Ofa

Shindano la #UberFrontSeatChallenge

Tarehe 24 Agosti, 2018 / Tanzania

Shindano la Kukalia Kiti cha Mbele ni mkakati unaolenga kuwasadia madereva na wasafiri kupata muda wa kuhamiana kwa undani zaidi, hasa maisha yao sambamba na kujenga jamii ya Uber inayothamini utu.

Ni mara ngapi umejikuta ukiketi kwenye kiti cha nyuma unapoabiri gari la Uber, na kuanza kuchati kwenye simu yako kisha ukashuka bila kumjulia hali dereva wako zaidi ya kujua jina lake? Tumeanzisha mpango ambao utakuwezesha kumjua dereva wako na unaweza kupata punguzo kwenye safari utakayofanya!

Huu ndio mpango mzima:

1. Unapoita gari la Uber unaketi kwenye kiti cha mbele.
2. Chukua muda wako kufahamu maelezo ya dereva wako.
3. Kwa kutumia taarifa msingi inayopatikana ndani ya app anzisha mazungumzo yatakayokusaidia kumfahamu dereva wako.
4. Tumia mitandao ya jamii ya Twitter au Instagram kutuambia ulichojifunza kwa dereva huyo na hakikisha unatag <Uber_X> na utumie hashtag #UberFrontSeatChallenge.
5. Sasa umeingia kwenye droo hii na unaweza kupata punguzo kubwa kwenye safari yako inayofuata!

Safari bomba na mazungumzo mazuri! Shiriki shindano la #FrontSeatChallenge leo.

  • Terms & Conditions