Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Ahadi yetu kuhusu usalama

Tungependa usafiri bila wasiwasi, utumie wakati vizuri na ukutanishwe na watu na maeneo muhimu kwako. Ndiyo maana tumejitolea kulinda usalama, kuanzia kuunda viwango vipya hadi kubuni teknolojia kwa lengo la kupunguza ajali.

Kusaidia kudumisha usalama wa kila mmoja wakati wa COVID-19

Tunafuatilia kikamilifu hali ya virusi vya corona (COVID-19) na tunajitahidi kuendelea kuimarisha usalama wa wanaotegemea mfumo wetu.

Jinsi usalama unavyodumishwa kwenye usafiri wako

Vipengele vya usalama kwenye app

Kuwaonesha ndugu na marafiki maelezo ya safari Kufuatilia safari yako barabarani. Teknolojia yetu inasaidia kuondoa wasiwasi kwa urahisi.

Jumuiya inayojali maslahi ya kila mtu

Mamilioni ya wasafiri na madereva wanafuata Mwongozo wa Jumuiya na hivyo wanawajibika kufanya mambo yanayofaa.

Usaidizi popote ulipo

Timu yetu ya wataalamu inapatikana kila wakati. Wasiliana nayo kupitia programu, usiku au mchana, ukiwa na maswali yoyote au matatizo ya kiusalama.

Kuhakikisha safari salama kwa ajili ya kila mtu

Usalama wa dereva

Kuna usaidizi wa saa 24 siku 7 za wiki na msaada wakati wa matukio ya dharura. Onyesha safari yako kwa watu wako wa karibu. Tumeweka kipau mbele kwenye usalama wako, ili ujishughulishe na shughuli zinazokuingizia pesa.

Usalama wa msafiri

Mamilioni ya watu huomba safari kila siku. Kila msafiri anaweza kufikia vipengele vya usalama vilivyo kwenye programu. Na kila safari ina timu ya usaidizi kwa wateja inayopatikana wakati wowote.

Mustakabali wa usalama

Zaidi ya wafanyakazi 200 wa Uber, wakiwemo watafiti na wanasayansi, wasanifu na wahandisi, wanajitahidi kubuni teknolojia inayojumuisha usalama katika huduma zetu. Gundua wanachofanya.

“Kila siku, teknolojia yetu husaidia mamilioni ya watu kupata usafiri katika miji ulimwenguni kote. Jukumu la kuhakikisha usalama wa watu ni muhimu sana na tunalichukulia kwa makini zaidi.”

Dara Khosrowshahi, Afisa Mkuu Mtendaji wa Uber

Tunashirikiana ili kuleta mabadiliko.

Ahadi yetu ya usalama inadumu hata baada ya safari yako. Tumeungana na kikundi cha wataalamu wakuu - ikiwemo maafisa wa usalama wa umma na mashirika ya kupambana na vurugu - ili kusaidia kuimarisha usalama kwenye barabara na miji kwa ajili ya kila mtu.

Usalama wa dereva

Endesha gari mahali na wakati unapotaka bila wasiwasi.

Usalama wa msafiri

Nenda wakati wowote na ufike kwa starehe.

*Baadhi ya masharti na vipengee hutofautiana kulingana na eneo na huenda havipatikani.