Bidhaa

Jinsi ya kumtathmini dereva wako

Tarehe 6 Machi, 2017 / Tanzania

Uber imedhamiria kutoa huduma bora kwa pande zote. Njia mojawapo ni kupitia mchakato wa tathmini ya nyota 5 katika kila safari. Wasafiri huwatathmini madereva kulingana na uzoefu wao na madereva hufanya hivyo pia.

Jijini Dar es Salaam, tumeweka kiwango cha  tathmini ambacho  madereva wanatakiwa kukifikia ili kuweza kuingia na kutumia mtandao wa Uber. Kama tathmini yao ikiwa chini ya kiwango kilichopangwa, msafiri – mshirika atazuiwa kutumia Uber kwa muda na atatakiwa kufika ofisini kwaajili ya kurudia mafunzo.

Hii ni sababu ya umuhimu wa kukumbuka kumtathmini dereva wako, hivyo fanya kwa usahihi.

Kuna mambo matatu ya kuzingatia kila unapomtathmini dereva wa Uber, mambo hayo ni:

  • Ubora wa gariJe, gari lilikuwa safi na katika hali nzuri?
  • HudumaJe, dereva – mshirika alikuwa rafiki? Je, huwa wanakuuliza kuhusu chaguo lako la stesheni ya redio, njia au kisi cha joto?
  • Uwezo wa kuendeshaJe, hii ilikuwa safari salama na ya kufurahisha?

Vifuatavyo ni vitu muhimu vya kuzingatia wakati wa kumtathmini dereva wako:

★★★★★ – Hii ilikuwa safari bora. Dereva alikuwa mstaarabu, alikuwa msaada mkubwa kwangu na gari lilikuwa safi. Ulifika eneo ulilokuwa unaelekea kwa wakati na uliweza kutulia na kupumzika. Kwa ujumla, safari ilikuwa nzuri na ulifurahia safari hiyo.

★★★★ – Hii ilikuwa safari ambayo ingeweza kuwa bora zaidi lakini kuna jambo moja tu ambalo halikwenda sawa, jambo hilo linaweza kuwa muda ambao dereva alichukua kuja kukuchukua au uwezo wa dereva wa kutumia GPS haukuwa wa kiwango cha juu.

★★★ –  Ubora wa safari hii ni wa wastani. Umekutana na moja kati ya yafuatayo; dereva hakuwa na mwenendo mzuri wakati wa safari, gari halikuwa katika hali nzuri, au dereva alipotea njia wakati wa safari. Safari yako kwa ujumla haikuwa nzuri.

★★ – Haukuifurahia safari hii. Ulikutana na zaidi ya jambo moja kati ya haya:  dereva hakuwa na mwenendo mzuri wakati wa safari, gari halikuwa katika hali nzuri, au dereva alipotea njia wakati wa safari.
 – Safari hii ilikuwa mbaya sana. Haikukufurahisha kabisa. Dereva alikuwa jeuri na gari halikuwa katika hali nzuri. Safari ilichukua muda mrefu zaidi ya muda uliyokadiriwa kuwa utatumia kwenye safari na dereva alishindwa kabisa kutumia ramani (GPS) kwa usahihi.

Tafadhali usimtathmini dereva kwa kumpa nyota chache kama nauli ilikuwa kubwa kuliko kawaida. Mpatie tathmini kulingana na huduma aliyokupatia tu na kisha tutumie maoni juu ya kutoridhishwa na nauli uliyolipa.

Nyota ya sita kwa dereva washirika: Kama dereva alikuwa bora zaidi au huduma yake ilikuwa nzuri ajabu, tafadhali mpatie tathmini ya nyota 5 na kisha andika maoni kutujulisha juu ya jinsi safari yako ilivyokuwa. Kama safari yako ilikuwa nzuri sana, tafadhali tushirikishe kupitia mitandao ya kijamii – Facebook, Twitter au Instagram na tumia hashtag #UberHEROES