Ufikivu
Kutoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa kila mtu.
Ubora wa teknolojia yetu unatambulika tu ikiwa idadi kubwa ya watu wanaweza kuitumia. Kipaumbele chetu ni kuondoa vikwazo, ili kila mtu, bila kujali uwezo wake, aweze kusafiri kwa urahisi.
Kuimarisha ufikivu kwenye bidhaa zetu
App hii imeundwa ili uweze kutoa aina muafaka za usafiri kwa watu wengi kadri iwezekanavyo, wakiwemo walio na ulemavu au wanaohitaji usaidizi wa ziada.
WAV
WAV huwakutanisha wasafiri walio na matatizo ya kutembea na madereva wenye magari yanayoweza kupandwa na wasafiri walio kwenye viti vya magurudumu kwa kutumia ngazi au lifti maalum. Huduma hii inapatikana na inaendelea kupanuliwa katika miji mbalimbali kote Marekani. Ili kurahisisha usafiri mijini kwa wanaotumia viti vya magurudumu, teknolojia ya WAV inatumiwa pamoja na wahudumu wa teksi kote duniani.
Assist
Mfumo wa Assist huwakutanisha wasafiri na madereva wenye tathmini ya juu waliopokea mafunzo ya kuwasaidia wasafiri ambao wanahitaji kusaidiwa. Huduma hii sasa inapatikana katika zaidi ya miji 70 kote duniani.
Uber Health
Uber Health ni huduma ya usafiri usio wa dharura na imebuniwa ili kutimiza kanuni za HIPAA. Inawasaidia wagonjwa na walezi wao kwenda na kutoka kupokea kwenye vituo vya matibabu.
Wanyama wa kutoa huduma
Madereva washirika wa Uber wamepokea maelezo ya kuwasaidia kuelewa wajibu wao wa kuwakubali wasafiri walio na wanyama wa kutoa huduma.
Mifumo ya kusoma skrini
Ukiwa na VoiceOver kwenye iOS, TalkBack kwenye Android na Nuktanundu isiyotumia waya, App hizi zitarahisisha usafiri kwa walio na ulemavu wa kuona wanaposafiri. Vilevile, malipo ya elektroniki hayahitaji shughuli za kuhesabu au kubadilisha sarafu.
Ufikivu kwenye iOS
Ufikivu kwenye Android
App ya Dereva
Madereva wanaweza kujitambulisha kwamba wana ulemavu au matatizo ya kusikia katika App ya Dereva ili waweze kutumia vipengele vinavyowarahisishia kuendesha gari na kuwasiliana na wasafiri.
Madereva walio na matatizo au ulemavu wa kusikia
Kila mwezi, maelfu ya madereva wa Uber walio na matatizo na ulemavu wa kusikia husafirisha watu wengi zaidi nchini Marekani kuliko madereva wengine kwa wastani.
Kushirikiana na mashirika yanayoongoza katika shughuli za ufikivu
Ushirikiano wetu na Tume ya Huduma za Mawasiliano kwa walio na Ulemavu wa Kusikia, Muungano wa Kitaifa wa Walio na Ulemavu wa Kusikia na shirika la Telecommunications for the Deaf and Hard of Hearing Inc. (TDI) hutusaidia kuendelea kubuni vipengele na mikakati ya kuboresha safari kwa madereva walio na ulemavu wa kusikia.
Uber ilitajwa kuwa Kampuni Bora na Taasisi ya Ruderman 2016
Mnamo Septemba 2016, Uber ilituzwa na Ruderman Family Foundation kuwa miongoni mwa kampuni 18 zinazoongoza katika kuwasaidia watu wenye ulemavu.
Anza mazungumzo
Katika kuadhimisha Mwezi wa Uhamasisho kuhusu Ulemavu wa Kusikia, tumeanzisha zana mpya ya kuwasaidia wasafiri kuwasiliana na madereva walio na matatizo au ulemavu wa kusikia kwa kuwafundisha kauli rahisi za Lughaalama ya Marekani.
Njia zaidi za kubuni fursa za kazi
Kampuni