Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol (AMS)
Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Amsterdam au teksi? Iwe unasafiri kutoka Schiphol hadi katikati ya jiji la Amsterdam au kutoka katikati ya jiji la Amsterdam hadi Schiphol, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka AMS kwa kubofya kitufe.
Schiphol, 1118 CP+31 20-794-0800
Request a ride around the world
Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.
Safiri kama mkazi
Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.
Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber
Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.
Ways to ride in the area
Pickup at Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol (AMS)
Fungua programu yako ili uombe safari
Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa AMS linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.
Fuata maelekezo kwenye programu
Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri ya Uwanja wa Ndege wa Amsterdam moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo. Ishara za maeneo ya kuchukua wasafiri wanaosafiri pamoja zinaweza pia kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol.
Kutana na dereva wako
Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la AMS kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.
Top questions from riders
- Je, ninaweza kuitisha usafiri wa Uber katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam?
Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.
- Eneo la kuchukua wasafiri wa Uber katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam liko wapi?
Down Small Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.
- Je, safari ya Uber kutoka Schiphol kuelekea Amsterdam itagharimu pesa ngapi?
Down Small Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Schiphol zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.
- Itachukua muda gani kuchukuliwa na Uber?
Down Small Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.
More information
Unaendesha gari ukitumia Uber?
Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.
Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?
Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.
Vituo katika uwanja wa Schiphol: unachofaa kufanya
Uber ndiyo chaguo bora ya kusafiri kuenda na kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol (AMS). Itakuchukua dakika 20 kufika Uwanja wa Ndege wa Schiphol kutoka katikati mwa jiji la Amsterdam. Hupatikana kwa urahisi na wasafiri wa kwenda na kuondoka mji wa Amsterdam. Njia za usafiri katika Uwanja wa Ndege wa AMS ni pamoja na treni, basi na teksi huhakikisha kuwa wasafiri na wakaazi wengine wa Uholanzi wanapata huduma bora. Uber pia inapatikana ili kukuwezesha kufika unakoenda kwa urahisi.
Vituo katika Schiphol
Uwanja wa Ndege wa Schiphol una kituo kimoja kikuu cha wasafiri kilichoagawanywa katika ghorofa 3. Katika ghorofa ya chini ya Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Schiphol, utapata eneo la wanaowasili, pamoja na migahawa, maduka makuu na huduma nyingine mbalimbali zikiwemo vyumba vya mapumziko na ususi. Ghorofa ya 2 ina maeneo ya kukaguliwa na kuondoka, ilhali daraja ya 3 iina maeneo ya sebule za VIP. Ndege zinazoondoka katika uwanja wa Ndege wa AMS zinajumuisha:
- Croatia
- Delta
- HOP!
- Jet2.com
- United
Migahawa ya Uwanja wa Ndege wa Schiphol
Uwanja wa Ndege wa Amsterdam Schiphol una sehemu mbalimbali za kula na kunywa, zikiwemo vibanda vya vyakula, migahawa na baa. Uwanja wa ndege wa Amsterdam una aina nyingi za vyakula kutoka kila bara, vikiwemo vyakula kutoka Mediterania na Vyakula halisi vya Uholanzi. Kwa hivyo, huwezi kukosa mlo unaotaka.
Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa AMS
Kwa kuwa kuna kituo kimoja tu cha wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa Schiphol, ni rahisi kutembea.
Mambo unayoweza kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa AMS
Utapata bidhaa za kipekee kama vile wanasesere, vidude vya kuchezea, jibini na chokoleti wakati wowote kwenye maduka ya Uwanja wa Ndege wa Schiphol. Kabla ya kuondoka kwa ndege, mbona usimnunulie unayempenda zawadi? Utapata aina ya mapambo na vipodozi kochokocho kwenye maduka ya Uwanja wa Ndege wa Amsterdam. Isitoshe, kutokana na kuwepo kwa maduka mengi yanayouza bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam, AMS ni mahali bora zaidi pa kununua zawadi maridadi kwa ajili ya ndugu na marafiki kwa bei nafuu.
Kubadilisha sarafu kwenye Uwanja wa Ndege wa Schiphol
Kibanda cha kubadilisha sarafu katika ABN AMRO Exchange Schiphol kinakuwezesha kubadilisha aina 60 za sarafu. Kinamfaa mtu yeyote anayetaka kuwa na pesa chache taslimu kabla ya kuzuru Amsterdam. Hutatozwa ukibadilisha kiasi kisichopungua Yuro 200; ikiwa unabadilisha chini ya kiasi hicho, utahitaji kulipa ada ndogo. Kwa hivyo ni bora kubadilisha pesa nyingi ikiwa unapanga kukawia.
Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Amsterdam
Migahawa mingi inafikiwa kupitia usafiri wa Uber katika Uwanja wa Ndege wa AMS. Pia kuna migahawa mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Amsterdam ambako unaweza kwenda kwa miguu. Kwa hivyo wakati wowote unapowasili, iwe unawasili alfajiri au usiku wa manane, una uhakika wa kupumzika. Isitoshe, kuna vituo vya biashara vinavyopatikana katika migahawa mingi. Vituo hivi vinawafaa wafanyabiashara popote walipo.
Sehemu za kuzuru karibu na Schiphol
Wakati unasubiri ndege nyingine katika Uwanja wa Ndege wa Schiphol, kuna mambo mengi unayoweza kufanya, haswa ikiwa unaweza kuzuru mji wa Amsterdermr:
- Anne Frank House
- Dam Square
- Rijksmuseum
- Royal Palace
Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa AMS hapa.
This page contains information from third-party websites that are not under the control of Uber and that may be periodically changed or updated. Any information included on this page that is not directly related to Uber or its operations is for informational purposes only and in no way shall be relied upon, or interpreted or construed to create any warranties of any kind, either express or implied, regarding the information contained herein. Certain requirements and features vary by country, region, and city.
Kuhusu