Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Bima ya ajali kutoka Britam

Bima ya ajali kutoka Britam

Wakati mwingine ajali hutokea. Kwa hivyo ni vizuri kufahamu kwamba utafidiwa gharama za matibabu na ukipoteza fursa za kutengeneza mapato.

Maelezo muhimu

Unapokuwa na bima

Kuanzia tarehe ya uzinduzi

Mpango wa Bima ya Majeraha kwa Washirika unaanza tarehe 21 Desemba 2018.

Inakulinda unapokuwa kwenye Safari

Unalindwa kuanzia unapokubali ombi la kumsafirisha abiria au chakula, hadi wakati unapokamilisha safari au kufikisha chakula.

Bima hii inamlinda nani?

Wasafiri na madereva kwenye Uber wanalindwa kwa bima. Bima inategemea vigezo na masharti.

Hali hii inamaanisha nini?

Utaratibu wake

Hati za ziada

Kwa madereva washirika

Maelezo kamili ya bima na matukio yasiyofidiwa.

Maswali Yanayoulizwa Sana

  • Bima ya Majeraha kwa Washirika huwalinda dhidi ya matukio mahususi yanayotokea wakati Msafiri au Mshirika wa Dereva Yuko Safarini. Sifa kuu za bima zimeorodheshwa hapa chini. Kwa maelezo kamili tafadhali soma maelezo haya kutoka Britam.

    Gharama za matibabu: Kama ajali itatokea ukiwa safarini, bima hii itakurejeshea gharama zote za matibabu ulizolipa baada ya ajali (k.m eksirei, huduma, dawa) ilimradi gharama hiyo isipite kima kilichowekwa.

    Malipo ya kifo na mazishi: Ikitokea kwamba umepoteza maisha yako kwa sababu ya ajali ukiwa safarini, familia yako au warithi wako watapokea malipo kwa mkupuo mmoja.

    Malipo ya Ulemavu wa Kudumu: Ikiwa kwa bahati mbaya utapata ulemavu kwa sababu ya ajali iliyofanyika ukiwa safarini, utapokea malipo kwa mkupuo mmoja. Kiasi hicho kinategemea kiwango cha ulemavu, jinsi ilivyobainishwa na Britam.

    Manufaa ya Malipo ya Kila Siku (majeraha): Kama utalazwa kwa zaidi ya saa 24 kutokana na ajali iliyotokea ukiwa kazini na baada ya hapo usiweze kufanya kazi kwa sababu ya majeraha hayo, utapokea malipo ya kila siku kwa hadi siku 30 katika kipindi ambacho daktari aliyeidhinishwa atathibitisha kwamba bado huwezi kufanya kazi.

    Malipo ya Usumbufu: Kama Dereva atapata Jeraha la Mwili kutokana na ajali akiwa safarini, na kusababisha kulazwa hospitali kwa muda usiopoungua saa 24 mfululizo, anayetoa bima atamlipa dereva kiasi chote cha bima.

    Kumbuka: Manufaa yote yaliyotajwa hapa juu yanapatikana tu katika hali zilizothibitishwa na daktari. Uber inaweza kubadilisha masharti haya kwa hiari yake.

  • BimaKipindi cha BimaMasharti nchini Tanzania - (TZS)
    Bima ya MatibabuUkiwa SafariniHadi: 1,250,000 Ambulensi ni hadi 500,000
    Malipo ya kifo na matangaUkiwa SafariniKifo:5,000,000: Matanga: 500,000
    Malipo ya Ulemavu wa KudumuUkiwa SafariniHadi 5,000,000
    Malipo ya Kila Siku (kwa majeraha)Ukiwa SafariniKwa Madereva Washirika: 10,000 kwa siku
    Malipo ya usumbufu (majeraha)Ukiwa SafariniKwa Madereva Washirika: 50,000
  • Wakati mwingine ajali hufanyika barabarani. Tungependa kukusaidia kufidia gharama za matibabu na kupoteza fursa za mapato kutokana na majeraha ya ajali Ukiwa Safarini. Tunajivunia kushirikiana na kampuni kubwa ya Britam kwa kuwa mshirika wako barabarani.

  • Tumekuwa tukishirikiana na Britam kubuni bidhaa mpya nchini Tanzania. Sasa huduma hizi zinapatikana kwa Madereva Washirika nchini Tanzania, na pia Wasafiri.

  • Ndiyo, madereva na washirika wote wa Uber wa kusafirisha vyakula sasa wanalindwa, lakini unaweza kukataa ukipenda (soma swali linalofuata ili uelewe jinsi ya kufanya hivyo).

  • Ni wewe utaamua kuingia katika mpango huu wa bima. Unaruhusiwa kuikataa wakati wowote na hutaathirika kwa namna yoyote ile. Ukikataa, hutalindwa tena na Bima ya Majeraha kwa Washirika & Wasafiri, inayojumuisha usaidizi wa gharama za matibabu na kupoteza fursa za mapato endapo utapata ajali ukiwa katika safari ya Uber. Ikiwa una hakika kwamba hutaki ulinzi unaotolewa na Bima ya Majeraha kwa Washirika & Wasafiri, bonyeza hapa ili uweke maelezo yako na uwasilishe ombi la kuikataa, au tembelea Kituo cha Madereva wa Uber kilicho karibu nawe.

  • Ni wewe utaamua kuingia katika mpango huu wa bima. Unaruhusiwa kuikataa wakati wowote na hutaathirika kwa namna yoyote ile. Ukikataa, hutalindwa tena na Bima ya Majeraha kwa Washirika & Wasafiri, inayojumuisha usaidizi wa gharama za matibabu na kupoteza fursa za mapato endapo utapata ajali ukiwa katika safari ya Uber. Ikiwa una hakika kwamba hutaki ulinzi unaotolewa na Bima ya Majeraha kwa Washirika & Wasafiri, bonyeza hapa ili uweke maelezo yako na uwasilishe ombi la kuikataa, au tembelea Kituo cha Madereva wa Uber kilicho karibu nawe.

  • Mshirika & Bima ya Majeraha kwa Wasafiri hutolewa nchini Tanzania ambako Uber inatoa huduma za Usafiri.

  • Hapana, Bima ya Majeraha kwa Washirika haichukui nafasi ya bima ya gari la biashara wala nafasi ya bima kamili ya gari lako. Tafadhali wasiliana na shirika lililokupa bima, muuzaji au wakala ikiwa una maswali yoyote kuhusu bima ya gari lako.

  • Hapana, bima ya matibabu haitumiki badala ya bima ya jumla ya matibabu. Bima inayotolewa kwa ajili ya matibabu inahusiana na ajali zinazotokea Ukiwa Safarini pekee.

  • Huhitaji kufanya jambo lolote. Kuanzia tarehe 21 Disemba 2018 una bima inayojali masilahi yako unapotumia programu ya Uber safarini.

  • Huhitaji kufanya jambo lolote. Una bima inayojali masilahi yako ukiwa safarini kwa kutumia App ya Uber.

  • Sawa na sera nyingi za bima, Bima ya Majeraha ya Washirika & Wasafiri ina matukio na hali za jumla na maalum zisizofidiwa. Tafadhali soma maelezo kamili ya bima na matukio yasiyofidiwa hapa

Bima hii inatolewa kulingana na vigezo na masharti yafuatayo:

  1. Uber inaweza kufutilia mbali, kubadilisha au kurekebisha bima hii wakati wowote kwa hiari yake.
  2. Bima hii inatumiwa na Uber kwa gharama na hiari yake.
  3. Madereva na Washirika Wanaosafirisha Vyakula hawana wajibu au jukumu la kulipia chochote au dhamana zozote zinazohusiana na bima.
  4. Madereva/Washirika wa Kusafirisha Chakula na Uber wanaelewa na kukubali kwamba Dereva/Mshirikwa wa Kusafirisha Chakula anaweza kuamua kujiondoa kwenye Bima wakati wowote kwa kubainisha kwamba hakubali bima hiyo mara anapopokea arifa au ombi. Kukataa bima hakutaathiri uwezo wako wa kutumia Programu ya Uber.
  5. Madereva na Washirika wa Kusafirisha Chakula ni wakandarasi wa kujitegemea . Kwa vyovyote vile, bima hii haianzishi uhusiano wa ajira au matarajio ya kuajiriwa (iwe ni katika mtazamo wa sheria ya leba, sheria ya kodi au sheria ya ustawi wa jamii) kati ya Uber na Dereva au Mshirika wa Kusafirisha Chakula.