Jinsi ya kutumia App ya Uber
Huduma yetu ya msingi ni kubuni teknolojia inayowakutanisha madereva na wasafiri panapohitajika. Hivi ndivyo App inavyofanya kazi, hatua kwa hatua:
Msafiri hufungua App
Msafiri anaweka mahali anakoenda kwenye kisanduku cha “Unakwenda wapi?”; hukagua kila aina ya usafiri kulingana na ukubwa wa gari, bei na muda unaokadiriwa kuwasili; kisha anathibitisha kuchukuliwa.
Msafiri hukutanishwa na dereva
Dereva aliye karibu huona na kukubali ombi la usafiri. Msafiri huarifiwa kiotomatiki wakati gari la dereva limebakisha dakika 1 kuwasili.
Dereva humchukua msafiri
Dereva na msafiri huthibitisha majina yao na mahali msafiri unakoenda. Kisha dereva huanzisha safari.
Dereva humpeleka msafiri mahali anakoenda
App humpa dereva chaguo la kufikia maelekezo ya hatua kwa hatua.
Dereva na msafiri hutoa tathmini na maoni
Mwishoni mwa kila safari, madereva na wasafiri wanaweza kutathminiana, kuanzia tathmini ya nyota 1 hadi 5. Wasafiri pia wana chaguo la kumpa dereva pongezi na kutoa bakshishi moja kwa moja kwenye App.
Jisajili leo
Uko tayari kujaribu huduma ya Uber? Kubali safari ya kwanza ukiwa msafiri au anza kuendesha gari ukiwa dereva ili utengeneze pesa.
Njia ambazo watu hutumia kusafiri kote ulimwenguni
App ya Uber inakupa uwezo wa kufika unakotaka kwenda kwa kutumia aina mbalimbali za usafiri katika zaidi ya miji 10,000.
App ya wasafiri
Fika unakoenda kwa njia rahisi na salama kwa kubonyeza kitufe tu. Chagua aina ya usafiri unaokidhi mahitaji yako.
App ya madereva
Ukiwa na App ya Driver, uamuzi ni wako. App ya Driver ina vipengele vinavyokusaidia kutoa uamuzi kuhusu mahali, wakati na jinsi ya kutengeneza pesa.
Kampuni