Matangazo ya Madereva

Maboresho ya kiteknolojia kurahisisha uendeshaji wako

Tarehe 24 Januari, 2018 / Tanzania

Kila siku dereva-mshirika anawapeleka wasafiri wanapotaka kwenda. Na kila siku tunataka kuhakikisha ya kwamba upo katika miko salama.

Mwaka huu tumepata fursa ya kufikiria ni jinsi gani vipengele vya Uber na teknolojia vinaweza kukusaidia ukiwa barabarani. Matokeo yake ni programu iliyotengenezwa kwa maoni yako – ikiweka mbele usalama kabla, baada na ukiwa safarini. Kama ulikosa vipengele hivi mwaka jana, tupo hapa kwa ajili ya kukukumbusha yote uliyokosa mwaka 2017:

Taarifa ya safari ndefu

Madereva hutaarifiwa kama safari ni ndefu, hii itakusaidi kuamua kama utataka kuichukua au la. Hamna kushtukizwa tena.

Malipo unapo msubiria msafiri

Ikifika dakika 5 baada ya kufika kwenye eneo la kumchukua msafiri, dereva atalipwa kwa dakika akiwa anasubiria kuanzisha safari.

Ulinzi wa nyota

Kama dereva-mshirika akipewa nyota Mbaya kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, kama vile foleni na tatizo la programu, hizi nyota hatiza haribu wastani wake wa nyota.

Shirikisha taarifa za safari

Kama msafiri anavyoweza kuwashirikisha awapendao taarifa za safari na wewe pia unaweza kuwashirisha uwapendao kupitia programu yako ya dereva.

Weka sehemu unapotaka kwenda, na muda unaotaka kufika

Sasa unaweza kuweka sehemu unayotaka kwenda, na muda unaotaka kufika hilo eneo. Sisi tutakusaidia kufika hilo eneo kwa wakati.

Mawasiliano ndani ya app

Unajua ya kwamba dereva na msafiri wanaweza kuwasiliana kupitia progamu ya Uber? Unaweza kuchagua kutuma message au kupiga simu.

Na sio haya tu, yapo maboresho mengi yanakuja. Bado tunazidi kuboresha programu ili iweze kukidhi mahitaji yako.