Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Fursa iko kila mahali

Tumia wakati wako vizuri unapoendesha gari kwenye mtandao mkubwa zaidi wa wasafiri.

Unapata pesa kwa muda wako

Weka ratiba yako mwenyewe

Wewe ndiye boss. Unaweza kutumia App ya Uber kuendesha gari wakati wowote, usiku au mchana. Badilisha kazi yako isihitilafiane na shughuli zako nyingine za maisha, sio kubadilisha maisha yako ili kutosheleza mahitaji ya kazi yako.

Unapata pesa bila masharti yoyote

Kadri unavyofanya safari nyingi ndivyo unavyopata pesa nyingi. Unaweza kupata nyingi zaidi mahitaji ya gari yakiongezeka.

App itakuongoza katika kila hatua

Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza simu yako tu. Utaongozwa hatua baada ya hatua, utapata mapendekezo yatakayokusaidia kupata pesa nyingi zaidi, na tuko hapa kukusaidia katika kila hatua usiku na mchana.

Anza sasa

 • Jisajili mtandaoni

  Tuambie tu mji unaotaka kuendeshea gari na aina ya leseni uliyo nayo.' 'Tutakutumia barua pepe iliyo na hatua zinazofuata.

 • Angalia masharti ya kuendesha gari

  Watu wengi wametimiza masharti ya kuendesha gari kwenye mfumo wa Uber. Yafuatayo ni mambo unayohitaji kujua ikiwa unaendesha gari mjini Dar es Salaam.

 • Pata gari

  Ni gari gani linalokufaa? Hakikisha linatimiza masharti yetu nchini Tanzania. Pia, kumbuka kuwa utatengeneza pesa zaidi ikiwa bei zako ni nafuu.

1/3

Huduma za ziada

Huduma tunazokupatia nchini Tanzania

Pata usaidizi

Tushirikiane kurahisisha safari zote za Uber. Kurasa zetu za usaidizi zinaweza kukusaidia kufungua akaunti, kuanza kutumia programu, kubadilisha nauli na mengine.

Wasiliana nasi

Je, una swali lolote? Utajibiwa. Utahudumiwa kwa namna pekee katika Kituo cha Madereva wa Uber katika ofisi za Dar es Salaam.

Usalama barabarani

App ya Uber ina vipengele vingi vinavyosaidia kulinda usalama wako barabarani sambamba na kujiamini kabla ya safari, wakati wa safari na hata baada ya safari. Ukihitaji usaidizi wowote, Uber ina huduma inayopatikana usiku na mchana ili kukupa usaidizi unaohitaji.

App ya Dereva

Ni rahisi kutumia na inaaminika. App hii iliundwa na madereva kwa ajili ya madereva.

Maswali yanayoulizwa sana

 • Uber inapatikana katika mamia ya miji kote ulimwenguni. Gusa hapa chini ili uone ikiwa huduma inapatikana katika mji wako.

 • Lazima uwe umefikisha umri unaotakikana ili uendeshe gari katika mji lako, uwe na aina inayostahiki ya usafiri na uwasilishe hati zinazotakikana, ikiwemo leseni halali ya udereva. Madereva nchini Marekani lazima pia wapitie uchunguzi wa rekodi ya uhalifu na wawe na uzoefu wa kuendesha gari wenye leseni kwa angalau mwaka mmoja.

 • Tunathamini usalama wako zaidi. Uber ina Timu ya Usalama ya Kimataifa inayojitolea kuhakikisha kuwa tunazuia matukio hatari. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya usalama katika App, pamoja na vipengele vya ulinzi kama vile ufuatiliaji wa GPS na kuficha namba ya simu yako, kwa kufungua kiungo kilicho hapa chini.

 • Ikiwa unataka kuendesha gari katika mfumo wa Uber lakini huna gari, unaweza kupata gari kutoka kwa mmoja wa washirika wetu wa magari au kutoka kwa mmiliki wa magari katika mojawapo ya masoko mahususi. Tafadhali kumbuka kuwa aina za magari zinaweza kutofautiana kulingana na jiji.

Endesha gari kupitia App

Ofa hii si ahadi au hakikisho kuhusu mapato unayofaa kutarajia siku zijazo. Ofa hii inapatikana tu kwa madereva na wasafirishaji wapya wa chakula kwenye App ya Uber ambao (i) hawajawahi kujisajili hapo awali kuendesha gari au kusafirisha chakula kwa kutumia mfumo wa Uber; na (ii) wanaopokea ofa hii moja kwa moja kutoka kwa Uber na kuiona kwenye kifuatiliaji cha hakikisho katika App ya Uber Driver; (iii) wamepewa idhini ya kuendesha gari au kusafirisha bidhaa kwa kutumia Uber; na (iv) wanaokamilisha idadi ya safari watu au oda zinazoonekana kwenye kifuatiliaji cha hakikisho katika miji walikosajiliwa ndani ya siku zilizobainishwa za usajili. Huenda vigezo na masharti ya ofa kama vile idadi ya safari za watu au oda na zawadi, zikatofautiana kulingana na eneo. Ofa unayohakikishiwa na unayoona kwenye App inachukua nafasi ya pesa zozote ulizohakikishiwa na Uber hapo awali.

Mapato yanayotokana na safari zako (baada ya ada ya huduma na matozo mengine, kama vile ada za jiji au serikali za mitaa) yanahesabiwa katika kipato unachohakikishiwa; bakshishi na ofa zozote unazopata huongezwa kwenye kiasi hicho. Mapato yanayotokana na usafirishaji wa chakula (baada ya ada za huduma na tozo zingine, kama vile ada za jiji au serikali za mitaa) na ofa za Eats Boost hujumuishwa kwenye jumla ya ofa yako; bakshishi na ofa zozote za ziada unazopata huongezwa kwenye kiasi hicho.

Malipo yoyote unayodai yatawekwa kiotomatiki kwenye akaunti yako baada ya kukamilisha safari zinazotakiwa. Kila usafirishaji wa oda au wasafiri huhesabiwa mara moja kwenye idadi ya chini inayotakiwa. Usafirishaji ulioghairiwa wa watu au oda hauhesabiwi. Ofa hii inatumika tu kwa watu walioipokea kutoka Uber (kupitia barua pepe, tangazo, ukurasa wa wavuti au kiungo maalum cha mwaliko) na kutimiza masharti ya ustahiki. Uber ina haki ya kutolipa au kukata malipo ambayo inabaini au inaamini kwamba yalifanywa kimakosa, kwa ulaghai, kinyume cha sheria au yanayokiuka vigezo na masharti ya madereva au masharti haya. Ofa ni ya muda mfupi tu. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.