Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Madereva wanaweza kupata kiasi gani cha pesa kwa kutumia Uber?

Pesa unazopata kwa kuendesha gari kupitia App ya Uber hutegemea wakati, mahali na mara unapoendesha gari. Fahamu jinsi nauli unayopata inavyohesabiwa na upate maelezo zaidi kuhusu ofa ambazo zinaweza kukusaidia upate mapato zaidi.¹

Jinsi mapato huhesabiwa

Huenda unataka kujua kiasi cha hela unachoweza kupata kupitia Uber. Vipengele vifuatavyo vinasaidia kuchangia mapato unayopata katika kila safari.

Nauli ya kawaida

Utapokea nauli kwa kila safari unayokamilisha.

Ongezeko la Nauli

Angalia ramani ya rangi kwenye programu yako ili kujua wakati na maeneo ambako wasafiri wanahitaji sana Uber, ili utengeneze hela zaidi kando na nauli yako ya kawaida.

Mapato ya chini kabisa ya safari

Kila mji una kiasi cha chini zaidi cha pesa utakazopata kutokana na safari yoyote. Hatua hii inahakikisha mapato yako yanaonesha jitihada unayoweka, hata katika safari fupi.

Ada ya huduma

Ada hii inatusaidia kulipia huduma kama kuboresha App, usaidizi kwa wateja, na kuchakata malipo.

Kughairi

Mara nyingi, utapokea ada ya kughairi iwapo msafiri ataghairi usafiri anaoitisha.

Ofa na jinsi zinavyotumika

Ofa za ndani ya App kutegemea maeneo ambapo App ya Uber Driver inatarajia maombi mengi ya usafiri zinakusaidia kujipanga mapema na kuweka malengo ya kupata hela zaidi. Ofa hutolewa kulingana na aina ya madereva. Angalia vigezo na masharti hapa chini.²

Fikia idadi ya safari zilizowekwa

Pata pesa zaidi kwa kukamilisha idadi fulani ya safari katika kipindi fulani wakati ofa inatumika.

Endesha gari nyakati za shughuli nyingi

Pata hela zaidi kwa safari katika maeneo fulani nyakati za shughuli nyingi.

Njia za kutengeneza pesa kwa urahisi

Jinufaishe kwa kutumia programu hii

Programu hii ina vipengele vinavyokuwezesha utumie muda wako vyema zaidi ukiwa safarini. Programu hii inakuwezesha kufuatilia mitindo na kukufahamisha kuhusu fursa za kupata pesa karibu nawe na zaidi. Ni rafiki yako barabarani.

Wakati na jinsi unavyolipwa

Pokea malipo kwa haraka

Ni rahisi kupokea malipo. Unatakiwa tu kuwa na akaunti ya benki. Mapato yako huwekwa kwenye akaunti kila wiki.

Mteja wako akilipa pesa taslimu

Utalipwa pesa taslimu pindi utakapokamilisha safari. Programu hii itakuonesha nauli ya kumlipisha mteja wako na kuhesabu ada unazostahili kulipa Uber.

Maswali yanayoulizwa sana na madereva

  • Nyakati za shuguli nyingi, nyongeza ya nauli itaonekana kwenye ramani kwa rangi nyekundu, ya chungwa au manjano. Ili upate nyongeza ya nauli, endesha gari katika maeneo yenye rangi, usiondoke mtandaoni na kubali safari inayofuata.

    Utapata kiasi cha nyongeza ya nauli baada tu ya kukamilisha safari husika.

  • Unaweza kuona muhtasari wa mapato yako kwenye programu. Bonyeza aikoni ya nauli kwenye ramani ya skrini, kisha utelezeshe kidole kulia na kushoto ili uone mapato yako yote.

  • Ndiyo. Ni wewe utakayeamua jinsi na wakati wa kuendesha gari. Iwapo unatafuta njia rahisi ya kupata hela, kazi ya kuendesha gari ukitumia Uber huenda itakufaa zaidi.

  • Ukiwa safarini, wasafiri hutozwa ada ya vibali na kiasi hiki huongezwa kiotomatiki kwenye nauli unayopokea. Unaweza kuangalia mapato yanayotokana na vibali katika sehemu ya mapato au kwenye maelezo ya safari katika programu.

¹Maelezo yaliyo kwenye ukurasa yanalenga kukufahamisha tu na hayakuhakikishii mapato. Huenda hali za mapato zikawa tofauti kulingana na mji. Angalia tovuti mahususi ya mji wako kila wakati ili upate maelezo sahihi zaidi kuhusu ada ya usafirishaji.

²Uber itakujulisha utakapotimiza masharti ya kupata ofa. Masharti ya ofa yatazingatiwa. Tutakutumia vigezo na masharti yoyote kwenye zana au ofa mahususi. Uber inaweza kubadilisha au kughairi ofa yoyote, ikiwemo masharti yanayohitajika ili kupata ofa hiyo.