
Hakuna anayejua undani wa kuendesha gari katika mfumo Uber kuliko wewe. Kwa hivyo, tulipoanza kuunda programu bora zaidi, tuliomba usaidizi wako.
Katika kipindi cha mwaka uliopita, zaidi ya madereva 400 na washirika wanosafirisha mizigo katika miji 7 kote ulimwengini wamekuwa wakishiriki katika mpango maalum wa majaribio ya Beta ili kusaidia timu yetu kuunda programu mpya ya madereva na kuifanyia majaribio. Wamekuwa wakishirikiana na wasanifu na wahandisi wa Uber kwa kutoa mawazo mapya, kutoa maoni na kuripoti hitilafu.
“Majaribio ya kawaida ya Beta hayangetosheleza mahitaji yetu. Ilitubidi tufanye zaidi ya hilo. Tulihitaji kuelewa jinsi programu ilivyofanya kazi katika miji tofauti na katika mazingira tofauti kwa wanaosafirisha mizigo na madereva mbalimbali. Tulitaka kujua wakati ambapo ilifanya kazi vizuri na kuwaridhisha na wakati ambapo haikufanya kazi vizuri. Kwa hivyo, tulibuni mbinu kadhaa za kuwasikiliza na kujifunza kutoka kwao.” – Haider, mhandisi wa Uber
Kwake Eva aliyeshiriki katika majaribio ya Beta, fursa ya kutoa maoni moja kwa moja ndiyo ilimridhisha zaidi katika mpango huo.
“Nilifurahia sana kwa sababu maoni yangu yalithaminiwa. Nilipata fursa ya kuwaeleza ambayo niliona kuwa yalihitaji kurekebishwa na yaliyokuwa mazuri ili yaendelezwe… Nilifurahia kushiriki katika mchakato huo.” – Eva, dereva
Steph, aliyeshiriki katika mpango wa majaribi ya Beta jijini Los Angeles, alifurahi kushirikiana na wafanyakazi wa Uber na madereva wenzake.
“Ilinipa fursa ya kuwasiliana na madereva wengine na watu wanaofanya kazi katika Uber. Niliweza kuzungumza ana kwa ana na watu kadhaa. Nilifurahi hata zaidi kuhudhuria tamasha ya kwanza ya Beta.” – Steph, dereva
Madereva wetu na washirika wanaosafirisha mizigo walitusaidia sana katika kutambua matatizo na sehemu zilizohitaji kuboreshwa. Katika kipindi cha wiki 16, waliripoti zaidi ya hitilafu 2600 kwa kutuma picha za skrini kwa wafanyakazi wa Uber kwa njia mbalimbali, ikiwemo mitandao ya jamii. “Nilifurahi kushirikiana na [timu ya Uber] kupitia WhatsApp,” alisema Steph, “Nilikuwa nikiandika ujumbe na kupiga picha za hitilafu zilizokuwa kwenye programu.”
“Suala moja nililoliibua wakati wa jaribio la beta ni lile la safu zenye rangi za kuonesha Nyongeza na kuongezeka kwa nauli kwenye ramani. Zilikuwa aidha za gridi kubwa, zisizo na gridi au zisizo bayana. Sasa unaweza kutambua haraka kwamba kuna eneo lenye wasafiri wengi. Hapo awali, ungeona rangi hafifu kisha ungehitajika kukuza picha ili uielewe.” – Mike, dereva
Wafanyakazi wa Uber pia walijiunga na madereva na washirika wanaosafirisha mizigo katika safari kwa kuwachukua wasafiri au kusafirisha mizigo huku wakitumia programu mpya.
“Nilipendezwa na hatua ya Uber ya kuwahusisha madereva wenyewe. Wangetuma fomu ya utafiti, lakini nahisi kwamba kwa kushirikiana nao ana kwa ana na kwa kuwa nao ndani ya gari, wangejionea jinsi hali ilivyo na tunavyofanya kazi. Ni vizuri niliweza kuongea nao papo hapo, badala ya kutuma barua pepe na kusubiri majibu yao.” – Glory, mshirika anayesafirisha mizigo.
Shukurani kwa madereva na washirika wote wanaosafirisha mizigo ambao walichangia katika kuunda programu mpya ya madereva. Tunapoendelea kuboresha huduma ya Uber, tunatarajia kuleta fursa zaidi za kushirikiana.
Posted by Uber Editor
Get a ride when you need one
Start earning in your city
Get a ride when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular

Automating Efficiency of Go programs with Profile-Guided Optimizations

Enhancing Personalized CRM Communication with Contextual Bandit Strategies

Introducing the Audio Recording feature in Tanzania
