Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Weka nafasi ya safari ukitumia Uber mapema katika Adolfo Suárez Madrid-Barajas Airport

Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya safari ukitumia Uber kwenda Adolfo Suárez Madrid-Barajas Airport. Omba safari hadi siku 30 kabla ya safari yako ya ndege, wakati wowote na siku yoyote ya mwaka.

Mahali unakoenda
Chagua tarehe na saa

Date format is yyyy/MM/dd. Press the down arrow or enter key to interact with the calendar and select a date. Press the escape button to close the calendar.

Selected date is 2023/09/19.

10:29 PM
open

Huenda huduma ya kuweka nafasi isipatikane katika eneo lako la kuchukuliwa

Omba safari kote ulimwenguni

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 600.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

 • Uber Metropolitano

  1-4

  Fixed price for trips from and to the station

 • Uber Pet

  1-3

  Ride with your pet

 • UberX Saver

  1-4

  Chaguo jipya la safari lenye nauli za chini kwenye VTC na Taxi

 • Uber for Morocco

  1-4

  The Uber for Morocco fare is €1 higher compared to an UberX trip ordered at the same time for the same route. €1 from each trip on Uber for Morocco is not part of the fare, but is the amount that Uber B.V. sends to the Red Cross in support of the humanitarian response to the earthquake in Morocco. Red Cross does not endorse any company, brand, product or service.

 • Kijani

  1-4

  100% electric rides at the same price as UberX

 • UberX

  1-4

  Affordable rides with VTC and Taxi

 • Black

  1-4

  High end cars with top-rated drivers

 • Raha

  1-4

  Magari mapya zaidi yaliyo na nafasi ya kutosha

 • Gari aina ya Van

  1-6

  High end cars for 6 with top-rated drivers

1/9

Chukua msafiri katika Adolfo Suárez Madrid-Barajas Airport (MAD)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa MAD linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Madrid moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Adolfo Suárez Madrid-Barajas Airport.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la MAD kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Madrid, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

 • Maeneo ya kuchukua wasafiri wa Uber katika viwanja vya ndege yanaweza kubadilika, kwa hivyo ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia App yako ya Uber kila baada ya kuitisha usafiri.

 • Ada za safari za Uber kwenda na kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Madrid zinaweza kuathiriwa na wakati, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa Uber wa kukadiria nauli kwenye App ya Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

 • Unapoitisha usafari, App itakupa makadirio ya muda ambao dereva atachukua kufika katika eneo la kuchukua wasafiri.

Taarifa zaidi

 • Unaendesha gari ukitumia Uber?

  Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

 • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

  Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Madrid

Safari za kwanza za ndege za kibiashara ziliondoka Uwanja wa Ndege wa Madrid mwaka 1933. Kuanzia wakati huo, uwanja huo umekuwa mojawapo ya vituo muhimu kwa watalii wanaoingia Uhispania. Kila mwaka, MAD hupokea takribani wasafiri milioni 58 na kushughulikia zaidi ya safari 400,000 za ndege. Uwanja wa Ndege wa Madrid-Barajas uko takribani kilomita 15 (maili 9) kaskazini mashariki mwa eneo la katikati ya jiji la Madrid, safari ya takribani dakika 20, hivyo kufanya Uber iwe chaguo bora la usafiri wako.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Madrid

Uwanja wa Ndege wa Madrid una vituo 5: T1, T2, T3, T4 na T4S. Vituo vyote vinashughulikia safari za kimataifa, kitaifa, za Schengen na zisizo za Schengen. Kuna usafiri wa basi bila malipo kwa ajili ya kuwapeleka wasafiri katika vituo mbalimbali.

Migahawa katika Uwanja wa Ndege wa Madrid

MAD ni uwanja mkubwa wa ndege ambao una aina mbalimbali za vyakula kwa wasafiri, iwe unataka mlo mkuu, kinywaji cha kukuburudisha au kitafunwa chepesi kabla au baada ya safari yako. Uwanja huu una migahawa kadhaa yenye vyakula unavyoweza kujichagulia yakiwemo mapishi kutoka duniani kote kama vile vyakula vya Kijapani, Kifaransa, bila kusahau Tapas na vyakula vingine vya Kihispania. Ikiwa huna muda wa kula ndani ya mgahawa, kuna aina kadhaa ya vyakula vya kufungashwa kama vile sandwichi, aina kadhaa za maandazi, saladi na vitafunwa vingine vitamu, vilevile kuna vyakula vya kuchukua haraka kama vile chipsi na baga. Pia kuna baa kadhaa zinazouza bia, mivinyo na pombe za mchapalo.

Maduka katika Uwanja wa Ndege wa Madrid

Wanaopenda ununuzi wa rejareja watafurahia maduka yaliyo katika Uwanja wa Ndege wa Madrid, hasa sehemu ya msururu wa maduka ya bidhaa zisizotozwa kodi, ambayo ndiyo sehemu kubwa kabisa Uhispania na ina bidhaa za kiwango cha kimataifa zinazouzwa kwa bei nafuu. Katika maeneo yote ya uwanja wa ndege kuna maduka yanayouza vifaa vya mavazi, nguo, mapambo, saa, vifaa vya kielektroniki, vifaa muhimu kwa ajili ya usafiri na hidaya. Mashabiki wa Kandanda pia wanaweza kuzuru sehemu ya maduka ya bidhaa za michezo ili kupata bidhaa mahususi za Real Madrid.

Kumbi katika Uwanja wa Ndege wa Madrid

Ikiwa una muda kabla ya safari yako, unaweza kufurahia kumbi kadhaa zilizo katika MAD ambapo wasafiri wanaweza kufanya kazi au kupumzika kwa muda. Vituo vyote vina kumbi ambapo wasafiri wote wanaweza kukaa kwa kulipia kiasi fulani cha ada, ikiwa ni pamoja na familia zilizo na watoto. Huduma zinazopatikana ni pamoja na vinywaji na vyakula baridi na moto, magazeti na majarida, bafu, viti vya kujimwaya na Wi-Fi bila malipo.

Huduma katika MAD

Uwanja wa Ndege wa Madrid una huduma mbalimbali kwa wasafiri ili kuwawezesha kuwa na safari njema bila usumbufu. Familia zinazosafiri pamoja na watoto wachanga zinaweza kupata maeneo ya kuchezea, kumbi za kunyonyeshea watoto, vijigari vya kusukumia watoto na kipaumbele katika ukaguzi wa usalama. Kuna huduma za usaidizi kwa watu walio na matatizo ya kutembea, lakini ni sharti huduma hiyo iombwe angalau saa 48 kabla ya wakati wa ndege kuondoka. Wanaosafiri kibiashara wanaweza kutumia sehemu za kufanyia kazi na vyumba vya mikutano na mawasilisho.

Hoteli katika Uwanja wa Ndege wa Madrid

Kuna aina mbalimbali za sehemu za kulala karibu na uwanja wa ndege. Ikiwa ndege yako haitaondoka asubuhi sana, kuna mamia ya hoteli jijini Madrid, zinazoweza kufikiwa kwa urahisi kwa kutumia mfumo wa Uber kutoka kwenye uwanja wa ndege.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Madrid

Madrid ndilo jiji kuu la Uhispania na wageni wanaweza kuzuru bustani, medani na barabara mbalimbali za jiji. Licha ya kuwa makao ya mojawapo ya vilabu maarufu zaidi vya soka duniani, Madrid ina sanaa, mijengo na migahawa mingi. Baadhi ya vivutio ni pamoja na:

 • Museo del Prado
 • Parque del Buen Retiro
 • Real Academia de Bellas Artes de San Fernando
 • Jumba la muziki la Teatro Real

Pata maelezo zaidi kuhusu MAD hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji. Uokoaji wa pesa kwenye ofa unatumika kwa watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Ofa na masharti yanaweza kubadilika.