Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kutuhusu

Tunafikiria upya jinsi ulimwengu unavyoendelea kuwa bora.

Kazi yetu ni usafiri. Ndicho kiini chetu. Ni uhai wetu. Ndio unaotutoa kitandani kila asubuhi. Unatuhimiza daima kufikiria upya kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha huduma yetu. Kwa ajili yako. Kwa maeneo yote unayotaka kwenda. Kwa vitu vyote unavyotaka kupata. Kwa njia zote unazotaka kujipatia mapato. Ulimwenguni kote. Katika wakati halisi. Kwa kasi ya ajabu ya wakati huu.

  • Sisi ni Uber. Watu tunaojituma. Aina ya watu wasiokata tamaa kuhusu dhamira yetu ya kusaidia watu kwenda popote na kupata chochote na kujipatia mapato jinsi wanavyopenda. Kazi yetu ni usafiri. Ndicho kiini chetu. Ni uhai wetu. Ndio unaotutoa kitandani kila asubuhi. Unatuhimiza daima kufikiria upya kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha huduma yetu. Kwa ajili yako. Kwa maeneo yote unayotaka kwenda. Kwa vitu vyote unavyotaka kupata. Kwa njia zote unazotaka kujipatia mapato. Ulimwenguni kote. Katika wakati halisi. Kwa kasi ya ajabu ya wakati huu.

    Sisi ni kampuni ya kiteknolojia ambayo inauunganisha ulimwengu halisi na wa kidijitali ili kuwezesha usafiri kwa kubofya kitufe tu. Kwa sababu tunaamini katika ulimwengu ambapo usafiri unapaswa kupatikana. Ili uweze kusafiri na kujipatia mapato kwa usalama. Kwa namna ambayo ni endelevu kwa ajili ya sayari yetu. Na bila kujali jinsia, mbari, dini, uwezo au mwelekeo wako wa kingono, tunatetea haki yako ya kusafiri na kujipatia mapato kwa uhuru bila woga. Bila shaka, wakati mwingine sisi hukosea. Lakini hatuogopi kushindwa, kwa sababu kunatufanya tuwe bora zaidi, wenye hekima zaidi na imara zaidi. Na kunatufanya tujizatiti zaidi kufanya jambo linalofaa kwa wateja wetu, jumuiya za maeneo husika na miji na washirika wetu anuwai wa kimataifa.

    Wazo la kuanzisha Uber lilitokea katika usiku mmoja wenye theluji jijini Paris mwaka 2008 na tangu wakati huo vinasaba vyetu vya ubunifu na uvumbuzi bado vinaendelea. Tumekua na kuwa tovuti ya kimataifa inayowezesha mapato yanayoweza kubadilika na usafiri wa watu na vitu kwa njia zinazoendelea kupanuka. Tumeanzia kwenye magari yenye magurudumu 4 na hadi vyombo vyenye magurudumu 2 na hatimaye malori ya kusafirisha mizigo yenye magurudumu 18. Kuanzia vyakula vya kuchukuliwa mgahawani hadi bidhaa muhimu za kila siku hadi maagizo ya dawa hadi karibu chochote unachohitaji wakati wowote na kujipatia mapato jinsi unavyopenda. Kuanzia madereva ambao rekodi zao za uhalifu zimekaguliwa hadi uthibitishaji wa wakati halisi, usalama ni jambo linalopewa kipaumbele kila siku. Hapa Uber, jitihada za ubunifu hazimaliziki, haziwezi kusimama na siku zote ni mwanzo tu.

Barua kutoka kwa Afisa Mkuu Mtendaji

Soma kuhusu ahadi ya timu yetu ya kumpa kila mtu kwenye tovuti yetu ya kimataifa teknolojia inayoweza kumsaidia afanikiwe.

Uendelevu

Uber imejizatiti kuhakikisha kwamba magari yake yote yanatumia umeme na hayachafui mazingira kufikia mwaka 2040, huku asilimia 100 ya safari zikifanyika katika magari yasiyochafua mazingira, kwenye usafiri wa umma au kwa kutumia magari madogo. Ni jukumu letu kama mfumo mkubwa zaidi wa usafiri duniani kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Tutafanya hivyo kwa kuwapa wasafiri njia zaidi za kusafiri bila kuchafua mazingira, kuwasaidia madereva kuhamia kwenye magari yanayotumia umeme, kufanya uwazi uwe kipaumbele na kushirikiana na NGO na sekta binafsi ili kusaidia kuharakisha mabadiliko katika matumizi ya nishati isiyochafua mazingira.

Usafiri na mengineyo

Mbali na kuwasaidia wasafiri kuweza kutoka sehemu moja hadi nyingine, tunawasaidia watu kuagiza chakula haraka na kwa bei nafuu, tukiondoa vizuizi kwa huduma ya afya, kuunda suluhisho mpya za kuweka nafasi ya kusafirisha mizigo na kuzisaidia kampuni kuwapa wafanyakazi wao huduma shwari za usafiri. Tunawasaidia madereva na matarishi kujipatia mapato kila wakati.

Tunaupa usalama wako kipaumbele

Tunathamini sana usalama wa wasafiri na madereva. Tumejitolea kutimiza wajibu wetu na tunaipa teknolojia kipaumbele. Tunashirikiana na watetezi wa usalama na kubuni teknolojia na mifumo mipya ili kuboresha usalama na kusaidia kurahisisha safari za kila mtu.

Maelezo ya kampuni

Wanaoendeleza Uber

Tunaunda utaratibu ndani ya Uber unaosisitiza kufanya jambo linalofaa kwa wakati unaofaa kwa manufaa ya wasafiri, madereva na wafanyakazi. Pata maelezo zaidi kuhusu timu inayotuongoza.

Kufahamu uanuwai

Tungependa kudumisha mazingira ya kazi ambayo ni jumuishi na yanayoonyesha uanuwai wa miji tunayohudumia, ambapo kila mtu anaweza kuwa jinsi alivyo kihalisi na ambako uhalisia wa kila mtu unathaminiwa na kuchukuliwa kuwa uthabiti. Kwa kuunda mazingira ambapo watu kutoka matabaka yote wanaweza kufaulu, tutaifanya Uber iwe kampuni bora zaidi, kwa ajili ya wafanyakazi na wateja wetu.

Kutenda kwa uadilifu

Hati ya Mpango wa Maadili na Uzingatiaji ya Uber inaelezea ahadi yetu ya kudumisha uadilifu wa viwango vya juu kabisa ndani ya kampuni. Uwazi ni muhimu katika utamaduni wa kimaadili; tunafanikisha hili kupitia Nambari yetu ya Simu ya Msaada ya Uadilifu na miradi kadhaa ya uzingatiaji inayokua na yenye ufanisi.

Pata maelezo ya hivi karibuni zaidi

Chumba cha Habari

Pata matangazo kuhusu ushirikiano, mabadiliko kwenye programu, mipango na mengi zaidi katika eneo lako na kimataifa.

Blogu

Pata maeneo mapya ya kuvinjari na upate maelezo kuhusu huduma za Uber, ushirikiano na kadhalika.

Mahusiano na wawekezaji

Pakua ripoti za kifedha, angalia mipango ya robo mwaka ijayo na usome kuhusu mipango yetu ya kuboresha maisha ya wanajumuiya.

Njoo uwe mbunifu pamoja nasi