Bidhaa

Kutoka kwenye kuchukuliwa mpaka kushushwa: kila kitu unachotakiwa kufahamu

Tarehe 11 Aprili, 2018 / Tanzania

Umesha pakua app yako ya uber, lakini hujui cha kufanya. Tupo hapa kukuwezesha kutumia app yako kwenye mizunguko yako ndani ya mji!

 

Jinsi ya kuagiza usafiri?

Fungua app yako, pata usafir ndani ya mda mfupi na uanze safari yako- hamna tena kuhangaika kutafuta dereva!
- Fungua app yako ya Uber
- Bonyeza ‘where to?’
- Andika unapoelekea
- Hakikisha eneo la kuchukuliwa
- Angalia chini kuchagua aina ya usafiri unaouhitaji

Jinsi tunavyopata nauli?

Nauli inapatikana kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kianzio cha nauli (hii huwa haibadiliki)
- Umbali wa unapoelekea kwa kilometa na muda uliyotumia kwenye safari
- Uhitaji wa usafiri wakati huo

Kwanini nichague Uber?

Kuanzia safari za usiku na marafiki mpaka mambo ya shopping wikiendi, agiza uber popote pale ndani ya dar - masaa 24 wiki nzima. Na zaidi ya hapo unaweza kulipa kwa pesa kamili au kwa kadi ya bank- ni rahisi sana!

Aina za usafiri?

Chagua usafiri unaoupenda baada ya kuandika unapoelekea kwenye app yako:
Chagua uberX kwa zile safari za kila siku ndani ya mji