Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber

Mwongozo wa jinsi ya kutumia Uber

Iwe unafanya shughuli mjini au unazuru mji wa mbali, safiri kwa urahisi. Pata maelezo zaidi kuhusu kusafiri kwa kutumia programu ya Uber.

Jisajili ili usafiri

Jinsi ya kutumia programu ya Uber

Fungua akaunti

Unachohitaji tu ni anwani ya barua pepe na namba ya simu. Unaweza kuitisha usafiri kwenye kivinjari chako au kupitia programu ya Uber. Tembelea App Store au Google Play ili upakue programu mpya.

Weka mahali unakoenda

Fungua programu na uweke mahali unakoenda katika kisanduku cha Ungependa kwenda wapi. Bonyeza ili uthibitishe mahali utakakochukuliwa kisha ubonyeze Thibitisha tena ili ukutanishwe na dereva aliye karibu nawe.

Kutana na derava wako

Unaweza kufuatilia muda atakaowasili kwenye ramani. Akiwa karibu, msubiri kwenye eneo la kuchukuliwa.

Kagua gari lako

Kwa usalama wako, hakikisha kuwa unaingia katika gari sahihi. Kabla ya kuabiri, thibitisha utambulisho wa dereva, aina ya gari na namba pleti ya gari na maelezo yaliyo kwenye programu. Ukishaabiri gari, hakikisha dereva wako amethibitisha jina lako kabla ya safari

Keti na utulie

Ni rahisi kulipa ukiwasili. Una chaguo mbalimbali, kulingana na eneo lako. Lipa kwa pesa taslimu au mbinu ya malipo kama vile kadi ya benki au salio la Uber Cash.

Tathmini ubora wa safari yako

Hebu tujulishe jinsi safari yako ilivyokuwa. Pia unaweza kumpa dereva wako pongezi na utoe bakshishi katika programu yako.

Safari rahisi kutoka mwanzo hadi mwisho

Nauli utakayolipa moja kwa moja

Kabla ya kuthibitisha safari, angalia makadirio ya nauli ili usibahatishe. Kwa hivyo, utaweza kulinganisha nauli ili upate gari linalokufaa zaidi kila wakati.

Boresha hali ya kuchukuliwa

Ukiitisha usafiri, programu itakupendekezea kiotomatiki mahali mwafaka pa kukutana na dereva wako. Ili ubadilishe mahali ulipo, andika eneo jipya ambapo ungependa kuchukuliwa au uburute kipini cha mahali na ukiweke katika ramani ndani ya mduara wa kijivu.

Mfahamu dereva wako.

Angalia Wasifu wa Madereva katika programu ili uone vidokezo vya kuvutia kumhusu dereva wako, ikijumuisha tathmini na pongezi.

Tathmini na bakshishi

Tusaidie kuboresha huduma za usafiri kwa kutathmini safari. Pia unaweza kumpa dereva bakshishi ikiwa amekuhudumia vizuri.

Unapata utulivu wa mawazo kila unaposafiri

Tunaupa kipaumbele usalama wako, kama vile kupitia uchunguzi wa madereva, bima, vipengele vya programu vinavyokuwezesha kufuatilia safari yako na kusalia mtandaoni.

Safiri bila wasiwasi

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Unaweza kuratibu safari siku 30 kabla ya kusafiri. Unaweza kufungua programu kisha ubonyeze aikoni ya gari na saa karibu na kisanduku cha Ungependa kwenda wapi?.

Jinsi ya kuratibu safari

Fungua programu kisha ubonyeze kisanduku cha Ungependa kwenda wapi? Ukibonyeza, utafungua chaguo la kusogeza chini la Badilisha Msafiri. Bonyeza kipengele hiki kisha umchague rafiki yako. Utapokea ujumbe ulio na maelezo ya safari, ikijumuisha muundo wa gari na namba pleti, jina la dereva na maelezo ya mawasiliano, na Muda Atakaowasili.

Jinsi ya kumwitishia rafiki usafiri

Nauli hukadiriwa kulingana na saa na umbali. Nauli hizi zinaweza kubadilika, unaweza kulipia ada za barabara, ada ya kughairi safari na ya muda wa kusubiri, panapohitajika, na ada za kuweka nafasi.

Mamia ya pointi za data zitatumika kukokotoa nauli utakayolipa. Kiasi cha nauli hutegemea muda uliotumika katika safari, umbali kutoka kituo cha kwanza hadi mahali unakoenda, wakati, barabara uliyofuata na wingi wa wasafiri. Kiasi cha nauli pia hutegemea ada za barabara, kodi, ada ya ziada na ada nyinginezo.

Pata maelezo ya bei

Tathmini hufanywa kwa madereva na wasafiri. Baadhi ya maoni tunayopokea mara nyingi kutoka kwa madereva ni kwamba wanapenda wasafiri wakiwa na mjadala wa kuchangamsha, walitumie vizuri gari na mali yao, ikijumuisha kufunga mlango wa gari bila kuugongesha wanapoingia au kushuka, na wasiwasumbue wanapoendesha gari. Angalia Mwongozo wa Jumuiya yetu ili upate ushauri zaidi.

Angalia Mwongozo wa Jumuiya Yetu

Unaweza kuongeza hadi vituo 2 kabla au wakati wa safari yako. Bonyeza kipengele cha + karibu na kisanduku cha Ungependa kwenda wapi? ili uweke nauli yako. Nauli yako inaweza kurekebishwa kulingana na muda na umbali wa mahali unakoenda.

Jinsi ya kuongeza vituo zaidi vya kusimama