Bidhaa

Karibu tujibu maswali yako yote kwenye vituo vyetu vya msaada!

Tarehe 9 Mei, 2019 / Tanzania

Sasa msaada wa moja kwa moja umefika!

Kuanzia sasa mpaka tarehe 9 Agosti 2019,unaweza kupata msaada wa moja kwa moja katika vituo vya msaada vya Uber vilivyopo maeneo yafuatayo hapa Dar Es Salaam.

  • Quality Centre Mall – mlango mkuu wa kuingilia
  • Mlimani City Mall – mbele ya Choppies supermarket

Vituo vyetu vya msaada viko wazi kuanzia Jumatatu-Ijumaa, saa 3 asubuhi hadi 11 jioni.

Mawakala wetu wako tayari kukusaidia kwa tatizo lolote na kutoa maelekezo zaidi kuhusu matumizi ya app yetu na vipengele mbalimbali.

Pia kaa tayari kuhudumiwa na wasanii mbalimbali na kujishindia zawadi kabambe!

Ukishindwa kufika kwenye vituo vyetu bado unaweza kupata msaada kupitia app yetu au kututumia ujumbe kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

#UberOn