Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Weka nafasi ya safari ukitumia Uber mapema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul

Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya safari ukitumia Uber kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul. Omba safari hadi siku 30 kabla ya safari yako ya ndege, wakati wowote na siku yoyote ya mwaka.

Mahali unakoenda
Chagua tarehe na saa

Date format is yyyy/MM/dd. Press the down arrow or enter key to interact with the calendar and select a date. Press the escape button to close the calendar.

Selected date is 2023/09/19.

10:29 PM
open

Huenda huduma ya kuweka nafasi isipatikane katika eneo lako la kuchukuliwa

Omba safari kote ulimwenguni

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 600.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

 • Large Taxi

  1-8

  Fare according to meter in taxi, pay in cash or credit card

 • Courier

  1-4

  Tuma na upokee vifurushi

 • Teksi ya Njano

  1-4

  Fare according to meter in taxi, pay in cash or credit card

 • CloneTaxiYellow

  1-4

  Fare according to meter in taxi, pay in cash or credit card

 • Turquoise Taxi

  1-4

  Fare according to meter in taxi, pay in cash or credit card

1/5

Chukua msafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul (IST)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa IST linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata maelekezo kwenye programu

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Istanbul Airport moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la IST kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul, kwa hivyo unaweza kufurahia safari ya starehe na inayokufaa hadi popote unapotaka kwenda.

 • Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

 • Hata ingawa safari si ndefu sana, ada za Uber za kwenda na kurudi kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul bado zinaweza kuathiriwa na wakati, msongamano wa magari na sababu nyingine. Angalia kikadiriaji cha nauli cha Uber ili ufahamu makadirio ya nauli za safari.

 • Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Taarifa zaidi

 • Unaendesha gari ukitumia Uber?

  Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

 • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

  Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Taarifa kwa wageni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul

Uber inafaa kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul. Ukiwa uwanja wa ndege ulio mkubwa zaidi nchini Uturuki kwa kuzingatia idadi ya wasafiri, IST ndio uwanja wa ndege ulio katika nafasi ya 2 kote ulimwenguni wenye safari nyingi zaidi za moja kwa moja. Kuendesha gari kutoka katikati ya jiji la Istanbul hadi Uwanja wa Ndege wa IST kunachukua takribani dakika 40 na kunafanya uwanja huu kuwa chaguo bora kwa yeyote anayesafiri kuingia au kuondoka Istanbul. Kwa wasafiri ambao hawana gari, ni rahisi kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul kupitia treni ya chini ya ardhi, basi au Uber.

Vituo vya Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Uwanja wa Ndege wa Atatürk una vituo 2 vya wasafiri: Kituo cha Safari za Nchini na cha Safari za Kimataifa. Kama unavyotarajia, Kituo cha Safari za Nchini kinashughulikia safari za ndege za nchini Uturuki ilhali Kituo cha Safari za Kimataifa kinashughulikia safari za ndege za kimataifa na kimabara. Vituo hivi 2 vimeunganishwa, hivi kwamba vimerahisisha usafiri wa ndani ya nchi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul ikilinganishwa na viwanja vingine vya ndege vyenye ukubwa sawa. Wi-Fi inapatikana katika vituo vyote viwili na unaweza kupata vituo vya kuchaji simu kila mahali kwenye uwanja huu wa ndege.

Kituo cha Safari za Nchini

 • Turkish Airlines
 • Primeclass Lounge

Kituo cha Safari za Kimataifa

 • Air France
 • Emirates
 • Safari nyingine za kimabara na kimataifa
 • HSBC Premier Lounge

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Kuanzia machaguo ya vyakula visivyosindikwa, vya kienyeji hadi vyakula vinavyotayarishwa upesi, kuna mikahawa mingi tofauti ya kuvinjari kwenye Uwanja wa Ndege wa IST. Iwe ungependelea kufurahia mtindo wa vyakula mbalimbali au chakula cha haraka, kuna machaguo mengi yanayopatikana yenye kitu kinachomfaa kila mtu.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Vituo vya Safari za Nchini na za Kimataifa vimekaribiana sana, kwa hivyo unaweza kutoka kwenye kituo kimoja hadi kingine kwa miguu au kijia kinachosonga—ambayo ni bora zaidi ikiwa una haraka.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Kivutio kikuu katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul ni maeneo yake mazuri ya ununuzi, kuanzia duka kubwa la bidhaa zisizotozwa ushuru hadi Old Bazaar, ambapo unapoweza kupata bidhaa halisi za Uturuki kama vikolezo, vifaa vya glasi na vito. Maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul ni sehemu bora ya kuwanunulia marafiki na familia yako hedaya na bidhaa mbalimbali kama vile pombe, mapambo, marashi na hata pipi. Shughuli nyingine zinajumuisha huduma za spa na ukandaji wa mwili—ambazo zinafaa kwa ajili ya kujituliza kabla ya safari—huku kumbi nyingine zikiwa na mabafu.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Kuna hoteli moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Istanbul na nyingine nyingi karibu nayo, ambazo zinafaa kwa watu wanaowasili kwenye uwanja huu wa ndege alfajiri. Vituo vya kawaida vya biashara, vyumba vya mikutano, mikahawa na vyumba vya mazoezi vinaweza kupatikana kwenye hoteli hizi, lakini ni vyema kuchunguza kwa makini kwenye tovuti ya hoteli ili kuhakikisha ina kila kitu unachohitaji.

Maeneo ya kupendeza karibu na Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Kuna maeneo mbalimbali ya kupendeza ya kihistoria karibu na IST, kama ilivyo kwenye uwanja wowote wa ndege huko Istanbul, ikiwemo:

 • The Blue Mosque
 • Mnara wa Galata
 • Grand Bazaar
 • The Hagia Sophia
 • Kasri ya Topkapi

Pata taarifa zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Istanbul hapa.

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji. Uokoaji wa pesa kwenye ofa unatumika kwa watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Ofa na masharti yanaweza kubadilika.