Habari

Afrika, tunakusherehekea wewe!

Tarehe 23 Mei, 2018 / Tanzania

Hii ni kwa ajili yako Afrika!Tumekuwa tukikusafirisha kwa takribani miaka mitano sasa, na imekuwa safari moja nzuri sana kwetu!

Ilianza kwa kubonyeza kitufe tu, lakini kwa sasa imekuwa zaidi ya hiyo – tumezunguka miji mipya pamoja, tumekufikisha kwenye matukio muhimu kwa wakati na pia fursa nyingi za kiuchumi zimetengenezwa.

Umekuwa nasi ukiwa unaenda kwenye vikao vyako, kuenda kukutana na uwapendao, katika mitoko yako ya wikiendi na zaidi ya yote umeturuhusu tukurudishe nyumbani. Tunashukuru kwa kuwa nasi katika kipindi chote hiki – tusingeweza kufika hapa bila wewe.

Tuangalie tumetoka wapi, na zaidi ya yote tunaelekea wapi tukiwa pamoja.

Safari ndio kwanza imeanza! #UberMovesAfrica