Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Endesha gari lako bila wasiwasi

Ni haki yako kwenda mahali popote penye wasafiri. Tumia huduma yetu kuendesha gari na teknolojia inayosaidia kulinda usalama wako na wengine walio karibu nawe.

Barakoa hazihitajiki tena

Kufikia tarehe 19 Aprili, 2022, wasafiri na madereva hawahitajiki kuvaa barakoa wanapotumia Uber. Hata hivyo, CDC bado inapendekeza uvae barakoa ikiwa una sababu fulani binafsi za hatari na/au viwango vya juu vya maambukizi katika eneo lako.

Kumbuka: watu wengi bado wanajihisi salama zaidi wanapovaa barakoa kwa sababu ya hali ya afya binafsi au ya familia, kwa hivyo tafadhali heshimu mapendeleo yao. Na ukihisi wasiwasi, unaweza kughairi safari wakati wowote.

Tunasasisha sera yetu ya kutoketi kwenye kiti cha mbele

Wasafiri hawalazimiki tena kuketi kwenye kiti cha nyuma. Hata hivyo, ili kukupa nafasi zaidi, bado tunawaomba wasafiri watumie kiti cha mbele pekee ikiwa inahitajika kwa sababu ya ukubwa wa kikundi chao.

Asante kwa kusaidia kutunzana

Tunajua kwamba janga la ugonjwa limekuwa gumu. Lakini umeendelea kufanya zaidi ya ulivyotarajiwa ili kusaidia kulinda jumuiya zetu, iwe ni kuvaa barakoa, kuachiana nafasi au kuwasaidia watu kupata chakula wanachohitaji. Asante kwa mchango wako.

Bado ni muhimu kuchukua tahadhari za usalama unapoendesha gari na kusafirisha bidhaa. Kwa hivyo hakikisha kwamba unafungua madirisha kwa ajili ya mtiririko wa ziada wa hewa, unatakasa mikono yako kabla na baada ya safari au usafirishaji wa bidhaa na kila mara ufunike kinywa chako unapokohoa au kupiga chafya.

Tunahakikisha unapata huduma salama

Vipengele vinavyokusaidia kuimarisha usalama wako

App hii inatumia teknolojia itakayokusaidia kuwasiliana na ndugu na marafiki, timu yetu, na mamlaka zinazoshughulikia dharura, ili upate ufanisi mkubwa.

Kuna usaidizi wakati wowote

Timu ya matukio ya dharura iliyo na ujuzi maalum iko tayari kukuhudumia wakati wowote kupitia App.

Jumuiya inayojali maslahi ya kila mtu

Kupitia juhudi zetu za pamoja na kushirikiana na miji na wataalamu wa usalama, tumesaidiana kufanya safari ziwe salama kwa kila mtu.

Utulivu wa mawazo, popote uendapo

Huduma hii imeundwa ili kulinda usalama wako. Ili usiwe na wasiwasi wowote unapoendesha gari. Ili uwaambie ndugu na marafiki mahali unakoenda. Kwa hiyo, chochote kikitokea una uhakika kwamba kuna mtu atakayekusaidia.*

Kitufe cha usaidizi wa dharura

Unaweza kutumia kitufe cha dharura kwenye programu kupigia simu na kuita usaidizi unapouhitaji. Programu hii inaonesha mahali ulipo na taarifa nyingine kuhusu safari, ili uweze kuwasiliana na kitengo cha dharura tatizo lolote likitokea.

Usaidizi kwa wateja wakati wowote

Wataalamu wa matukio ya dharura kutoka Uber wako tayari kukusaidia usiku na mchana.

Fuatilia Safari Yangu

Ndugu na marafiki wanaweza kufuatilia barabara unayotumia na watajua mara tu unapowasili.

Tathmini kutoka pande mbili

Maoni yako ni muhimu sana. Tunaweka kumbukumbu ya safari zenye tathmini za chini, watumiaji husika wanaweza kuondolewa ili kulinda ya jamii ya Uber.

Ufuatiliaji wa GPS

Safari zote za Uber hufuatiliwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kwa hiyo tuna kumbukumbu ya kila kitu iwapo lolote litatokea.

RideCheck

Kwa kutumia sensa na data ya GPS, RideCheck inaweza kusaidia kutambua iwapo safari ina kituo cha kusimama kwa muda mrefu ambacho hakikutarajiwa. Ikiwa inayo, 'tutawasiliana na wewe kujua hali yako na kukupa zana za kukusaidia.¹

Thibitisha PIN Yako

Huenda ukalazimika kuweka PIN ya msafiri wako kabla ya kuanza safari kwenye App. Uthibitishaji wa PIN husaidia kuhakikisha kuwa msafiri sahihi ndiye anayeabiri gari lako, na inakuruhusu wewe na msafiri wako msafiri mkiwa na utulivu wa mawazo.

Huduma unayoweza kutegemea wakati wowote

Uber inashirikiana na kampuni maarufu za bima ili kukulinda unaposafiri.

Vidokezo vya kufanikisha kuchukuliwa kwa usalama

Tunaupa usalama wako kipaumbele. Hiyo ndiyo sababu tunakuomba wewe pamoja na wasafiri wako mchunguze maelezo yote kwa makini kabla ya kuingia kwenye gari, ili kuhakikisha kwamba kuna utulivu wa akili kuanzia mwanzo wa safari.

Usalama wa msafiri

Kabla ya safari kuanza, wasafiri hushauriwa waangalie kipande cha nambari ya gari lako, aina na muundo wa gari, pamoja na picha na jina lako kama dereva.

Usalama wa dereva

Unaweza pia kuwaomba wasafiri wathibitishe jina lako. Unaweza kusema, “Habari, dereva unayemtarajia anaitwa nani?” au “Unaweza kuthibitisha jina langu? Linapaswa kuonekana kwenye programu yako.”

Tunakushukuru kwa kuimarisha usalama barabarani

Wewe ni nguzo muhimu katika kusaidia kuimarisha usalama katika miji yetu na kufanya mazingira ya barabarani kuwa salama kwa kila mtu.

Hakikisha unakuwa mwangalifu unapokuwa barabarani

App hii inakukumbusha upumzike ukikaribia upeo wa muda wa kuendesha gari, uliobainishwa na jiji lako.

Vidokezo vya usalama

Sheria na ushauri wa eneo lako kutoka kwa maafisa wa utekelezaji wa sheria zinakupa njia ambazo unaweza kusaidia kuimarisha zaidi usalama wako na ule wa watu walio karibu nawe. Soma vidokezo zaidi vya usalama hapa.

Tunaimarisha jumuiya yetu

Mwongozo wa Jumuiya ya Uber huwasaidia wasafiri na madereva kufurahia usafiri bila wasiwasi. Mtu yeyote ambaye hatazingatia mwongozo huu anaweza kuondolewa kwenye mfumo wetu kwa ajili ya usalama wa Jumuiya ya Uber.

*Baadhi ya masharti na vipengee hutofautiana kulingana na eneo na huenda havipatikani.

¹ Bado tunasambaza kipengele hiki na kwa sasa kinapatikana katika baadhi ya maeneo tu.