Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Phoenix-Mesa Gateway (AZA)

Safiri kwenda na kutoka Uwanja wa Ndege wa Mesa ukitumia Uber. Badala ya kusubiri basi la AZA au teksi, unaweza kuomba safari moja kwa moja kwenye programu na utakuwa safarini.

Mesa, AZ 85212
+1 480-988-7600

search
Unatoka wapi?
Navigate right up
search
Unaenda wapi?

Omba usafiri ukiwa eneo lolote duniani

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

Utachukuliwa katika uwanja wa ndege wa Uwanja wa Ndege wa Phoenix-Mesa Gateway (AZA)

Itisha usafiri

Chagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Angalia App ili upate maelezo

Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha. Fuata masharti kwenye App umkute dereva wako kando ya barabara au katika sehemu maalum ya kuchukuliwa.

Thibitisha mahali ulipo

Nenda kwenye eneo lililobainishwa la kuchukuliwa kama lilivyo kwenye App (tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe karibu zaidi na lango la kuondoka) Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

    Taarifa zaidi

    • Unaendesha gari ukitumia Uber?

      Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

    • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

      Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

    1/2

    Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Mesa

    Uwanja wa Ndege wa Phoenix-Mesa Gateway, unaopatikana Mesa, Arizona, unahudumia zaidi ya wasafiri milioni 1.3 kila mwaka. Kwa kawaida, itakuchukua muda wa takriban dakika 25 kwenye gari kufikia Uwanja wa Ndege wa AZA ambao uko umbali wa maili 20 (kilomita 32) kutoka katikati mwa jiji la Mesa. Itakuchukua muda wa takribani dakika 40 kwenye gari kutoka katikati mwa mji wa Phoenix, ambao uko umbali wa maili 38 (kilomita 61) kutoka uwanja huu wa ndege.

    Kituo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mesa

    Kituo cha Charles L. Williams, ambacho ni kituo kikuu cha wasafiri kwenye uwanja huu wa ndege, kina milango mikuu, maduka ya ununuzi na maeneo ya kula. Mashirika 3 ya ndege yanahudumu kwenye uwanja wa ndege wa AZA: Allegiant, Swoop na WestJet. Kwa sababu ndege nyingine ni za kimsimu na zinaweza kubadilishwa, tembelea tovuti ya shirika la ndege uone maelezo mapya ya kuweka nafasi ya ndege.

    Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Mesa

    Wasafiri wanaweza kuchagua kati ya maeneo mengi ya kununua chakula kwenye Uwanja wa Ndege wa Mesa. Aina za vyakula zinajumuisha migahawa inayotayarisha vyakula vya Kimarekani; mgahawa unaouza vyakula mbalimbali na bidhaa zilizookwa ikiwemo vinywaji vya kahawa; na duka la zawadi linalouza vitafunwa na vinywaji baridi.

    Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Mesa

    Kwa wasafiri wanaopenda kununua bidhaa, Uwanja wa Ndege wa Phoenix-Mesa Gateway una maduka 2 yanayouza bidhaa mbalimbali zikiwemo, vitabu, hedaya, zawadi na vitafunwa.

    Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Mesa

    Iwe unasubiri ndege nyingine au safari yako ya usiku imechelewa, au unahitaji mahali pa kutulia kwa muda karibu na Uwanja wa Ndege wa Phoenix-Mesa Gateway, utapata hoteli na vyumba vingi vya kulala karibu na Chandler, Mesa, Phoenix na maeneo mengine.

    Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Mesa

    • Papago Park, Phoenix
    • Rose garden, Mesa
    • Usery Mountain Regional Park, Mesa

    Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu AZA hapa.

    Facebook
    Twitter

    Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa mara kwa mara. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au huduma zake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji.