Vituo vyote viwili vya Uwanja wa Ndege wa Detroit vina mikanda ya kutembelea inayojisogeza yenyewe. Kuna ExpressTram katika Ukumbi wa A katika Kituo cha McNamara, huu ni mfumo wa uchukuzi ambao huwasafirisha abiria kwa umbali wa maili 3 kati ya vituo 3 ambapo mfumo wenyewe upo ifuatavyo:

 • Stesheni ya Kituo: hiki ipo katikati ya ukumbi na unaweza kufikia malango kuanzia A29 hadi A55, eneo la kuingia, sehemu ya kuchukua mizigo, usafiri wa ardhini na njia ya chini kwa chini inayoelekea Kumbi za B na C
 • Stesheni South: inafanikisha usafiri kwenda malango ya A1 hadi A28
 • Stesheni ya North: inafanikisha usafiri kwenda malango ya A56 hadi A78

Isitoshe, abiria wanaweza kusafiri kwa mabasi kati ya vituo vya North na McNamara. Mabasi yanayohudumu kwenye uwanja wa ndege wa Detroit hutoka kila baada ya dakika 10 kutoka kwenye vituo vya usafiri wa ardhini na kwenye lango la Westin Hotel.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Kuna vivutio vingi vya kufurahia na shughuli za kufanya katika Uwanja wa Ndege wa DTW. Wasafiri wanaotafuta shughuli za kujituliza wanaweza kukandwa, kupambwa uso, kupata matunzo ya makucha ya miguu na mikono katika spaa iliyo kwenye uwanja wa ndege. Uwanja wa Ndege wa Detroit una maduka ya majarida, vipodozi na maduka ya nguo. Tundu lenye mwangaza lililo katika muunganisho kati ya njia ya A, B na C hucheza onesho la mwangaza na muziki kwa urari.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Ofisi za kubadilisha fedha katika uwanja wa ndege wa Detroit zipo katika maeneo yafuatayo: - Kituo cha McNamara: sehemu ya kuondoka (Central Link karibu na Lango la A38) na katika sehemu ya wanaoondoka kuelekea safari za kimataifa - Kituo cha North: sehemu ya kuondoka (moja kwa moja kutoka Lango la D9) na katika eneo la wanaowasili (karibu na sehemu ya kuchukua mizigo)

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Detroit

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na DTW, kuna zaidi ya hoteli nyingi na maeneo ya kulala karibu, katika maeneo ya Dearborn na jijini Detroit.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Detroit

 • Belle Isle Park
 • Eastern Market
 • Ford Field
 • Jumba la makumbusho la Detroit kuhusu muziki wa Motown

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa DTWhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.