Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kitaifa wa Ronald Reagan Washington (DCA)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa DCA kwenda National Mall au kununua bidhaa Old Town Mjini Alexandria.

2401 Smith Boulevard, Arlington, VA 22202
+1 703-417-8000

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • Pool1-2

  Usafiri wa pamoja, bei nafuu

 • UberX1-4

  Usafiri wa bei nafuu unaopatikana kila siku

 • Comfort1-4

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL1-6

  Affordable rides for groups up to 6

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa DCA

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Kwenye Kituo cha B/C, utadokezwa ndani ya programu kuchagua ikiwa ungependa kuchukuliwa kwenye ghorofa ya juu ya wanaoondoka (tiketi/kujisajili) au ghorofa ya chini ya wanaowasili. Hakikisha umechagua aina ya gari linalotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kwenye uwanja wa ndege

Kwa wasafiri wa kuchukuliwa katika Kituo cha A, elekea nje baada ya kuita gari kisha umsubiri dereva wako kando ya barabara.

Ikiwa unawasili katika Kituo cha B/C, unaweza kuchagua kuchukuliwa katika sehemu ya nje kando ya barabara nje ya milango ya 6, 7 au 8 kwenye ghorofa ya chini ya wanaowasili au kando ya barabara katika eneo jipya kwenye milango ya 1, 3, 4 au 6 ya ghorofa ya juu ya wanaoondoka.

Mkute na umthibitishe dereva wako.

Hakikisha kila wakati kwamba namba pleti ya gari inalingana na ile unayoona kwenye programu. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa DCA

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa DCA na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Jumba la Maegesho la Kituo cha A

Jumba la Maegesho ya Kituo cha B/C

Maegesho ya Kawaida

Ada

$25 kila siku
$25 kila siku
$17 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa DCA

Uwanja wa Ndege wa Reagan ndio uwanja mkuu unaohudumia mji wa Washington DC. Uwanja wa Ndege wa DCA una vituo 4. B na C ni vipya na kubwa zaidi.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa DCA inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye programu kwa kutegemea hali za wakati huo.

Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye programu kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Msimbo wa Uwanja wa Ndege DCA unasimamia Washington, DC, USA.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa DCA

Uwanja wa Ndege wa Kitaifa wa Ronald Reagan Washington (DCA) ndio uwanja wa msingi katika eneo la Washington, DC, huku ukiwahudumia zaidi ya abiria milioni 21 kila mwaka. Uwanja wenyewe upo maili 5 (kilomita 8) kutoka katikati ya jiji la Washington na ndio uwanja wa kibiashara ulio karibu kabisa na jiji kuu la Marekani. Uwanja wa ndege upo mwendo wa dakika 25 kwa gari kutoka katikati ya jiji la DC wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa DCA

Uwanja wa ndege wa DCA una vituo 3—A, B na C—vyote vikiwa na jumla ya malango 44. Kumbi za uwanja wa ndege wa DCA zipo katika vituo vyote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha A katika DCA

 • Air Canada
 • Frontier
 • Kusini magharibi
 • Ukumbi wa USO

Kituo cha B katika DCA

 • Alaska
 • Delta
 • United
 • American Airlines Admirals Club
 • Delta Sky Club
 • United Club

Kituo cha C katika DCA

 • American
 • American Airlines Admirals Club

Kituo cha kimataifa katika DCA

Uwanja wa Ndege wa DCA haufanyi safari za kimataifa (isipokuwa kwenda Kanada).

Kupata chakula katika Uwanja wa ndege wa DCA

Wasafiri wanaweza kuchagua miongoni mwa maeneo 40 ya kula katika uwanja wa ndege wa DCA yanayouza vyakula kadhaa vikiwemo vya kufungashiwa, vitafunio na vyakula vya kimataifa. Sehemu nyingi za kula katika uwanja wa DCA zipo katika vituo, lakini baadhi yazo zinapatikana katika ukumbi wa National kabla ya ukaguzi wa usalama.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa DCA

Usafiri wa mabasi katika uwanja wa ndege wa DCA huwasafirisha wasafiri kati ya vituo vya A, B na C; maegesho; na kituo cha magari ya kukodisha. Unaweza kupata taarifa za mahali basi linaelekea katika sehemu ya mbele na ubavuni mwa mabasi. Usafiri wa mabasi katika Uwanja wa Ndege wa DCA huhudumu kwa saa 24 kwa siku.

Mambo ya kufanya katika uwanja wa ndege wa DCA

Uwanja wa Ndege wa DCA una miradi ya sanaa inayoonesha sanaa za eneo, taifa na kimataifa kwa kuhamahama. Roshani ya sanaa ipo katika Kituo cha Kihistoria cha A kati ya Ukumbi wa Kihistoria na ukumbi wa sasa wa kukata tiketi, ikijumuisha maonesho mbalimbali kutoka kwa wasanii wenyeji. Kadhalika, uwanja huu huwa na wanamuziki, waimbaji, wacheza ngoma na wasanii wengine. Uwanja wa Ndege wa DCA una maduka kadhaa, zikiwemo rafu za magazeti na maduka ya nguo.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa DCA

Ofisi ya kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa DCA ipo katika Njia iliyo karibu na Kituo cha C, kabla ya ukaguzi wa usalama.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa DCA

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na DCA, kuna zaidi ya hoteli 20 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa DCA

 • Georgetown
 • Sanamu ya ukumbusho wa Lincoln na nyinginezo za DC
 • National Mall na makavazi yanayoizunguka
 • Ikulu ya White House

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu DCA hapa.

Facebook
Instagram
Twitter