Chagua iwapo ungependa kupokea taarifa kuhusu bidhaa, mapendekezo au ofa maalum. Tafadhali kumbuka kuwa ukiamua kujiondoa, bado utapokea ujumbe usiohusu ofa, kama vile stakabadhi za safari zako au maelezo kuhusu akaunti yako. Asante kwa kutumia Uber.
jiondoe
barua pepe
Andika anwani ya barua pepe yako ikiwa hupendelei kupokea barua pepe kutoka Uber.
Unaweza pia kubofya 'Jiondoe' katika sehemu ya chini ya barua pepe yoyote. Tafadhali kumbuka kuwa huwezi kujiondoa ili usipokee barua pepe za shughuli za usafiri, ikijumuisha stakabadhi za safari na majibu ya usaidizi.
Ikiwa ungependa kurejelea mawasiliano kupitia barua pepe, wasiliana na Kituo cha Usaidizi katika ukurasa wa Usaidizi.
SMS
Ili uache kupokea SMS zote kutoka Uber, jibu kwa kutuma neno “STOP” kwa +14152370403. Ili uache kupokea SMS nchini <strong>Kolombia</strong>, jibu kwa kutuma neno STOP kwa +573009110122. Katika baadhi ya maeneo, unaweza kujibu ujumbe wowote kwa kutuma neno STOP au UBER STOP ili usipokee SMS. Unaweza kujisajili tena kwa kujibu ujumbe wowote kwa kutuma neno START. Unaweza pia kujisajili tena kwa kuwasiliana na Kituo cha Usaidizi kwa wateja kupitia ukurasa wa Usaidizi. Huenda ukatozwa ada za kutuma ujumbe na kutumia data.
Arifa za Programu
Ikiwa ungependa kujiondoa usipokee Arifa za programu, unaweza kufanya hivyo kwa kutumia simu yako kwa kufuata maelekezo yaliyo hapa chini. Unaweza kurejesha mawasiliano kwenye simu yako wakati wowote.
Kwa simu za IOS:
- Gusa "Mipangilio" kwenye skrini ya kwanza
- Sogeza chini ili uchague programu ya Uber
- Gusa “Arifa”
- Zima kipengele cha “Ruhusu Arifa”
Kwa Simu za Android:
- Gusa "Mipangilio" kwenye skrini ya kwanza
- Gusa “Programu na Arifa”
- Chagua programu ya Uber
- Chagua kuzima “Ruhusu Arifa” ili uzime arifa zote au zima “Mapunguzo na Taarifa” au “Taarifa za Safari na Akaunti”