Matangazo ya Madereva

Mapendeleo ya Aina ya Safari

Tarehe 8 Mei, 2018 / Tanzania

Chagua aina za safari ambazo ungependa kupokea kwa kuweka mapendeleo ya aina ya safari.

Kampuni ya Uber inafanya juhudi endelevu za kutafuta mbinu za kuimarisha huduma unayopata kweye programu ya dereva.

Kupitia kwa maoni uliyotoa, tumegundua kwamba unapenda kuwa na uhuru wa kufanya mambo unayopenda, na ndiyo maana tumezindua kipengele kitakachokusaidia kuweka aina ya safari unazotaka.

Maelezo ya mapendeleo ya aina ya safari.

Ukitumia kipengele hiki utaweza kuchagua aina ya safari ambazo ungependa kupata. Inatumia utaratibu wa kukupa uhuru wa kuwasha na kuzima aina yoyote ya safari ambayo umeidhinishwa kupokea kwenye programu ya Uber.

Utaratibu Inaotumia:

  1. Gusa aikoni ya menyu upande wa juu kulia mwa programu ya Uber.
  2. Gusa aikoni nyeupe ya gia karibu na upande wa juu kulia mwa skrini yako.
  3. Unaweza kuchagua aina ya safari ambazo ungependa  (hungependa) kupokea.

Unaweza kubadilisha mapendeleo yako ya aina ya safari ambazo ungependa kupokea.

Kadhalika, ikiwa hujapata maombi ya safari kwa muda mrefu, utapata ujumbe kwenye programu ya Uber utakaokuomba uatathmini iwapo kuna haja ya kubadilisha aina ya safari ambazo ungependa kupokea.

Mfumo rahisi wa kuweka nauli

Bado utaendelea kushuhudia mfumo rahisi wa kuweka nauli kwa safari zote unazoruhusiwa kufanya, hata kama umezima aina fulani ya safari.  Tunafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba unajua aina ya safari unazoruhusiwa kufanya.

Ingawa hutaweza kupokea aina ya safari ulizozima, unaweza kuwasha kipengele cha safari hizo wakati wowote.  

Je, umeshindwa kuona aina ya safari unayoruhusiwa kufanya?

Ikiwa kuna tatizo lolote linalokuzuia usione aina ya safari unayoruhusiwa kufanya, unashauriwa ufunge na ufungue upya programu yako ya Uber.