Bidhaa

Vidokezo kwa safari salama kipindi hiki cha sikukuu

Tarehe 23 Desemba, 2018 / Tanzania

Kipindi cha sikukuu kimewadia, nasi tupo tayari kukusaidia kufanya maisha yako kuwa rahisi zaidi katika kipindi hiki. Desemba hii, ukiwa unatoka ni muhimu kufikiria usafiri salama wa kukurudisha nyumbani. Iwe ni mtoko wa mchana au hata ukitoka usiku na marafiki, ni muhimu kukumbuku kutumia vipengele vya usalama vya kwenya app yako ya Uber kwa safari salama.

 

Kaa ndani mpaka unapo karibia kuondoka

Uzuri wa Uber ni kwamba unaweza kuita gari ukiwa ndani, ni wewe tu na simu yako.Hauna haja ya kutoka nje, au kwenda kusubiri barabarani – utapewa taarifa usafiri wako ukiwa unakaribia kufika.


Taarifa za kuangalia

Upo tayari kutoka? Hakikisha umeangalia taarifa za gari na dereva kupitia App yako! Hakikisha kwamba:

  • Rangi ya gari niu sawa na ile iliyopo kwenye App yako
  • Aina ya  gari lililo kuja na plate namba, ni sawa na taarifa zilizopo kwenye App yako.
  • Jina na sura ya dereva ni sawa na taarifa zilizopo kwenye App yako.

 

Wataarifu ndugu na jamaa juu ya safari yako

Sasa unaweza kuwataarifu ndugu na marafiki juu ya safari yako kirahisi zaidi! Unaweza kuchagua hadi watu 5 kama watu unaowaamini na ukachagua wapewe taarifa kila unapanda Uber kwa kufuata hatua chache tu. Wanaweza kukufuatilia kwenye safari nzima mpaka pale utakaposhuka.

Na kumbuka, kama una mpango wa kunywa, jiandae mapema – agiza usafiri wako kuhakikisha safari salama wakati wa kurudi nyumbani.