Matangazo ya Madereva

Tunakuletea Bima ya majeraha unapokuwa safarini

Tarehe 28 Novemba, 2018 / Tanzania

Tunafuraha kubwa kuwataarifu ya kwamba tunaendelea kutimiza ahadi zetu za kuupa usalama wa dereva-mshirika na abiria kipaumbele  nchini Tanzania. Tunawaletea bima kwa ajili ya majeraha kutoka UAP-Old Mutual kuanzia 21 Desemba 2018 – itasaidia sana kukupunguzia mzigo wa mawazo unapotumia Uber.

Madereva-washirika wote, pamoja na wa uberPOA watawekwa kwenye mpango huu bila kuchangia chochote; Kuanzia pale unapopokea safari kwenda kumchukua msafiri, mpaka unapomshusha na kumaliza safari. Bima hii itawalinda wasafiri wanapokuwa kwenye safari za Uber, mpaka pale safari itakapokamilika.

Pale itakapotokea kwamba umepata ajali au umetokea uhalifu wowote utakaopelekea majeraha wakati wa safari ya Uber, msafiri na dereva-mshirika watapata fidia zifutatzo:

  1. Bima ya matibabu:  Ukipata ajali ukiwa kwenye safari ya Uber, bima hii itampa  dereva-mshirika na msafiri hela kwa ajili ya matibabu kiasi kitakachofikia TZS 1 250 000. Zaidi ya hapo bima hii itagharamia huduma za Ambulansi.
  2. Kifo na malipo ya mwisho: Ikitokea bahati mbaya dereva-mshirika au msafiri amefariki kutokana na ajali kwenye safari ya Uber, wategemezi wao au warithi wa mali zao watapata TZS 5 000 000 kwa mkupuo. Pia watapata TZS 500 000 kwa ajili ya gharama za mazishi.
  3. Malipo kwa ajili ya ulemavu wa milele: Ikitokea bahati mbaya mtumiaji wa Uber akapata ulemavu wa milele kutokana na ajali itakayotokea kwenye safari ya Uber, atapata kiasi cha TZS 5 000 000 kwa mkupuo. Kiasi kitategemea na ukubwa wa ulemavu, kama ilivyo elezwa kwenye mwongozo wa UAP-Old Mutual.
  4. Malipo ya kila siku kwa dereva-mshirika (majeruhi): Kama dereva-mshirika atalazwa zaidi ya masaa 48 kutokana na ajali iliyotokea akiwa kwenye safari ya Uber na akashindwa kuendesha gari kutokana na majeraha hayo, atapata malipo ya TZS 10 000 kwa siku 30 wakati wakisubiria kuanza kufanya kazi kama ilivyoshauriwa na daktari.

Bima ya majeraha Tanzania imetengenezwa mahsusi kwa watu waliokuwa kwenye safari za Uber, na imejengwa kutoka kwenye mfumo wa ulinzi na usalama uliopo sasa, huku ikizingatia usalama wa kila safari inayofanywa kwenye App ya Uber. Hii ni moja ya jitihada zetu endelevu katika kusaidia usalama wa dereva-mshirika na msafiri barabarani, na tutaendelea kuimarisha mifumo ili kongeza utulivu wa mawazo mtu anapokuwa kwenye safari za Uber.