Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Tunakuletea mpango wa Uber Rewards

Mpango wa Uber Rewards unakusaidia upate pointi na manufaa. Kwa hivyo, kadri unavyozidi kusafiri ndivyo unavyonufaika. Ili ujue ikiwa mpango wa Uber Rewards unapatikana katika eneo lako, angalia mwaliko kwenye App yako. Iwapo bado, tutauanzisha hivi karibuni. Asante kwa subira yako tunaposambaza huduma za Uber Rewards kila mahali.

Jipatie pointi ukisafiri na kutumia Uber Eats

Jipatie pointi kwa kila dola unayotumia kulipia usafiri na Uber Eats na upate zawadi kwa kila pointi 500. Pia utapata pointi 2x kwenye UberX na 3x kwenye usafiri wa Uber Black.¹

Pata manufaa katika kila kiwango

Iwe unaanza au unasafiri kwa Uber kwenda popote, unaweza kujipatia pointi au manufaa katika kila kiwango cha uanachama.²

Pata maelezo kuhusu utaratibu wa Uber Rewards

Jishindie pointi 1 kwa kila dola unayotumia kulipia huduma za Uber Eats na safari za Pool.

Jipatie pointi 2 kwa kila dola unayotumia kulipia usafiri wa UberX, UberXL au Select.

Jipatie pointi 3 kwa kila dola unayotumia kulipia usafiri wa Uber Black na Uber Black SUV.

Maswali Yanayoulizwa Sana

  • Manufaa yote unayoweza kupata yanategemea kiwango chako cha uanachama. Unaweza kuangalia chati ya ulinganishi iliyo hapo juu ili kuelewa manufaa yanayopatikana katika kila kiwango. Angalia Vigezo na Masharti ya Manufaa ili upate maelezo..

  • Uber Cash ndiyo njia mpya na rahisi ya kulipia safari za Uber na Uber Eats kwa kuwa inakupa njia bora za kuokoa hela. Ukiwa na uanachama wa Uber Rewards, unaweza kubadilisha pointi za zawadi upate $5 za Uber Cash unapofikisha pointi 500. Na unaweza kupunguziwa ada kwa hadi 5% kwa pesa unazoweka kwenye salio lako. Hii ina maana kwamba unalipa pesa kidogo na unapata manufaa zaidi. Angalia Vigezo na Masharti ya Manufaa ili upate maelezo..

  • Mpango wa Uber Rewards utakapopatikana katika eneo lako, skrini ya kujisajili itatokeza kwenye App ya Uber na/au utapata mwaliko kupitia barua pepe utakaokuomba ujiunge na mpango huu.'

  • Kwa sasa, huwezi kupata pointi kwa kuendesha baiskeli au skuta. Lakini tunapanga kuzijumuisha kwenye mpango wa Uber Rewards hivi karibuni.

¹Haijumuishi UberTaxi, baiskeli na skuta. Masharti mengine yatazingatiwa. Angalia Vigezo na Masharti ya Manufaa ili upate maelezo..

²Viwango vya uanachama ni Blue (pointi 0 ili ustahiki), Gold (pointi 500 ili ustahiki), Platinum (pointi 2,500 ili ustahiki) na Diamond (pointi 7,500 ili ustahiki). Angalia Vigezo na Masharti ya Mpango ili upate maelezo..