
Kila mtu anastahili kuwa na safari ya hadhi ya nyota 5 – wasafiri na madereva kwa pamoja. Bado hujapata huduma ya hadhi hii? Usijali. Kila safari unayofanya inakupa fura ya kuboresha tathmini unayopata kama msafiri!
Ifuatayo ni baadhi ya mikakati maarufu #ProTips inayoweza kukusadia kuboresha tahmini unayopata kama msafiri wa Uber:
Kufika mahali eneo la kuchukuliwa kwa muda
Bila shaka utapata tathmini mbaya iwapo dereva atalazimika kuzunguka mitaa mbalimbali akikutafuta. Hakikisha eneo ulilosimama ndio sehemu uliyoweka kama eneo lako la kuchukuliwa kisha uite gari ukiwa umesimama eneo hilo. Je, unachelewa sehemu na ungependa uwahi kufika? Mwandikie ujumbe au umpigie simu dereva wako kumjulisha.
Iwe uko tayari au la, gari la Uber limefika
Usimpotezee muda dereva wako – muda wao ni muhimu sana na wana shughuli zao za kufanya. Ikiwa unaitia marafiki usafiri, hakikisha wamejiandaa na wako tayari kabla uite gari la Uber.
Samahani, ni mimi unatafuta?
Hali hii hutokea kila isku – usiwafanyie wenzako kinyume na ambavyo ungependa kufanyiwa – usimwonee unyonge mtu yoyote unapokuwa kwenye safari yako ya Uber. Ni vizuri kumsalimia, na jitambulishe ukishaabiri gari. Hii itamsaidia dereva hasa katika kuhakikisha kwamba habebi msafiri tofauti na aliyeita gari ili aanze safari mara moja!
H-E-S-H-I-M-A
Usiwafanyie watu wengine visivyo: waheshimu madereva. Usiseme nao kwa sauti kubwa, kutukana, kubamiza mlango kwa nguvu. Chukulia gari la dereva kama gari lako. Bila shaka huwezi kuacha taka ndani ya gari lako, au sio? Na huwezi kubamiza mlango wa gari lako kwa nguvu baada ya kushuka? Madereva wengi hutumia magari yao binafsi, kwa hiyo jitahidi sana usichafue au kuharibu gari unalotumia kwenye safari yako. Zaidi ya yote, ni zivuri kuheshimiana na kuchukuliana licha ya tofauti mbalimbali. Tungependa kila mtu ajisikie huru na salama anapotumia usafiri wa Uber.
Furahia safari yako, upate tathmini nzuri
Nia yetu ni kukuona unafurahia safari yako, unachotakiwa kufanya ni kutulia na kufurahia safari yako na madereva watakupatia huduma ya hadhi ya nyota 5. Hakikisha unamtathmini dereva wako kulingana na huduma yake. Kuna mambo ambayo yako nje ya uwezo wa dereva, kama vile nauli. Ikiwa kuna tatizo lolote, unaweza kutumia sehemu ya usaidizi kwenye app yako na bila shaka tatizo lako litapata ufumbuzi.
Kimsingi haya nidyo mambo ya kuzingatia. Mwongozo utakaokusaidia kupata tathmini ya nyota 5, na utajivunia tathmini yako!
Posted by Uber Editor
Get a ride when you need one
Start earning in your city
Get a ride when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular

Automating Efficiency of Go programs with Profile-Guided Optimizations

Enhancing Personalized CRM Communication with Contextual Bandit Strategies

Introducing the Audio Recording feature in Tanzania
