Matangazo ya Madereva

Ulituma maoni na tuliyafanyia kazi

Tarehe 13 Juni, 2018 / Tanzania

Tunatambua kwamba mbali na kuwa dereva wewe ni mama, baba, mwanaridha, mjasiriamali, au una ndoto za kuwa mwanamuziki –  na tungependa ulimwengu wote ujue hilo.

Tumezindua kampeni ya ‘Zaidi ya Kufanya Safari’ – kampeni ambayo italeta mabadiliko chanya katika namna ambavyo watu wanakuchukulia. Kampeni ya ‘Zaidi ya Kufanya Safari’ itawaunganisha wasafiri na madereva, ili kuunda mtandao wa watu wanaoaminiana na kuheshimiana miongoni mwa wadau wa Uber.

Katika kipindi chote cha mwaka huu, tutatumia vyanzo mbalimbali kusambaza hadithi za maisha ya  wasafiri/madereva, matukio muhimu katika kazi yao ya udereva ili watu wapate fursa ya kujua hatua muhimu ulizopiga maishani mwako kupitia mpango wa kila mwezi wa kuwatambua utakaoanza hivi karibuni

Tumekuandalia mambo mazuri. Jiunge nasi tunapopiga hatua hii muhimu.