Matangazo ya Madereva

Shea safari yangu: Kipengele kipya cha dereva-mshirika

Tarehe 20 Novemba, 2017 / Tanzania

Kama vile msafiri anavyoweza kushea safari yake na ndugu zake, sasa na dereva-mshirika anaweza kushea safari yake na awapendao kupitia app ya Uber.

Ndugu na marafiki wanaweza kukuona mwanzo wa safari hadi mwisho wa safari kupitia ramani,.kama unaenda sehemu na hupaamini sana unaweza kushea.

Jinsi inavyofanya kazi:

  1. Nenda kwenye ‘Share My Trip’ kwenye settings za app yako
  2. Chagua namba za simu za watu unaotaka wakuone ukiwa safarini halafu shea safari yako
  3. Watu uliowachagua watakuwa na uwezo wa kukuona kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho

 

Unachotakiwa Ufahamu?


Taarifa za msafiri kama vile sehemu ya kumchua, vituo vyake na sehemu ya kumshusha havitaonyeshwa wakati una shea safari yako.