Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Tunavyoshughulikia COVID-19

Kipaumbele chetu ni usalama na afya ya kila mtu anayetumia Uber. Tunaendelea' kuongeza mbinu tunazotumia kukabili COVID-19 kupitia vipengele vipya kwa watumiaji wetu, usaidizi kwa wale wanaotengeneza pesa kwenye mfumo wetu, ushirikiano na mikakati inayohudumia miji yetu.

Tumejitolea kusaidia

Tunaahidi safari milioni 10 bila malipo na usafirishaji wa chakula kwa wahudumu wa afya, wakongwe na watu wenye uhitaji kote ulimwenguni.

Kusaidia wafanyakazi wa huduma za afya

Uber inawapa usafiri wa bila malipo wafanyakazi wa huduma ya afya wa mstari wa mbele, na kuwasaidia kufika na kutoka kwenye nyumba za wagonjwa na vilevile kati ya vituo vya huduma ya afya."

Kulisha watoa huduma ya dharura

Katika masoko ambapo Uber Eats inapatikana, tunawapa watoa huduma wa mstari wa kwanza na wa huduma ya matibabu chakula kwa kushirikiana na serikali za mitaa.

Tunasaidia migahawa nchini mwako

Katika baadhi ya maeneo, tumeondoa Ada ya Kusafirisha Chakula kwa migahawa inayojitegemea kwenye Uber Eats *

Vifaa vya kuhamia

Katika masoko ambapo Uber Freight inafanya kazi, usafirishaji wa bidhaa muhimu unafanywa kwa nauli isiyo na faida yoyote.

Kusaidia mamlaka za afya

Tumeweka kipaumbele kwenye usalama na afya ya kila mtu anayetumia Uber. Tunaunga mkono juhudi za serikali na miji mbalimbali katika vita dhidi ya janga la COVID-19.

Maelezo muhimu kwa madereva na watu wanaosafirisha chakula

 • Tunajitahidi kuwapa madereva na washirika wanaosafirisha chakula chaguo la kufikia dawa za kuua viini ili kuwasaidia waendelee kusafisha magari yao. Bidhaa zinapatikana kwa ugumu mno, kwa hivyo tunawapa kipaumbele madereva na washirika wa kusafirisha mizigo katika miji yenye uhitaji mkubwa *.

 • Wateja wa Uber Eats wana chaguo la kuchagua jinsi wanavyopenda 'oda zao kusafirishwa , ikiwa ni pamoja na kuchagua "Weka mlangoni "wakati wanakamilisha oda.

 • Tuna timu inayoshirikiana na wataalam kutoka idara ya kutoa msaada saa 24/7 katika kukabiliana na mlipuko huu. Kwa kushirikiana nao, tunaweza kufunga kwa muda akaunti za wasafiri na madereva waliothibitika kuwa na COVID-19 au walio na uwezekano mkubwa wa kuwa na ugonjwa huo. Tunapata ushauri wa wataalamu wa magonjwa ya mlipuko ili kuhakikisha kwamba hatua tunazochukua kama kampuni zinazingatia ushauri wa kitiba.

 • Hupaswi kuwa na wsiwasi wowote kuhusu kupoteza hadhi yako ya Uber Pro. Tunalinda hadhi ya sasa ya Uber Pro ya kila dereva katika kipindi kilichosalia cha ustahiki.

 • Ikiwa uko 'katika soko linalotoa huduma za ukodishaji wa magari, tumeshirikiana na washirika wetu wa ukodishaji wa kimataifa ili kuhakikisha kwamba dereva yeyote anayetambuliwa kuwa na COVID ‑ 19 au mtu mmoja aliyetengwa, anaweza kurejesha gari lake bila adhabu yoyote. Katika baadhi ya maeneo, washirika wa ukodishaji hawaruhusu dereva yeyote anayetaka kurudisha gari alilokodisha.

Mbinu za kujikinga na maambukizi

Tunamkumbusha kila mtu anayetumia Uber kufuata ushauri wa wizara ya afya. Ikiwa wewe ni mgonjwa, kaa nyumbani na usitangamane na watu wengine. Nawa mikono mara kwa mara na hakikisha unafunika kinywa chako unapokohoa au kupiga chafya. Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti ya Shirika la Afya Duniani.

Kwa madereva na washirika wanaosafirisha chakula

 • La muhimu zaidi, usiendeshe gari au kusafirisha chakula ikiwa unajihisi mgonjwa.

  Jambo muhimu zaidi unaloweza kufanya kwa sasa ni kukaa nyumbani ikiwezekana.

  Jambo hili ni muhimu zaidi ikiwa unaugua. Jambo hili litazuia kuenea kwa virusi. Hebu na tudumishe usalama wa madereva wetu na kuhakikisha kwamba safari zinapatikana kwa wale tu wanaozihitaji.

 • Ikiwa unaendesha gari

  • Funika kinywa na pua yako. Ukipiga chafya au kukohoa, tafadhali tumia sehemu ya kiwiko chako au kitambaa safi.
  • Waambie wasafiri wasikaribiane Hamna shida ukiwaambia wasafiri waketi nyuma ili msikaribiane.
  • Fungua madirisha ya gari. Ikiwezekana, teremsha vioo ili hewa safi iingie.
 • Ikiwa unasafirisha chakula:

  • Safirisha chakula hadi mlangoni. Ikiwa mteja wa Eats ataagiza chakula, tafadhali kiache mlangoni ili upunguze kugusana.
  • Nawa mikono yako. Tafadhali safisha mikono yako au utumie kitakasa mikono mara nyingi iwezekanavyo.
1/3

Wateja wa Uber

 • Kaa nyumbani ikiwezekana

  Jambo muhimu zaidi unaloweza kufanya kwa sasa ni kukaa nyumbani ikiwezekana.

  Jambo hili ni muhimu zaidi ikiwa unaugua. Jambo hili litazuia kuenea kwa virusi. Hebu na tudumishe usalama wa madereva wetu na kuhakikisha kwamba safari zinapatikana kwa wale tu wanaozihitaji.

 • Unaposafiri:

  • Nawa mikono yako. Baada na kabla ya kusafiri.
  • Funika mdomo na pua yako. Ukipiga chafya au kukohoa, tafadhali tumia sehemu ya kiwiko chako au kitambaa safi.
  • Keti nyuma. Mpe dereva wako nafasi kwa kuketi nyuma.
  • Fungua madirisha ya gari. Ikiwezekana, teremsha kioo ili kupisha hewa.
1/2